Habari rafiki?

Kipo kitu kimoja ambacho nimekuwa nawashauri watu wote ambao ninawakochi, kuwashauri au hata kuwa na mazungumzo nao ya aina yoyote ile. Kitu hicho ni kupiga hatua na kukua zaidi kwenye chochote ambacho mtu anafanya.

Nimekuwa nasisitiza sana umuhimu wa watu kukua, mtu aanzie hatua ya chini na kuendelea kupiga hatua. Na siyo kubaki pale alipoanzia na kuridhika kwa sababu ameshapata kile alichokuwa anataka kwa mwanzoni.

Huwa nashangazwa sana na watu wanaoanza biashara ndogo, lakini miaka inaenda na biashara iko vile vile, haijakua na wala haijazalisha biashara nyingine zaidi.

Kuna fursa nyingi sana za kukua kwenye biashara, kazi na chochote tunachofanya. Na hili ndiyo nimekuwa nalishauri, kwa sababu kwenye maisha kama hukui basi unakufa, hakuna kusimama.

Na msimamo wangu kwenye ushauri ni kwamba mtu unapaswa kutoa ushauri ambao unauishi wewe, au unafanya. Kushauri kitu halafu wewe kufanya kinyume na kile unachoshauri haifai.

Hivyo mambo yote ambayo nimekuwa nashauri kupitia mafunzo mbalimbali ninayotoa, ndivyo ninavyofanya na kuishi, au nimewahi kufanya, au kama nikipata nafasi hiyo nitafanya hicho ninachoshauri.

Lakini kuna eneo moja ambalo nitashindwa kufuata ushauri wangu mwenyewe, na inabidi nikueleze wazi ili usije kushangaa unapokutana na usichotegemea.

Eneo hilo ni UKUAJI WA KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni huduma ya mafunzo ninayoitoa, ambapo kuna kundi la wasap ambapo kuna mafunzo mengi sana natoa kila siku na mijadala ya kujifunza na kuhamasika. Pia kuna blog ya KISIMA CHA MAARIFA ambayo ina makala nyingi nzuri, ambapo unaweza kusoma kama ni mwanachama tu.

Mipango yangu mara zote kupitia KISIMA CHA MAARIFA ni kuweza kuwafikia wengi zaidi na wao kunufaika. Kwa sababu wengi ambao wamekuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, wanaeleza wazi kwamba imekuwa ni sehemu nzuri kwao kujifunza.

Kutokana na manufaa haya ya KISIMA CHA MAARIFA, kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA limejaa. Uwezo wa kundi la wasap ni kuchukua watu 256 pekee, huwezi kuweka watu zaidi ya hapo. Na kwa sasa kundi hili limejaa watu hao 256.

KISIMA CHA MAARIFA

Hivyo kwa akili za kawaida za kibiashara, kinachopaswa ni kufungua kundi jingine na kuendelea kuunganisha watu. Hivi ndivyo huduma inavyokua na kuwafikia wengi zaidi. Lakini mimi sitaweza kufanya hivyo. Sitakuza huduma hii kwa kundi zaidi ya moja.

KISIMA CHA MAARIFA kitabaki kuwa kundi moja pekee la wasap, na watu watakapohitaji kujiunga zaidi watasubiri mpaka nafasi zitakapopatikana.

Nimefanya hivi kwa sababu ninaweza kuweka muda wangu na nguvu zangu kwa uhakika kwenye kundi moja pekee, zaidi ya hapo ufanisi wangu utashuka. Ninaamini ni bora kufanya vitu vichache, ni bora kuwahudumia watu wachache vizuri kuliko kufanya mengi kwa kawaida. Kawaida ni sumu, ni kitu ambacho siruhusu kwenye maisha yangu.

Zipo njia mbadala za kuweza kupokea watu wengi zaidi, kuna mitandao kama Telegram ambayo inaweza kupokea mpaka watu elfu 5. Lakini tumeijaribu telegram na imekuwa changamoto kwa wengi. Kwa kipindi kidogo ambacho tulijaribu kuendesha KISIMA CHA MAARIFA kupitia TELEGRAM, wengi walikuwa wanakosa mambo mengi na mazuri. Hivyo baada ya kufanya tathmini, nilichoona ni mtandao wa wasap ni rahisi kwa wengi kupata mafunzo haya.

Hivyo rafiki, tutabaki na kundi moja la watu 256 pekee kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo mtu yeyote atakayehitaji kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, atakaa kwenye orodha ya wanaosubiria nafasi zikipatikana. Nafasi zitakuwa zinapatikana kwa sababu kuna vigezo vya mtu kufikisha ili kuendelea kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ambaye hafikishi vigezo hivyo anaondolewa.

