Rafiki yangu mpendwa,
Kuanzisha biashara ni ndoto ya wengi, lakini kati ya wanaopanga kuanzisha biashara, na wale kweli wanaoanzisha biashara, ni wachache sana wanaoanza biashara kweli.
Na katika wale wanaoanza biashara, mambo siyo mazuri sana, kwanza zipo takwimu za kusikitisha, kwamba katika biashara 10 zinazoanzishwa, ndani ya mwaka mmoja, nane zinakuwa zimekufa.
Katika biashara ambazo watu wanaziendesha, nyingi hazijiendeshi kwa faida yaani biashara haitengenezi kipato cha ziada. Bali biashara inaenda kwa kiwango cha kawaida, cha mtu kupata fedha ya kuendesha maisha yake.
Sasa hili ni baya kwa sababu biashara haikui, badala yake inadumaa na kwa sababu gharama za maisha zinaongezeka kadiri muda unavyoenda, biashara inaanza kujiendesha kwa hasara na hatimaye inakufa.
Rafiki, hata zile biashara ambazo zinajiendesha kwa faida, faida inayopatikana imekuwa ni kidogo sana. Utakuta faida ambayo watu wanafurahia kupata na wanaona ni kubwa sana ni asilimia 10 kwa mwaka, na wakijitahidi sana basi inakuwa silimia 20 kwa mwaka.
Asilimia 10 mpaka 20 ya faida ni kidogo sana kwa mwaka hasa kama unataka kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Na kwa kuwa zama ambazo tunaishi sasa ni za changamoto, ambapo biashara ni nyingi na ushindani ni mkubwa, je hutafurahi ukiweza kujifunza njia ya kukuza biashara yako na kuongeza faida kwa zaidi ya asilimia 50 kwa mwaka?
Najua kila mfanyabiashara mwenye malengo makubwa atapenda kujifunza hilo, na ndiyo maana mimi rafiki yako nimekuandalia semina ya kujifunza hili wa kina.
Rafiki, kila mwaka huwa naendesha semina tatu tu, semina mbili kwa njia ya mtandao na semina moja ya kukutana ana kwa ana. Semina ya kwanza huwa ni mwanzoni mwa mwaka, ya kuuanza mwaka kwa mafanikio makubwa, ya pili katikati ya mwaka na ya tatu karibu na mwisho wa mwaka ambapo tunakutana pamoja kwa kuyapanga maisha ya mafanikio zaidi.
Sasa umefika wakati wa kupata semina yetu ya pili kwa mwaka huu 2018, ambayo itahusu njia za kukuza biashara zetu.
Semina itakuwa; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza faida kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.
Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;
UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.
NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.
NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.
NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.
NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.
NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.
HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.
Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.
Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.
Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.
Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.
Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.
Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.
Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.
Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.
Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018
Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.
Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa; www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha
Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha
Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog