Mpendwa rafiki,

Tumekuwa tukiona msimu wa sikukuu watu wengi sana wakifanya shopping mbalimbali kama vile nguo na mahitaji mengine. Kila mwaka watu wako tayari kufanya shopping za mwili lakini kuna shopping nyingine moja iliyosaulika siku hizi.

tai lopez

Kila msimu wa sikukuu watu wanakuwa napilika pilika za kuhakikisha anafanya shopping ya mahitaji yake muhimu huenda ikawa ni kwa ajili yake binafsi, familia au ndugu nakadhalika. Unaweza kukuta nyumba imejengwa vizuri lakini ukiingia ndani hakuna sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili ya maktaba ndogo ya vitabu. Hata baadhi ya ofisi nyingine ukienda huwezi kukuta mhusika anaweka baadhi ya vitabu vyake katika shelf ya kujisomea akiwa pale eneo lake la kazini.

Kwahiyo rafiki, shopping adimu sana kupatikana katika jamii yetu ni shopping ya akili. Watu wanafanyia shopping miili yao lakini wanashindwa kuifanyia shopping akili zao. Ni adimu sana kukuta mtu anaenda duka la vitabu kufanya manunuzi ya vitabu kwa ajili ya akili yake. Watu wamekuwa ni watu wa kuficha miili yao huku wakiacha akili zao zikiwa uchi.

Akili ndiyo iliyobeba mwili lakini tunakubali kuziacha uchi akili zetu kwa kutozifanyia shopping kama vile tunavyofanyia miili yetu. Matokeo yake mtu mwili unakuwa safi lakini akili ni chafu kwa sababu kile kinachoingia ndicho kinachotoka. Ingekuwa tunapigania kuwa smarti katika akili kama vile tunavyopigania kwenye shopping za mwili basi leo hii tungekuwa mbali sana.

Mpendwa msomaji, nakualika ujenge utamaduni wa kusoma vitabu, jenga utamaduni wa kununua vitabu noa akili yako kwani akili ikiwa safi na mwili utakua safi. Niliwahi kuandika kuwa ni afadhali ukonde kimwili kuliko kukonda kiakili. Ukikonda kiakili ni mbaya zaidi kuliko kukonda kimwili, akili yako iko safi itafanya mambo masafi lakini ikiwa chafu itafanya machafu.

SOMA; Hii Ndiyo Nyumba Adimu Sana Kupatikana Katika Zama Hizi Za Taarifa.

Ukitaka kuweza kumbadilisha mtu basi mjengee utamaduni wa kujisomea vitabu yaani atabadilika yeye mwenyewe kwa sababu kupitia vitabu vinamfanya mtu afanye tafakari ya akili hivyo ataweza kujigundua na kutambua mambo muhimu. Unaweza ukajiona unajua kila kitu lakini kama ukitaka kuona wewe hujui basi anza kujifunza leo ndiyo utaona kweli hujui.

Hatua ya kuchukua leo, kama hujawahi kusoma kitabu tokea umalize chuo au shule basi ujue unainyima akili yako haki yake, akili yako iko kama raba bendi jinsi unavyoiongezea maarifa nayo inavutika na kutanuka kama vile raba bendi. Hakikisha unafanya na shopping za akili yako kama vile unavyofanya katika mwili wako.

Hivyo basi, mafanikio yako yanatakiwa yawe na mlinganyo katika eneo la akili, kimwili na kiroho siyo kujali upande mmoja tu. Ukijali upande mmoja lazima utanyumba sehemu tu hivyo kuwa makini juu ya hili.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi ambayo ni www.mtaalamu.net/kessydeo