Maamuzi haya niliyofikia, kibiashara ni maamuzi ya hovyo kabisa, ni kuamua kujiwekea ukomo kwenye kipato. Lakini kwangu mimi KISIMA CHA MAARIFA ni zaidi ya biashara, ni huduma muhimu, ni damu yangu, ni mimi mwingine. KISIMA CHA MAARIFA ni kitu ambacho nakifanyia kazi kubwa kiweze kuwa sehemu ya mabadiliko yenye tija kwa wengi. Ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ambayo ni tsh elfu 50 siyo ada inayokidhi thamani ambayo mtu anaipata kwa kujiunga na KISIMA, bali ni kiasi tu ambacho watu wanachangia ili huduma hii iweze kuendelea.

Je wale ambao hawapati nafasi ya kuingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA mara moja wananufaikaje?

Kutaendelea kuwa na makala bora zaidi kwenye AMKA MTANZANIA kila siku, hii ni sehemu ya kujifunza bure kabisa, na mtu anaweza kujifunza mengi.

Nitaendelea kutoa vitabu vingi sana, mpango ni kutoa angalau kitabu kimoja kila mwezi kwa mfumo wa softcopy, hivyo kutakuwa na mengi sana ya kujifunza.

Pia nina huduma ya PERSONAL COACHING ambayo ninaitoa, mwanzoni nilikuwa nimeiweka kwa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA pekee, lakini kwa sasa ipo wazi kwa wote, ni sehemu ya kunufaika sana.

Nafasi Tatu (3) za PERSONAL COACHING kwa mwezi january 2018.

Kila mwezi nimekuwa natoa nafasi tano za kufanya kazi na mtu mmoja mmoja katika kumsaidia kupiga hatua kwenye maisha yake. Hapa mtu anakuja na changamoto inayomkabili au hatua anayotaka kupiga lakini yeye mwenyewe anashindwa kujisukuma kuchukua hatua, kwa mwezi mmoja tunafanya kazi pamoja na mtu anaweza kupata matokeo bora kabisa.

Napenda kuwataarifu kwamba nafasi za COACHING kwa mwezi januari zimebaki tatu pekee, mbili tayari zimeshachukuliwa na watu. Hivyo kama unahitaji tufanye kazi pamoja kwa changamoto yoyote au hatua yoyote unayotaka kupiga, una nafasi ya kuchukua hatua sasa.

Ada ya coaching kwa kipindi hicho cha mwezi mmoja ni tsh 100,000/=. Kama upo tayari kwa coaching kwa mwezi januari tuwasiliane kwa wasap 0717396253 tuweze kupanga coaching itakwendaje.

Zawadi ya mwaka mpya kwako rafiki yangu.

Wakati naenda likizo yangu ya mwisho wa mwaka 2017, nilitoa zawadi ya vitabu vyote nilivyoandika kwa mfumo wa softcopy. Mtu alikuwa analipia tsh 30,000/= na kupata vitabu vyote. Hii ni gharama ndogo sana kwa vitabu na maarifa hayo. Muda nilioutoa wa kupata zawadi hii ulikuwa mfupi hivyo wengi walikosa nafasi hii.

Baada ya maombi ya wengi, nimeona ni vyema kuitoa tena zawadi hii na kuwapa watu nafasi ya kuweza kuipata. Hivyo zawadi ya vitabu itaendelea kupatikana mpaka tarehe 01/01/2018.

Kama bado hujapata zawadi hii, una nafasi ya kuchukua hatua sasa.

Maelezo zaidi ya zawadi ni kama ifuatavyo;

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI; Sababu 25 kwa nini unaendelea kuwa masikini. Bei ya hichi ni tsh elfu 5.
  2. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA; Maandalizi na njia bora ya kunufaika na mabadiliko kwenye maisha, kazi na biashara. Bei yake tsh elfu 5.
  3. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, Jiajiri na utajirike kupitia mtandao wa intaneti. Bei yake elfu 10.
  4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016; Nidhamu, Uadilifu Na Kujituma. Bei yake ni tsh elfu 10.
  5. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Anzisha na kuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Bei yake tsh elfu 10.
  6. MIMI NI MSHINDI; Ahadi yangu na nafsi yangu. Bei tsh elfu 10.
  7. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU; dhibiti muda wako ili uweze kufanya zaidi. Bei yake tsh elfu 5.
  8. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING); Miliki biashara kubwa kwa kuanza na mtaji kidogo. Bei tsh elfu 5.

Kupata zawadi hii, tuma fedha tsh 30,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 (majina AMANI MAKIRITA) kisha nitumie ujumbe kwenye moja ya namba hizo wenye maneno zawadi ya vitabu ukiwa umeambatanisha na email yako kisha nitakutumia vitabu hivyo nane kwenye email yako.

MUHIMU; Zawadi hii ni kwa kipindi hichi cha mwaka mpya pekee, itapatikana mpaka tarehe 01/01/2018, hivyo chukua hatua sasa uweze kupata vitabu hivi vizuri.

Asante sana rafiki yangu kwa kuwa pamoja kwa kipindi chote hichi, na karibu sana tuendelee kuwa pamoja, tukijifunza na kuhamasika ili kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yetu.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog