Habari ya leo mpendwa rafiki? Hongera sana kwa zawadi nzuri ya siku hii ya leo lakini pia heri ya mwaka mpya wa 2018.  Karibu sana rafiki tuendelee kujifunza kupitia mtandao wetu Amka Mtanzania.

Kumbuka kuiendea siku hii ya leo kwa misingi yetu ya maisha ya mafanikio ambayo ni nidhamu, uadilifu na kujituma.

Maisha Hayajawahi

Kila mtu anapenda kusikiliza hadithi za mafanikio. Kila mtu anapenda kuona matokeo ya mafanikio fulani. Kiufupi watu wengi wanapenda sana siyo kusikia, kuona na hata kuwa nayo kabisa mafanikio yenyewe.

Licha ya watu wengi kupenda mafanikio lakini kuna kitu ambacho watu wengi hawataki kukisikia kabisa katika safari ya mafanikio. Kitu ambacho watu wengi hawataki kukisikia kabisa katika safari ya mafanikio ni mchakato.

Watu hawapendi kusikia kuhusu mchakato bali wanapenda kusikia tu juu ya matokeo ya kitu fulani. Ni rahisi kusikiliza hadithi za mafanikio ya mtu fulani lakini ukiambiwa mchakato wake aliopitia na wewe sasa upitie hapo ndipo panakuwa pagumu. Kwa mfano, unasoma hii makala lakini na kuifurahia lakini kama ungejua mchakato wake mpaka wewe inakufikia hapo ulipo basi kuna gharama kubwa ambayo imelipiwa na huenda hata wakati na andika hapa wewe umelala lakini ukija kumweleza mtu    mchakato huo hataki kusikia hadithi hizo.

SOMA; Hii Ndiyo Sababu Kuu Moja Kwanini Watu Wanaajiriwa Au Wanajiajiri Katika Maisha Yao.

Kumbe basi, watu wanapenda mafanikio lakini hawataki kuweka kazi, hawataki kupitia katika mchakato wa kuelekea katika mafanikio. Kwa mfano, unataka kuwa mtu fulani labda unataka kujenga jina lako kupitia katika uandishi lakini hutaki kuandika, hutaki kujifunza, hutaki kuwa na nidhamu binafsi ila wewe unataka tu kufurahia tayari umeshakuwa na mafanikio katika nyanja fulani.

Rafiki, kitu kigumu sana katika safari ya mafanikio yoyote yale ni mchakato. Muulize mtu yeyote aliyefanikiwa katika kitu fulani atakuambia ni jinsi gani mchakato unakuwa mgumu lakini kwa sababu mafanikio ni haki yetu ya kuzaliwa lazima tukubali kulipia gharama ili tuweze kuyapata.

Hatua ya kuchukua leo, kama unataka mafanikio yoyote yale basi kubali kulipia gharama za mchakato. Ukikimbia mchakato wa kupata mafanikio yoyote yale sahau kuhusu mafanikio unayoyatafuta.

SOMA; Tofauti Hizi Tano Za Matumizi Ya Muda Kwa Matajiri Na Masikini Ndiyo Zinawatofautisha Matajiri Na Masikini.

Hivyo basi, kwa chochote unachofanya unatakiwa uwe mtu wa subira, usitegemee hata kama unapitia mchakato fulani na mambo yatabadilika papo kwa papo. Ni swala la muda kwani muda hutibu kila kitu.

Kila la heri rafiki yangu, ukawe na siku bora sana yenye furaha na mafanikio makubwa.

Rafiki na Mwalimu wako,

Deogratius Kessy

Unaweza kuwasiliana nami kupitia;

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com, kessydeo @mtaalamu.net

Au unaweza kutembelea mtandao wangu http://www.mtaalamu.net/kessydeo kujifunza zaidi.

Asante sana.