Mpendwa rafiki,

Hakuna biashara bila kuwa na mteja na kama tunafanya biashara na hakuna mtu wa kumuuzia ni rahisi sana kufunga zile biashara ambazo tunafaya kila siku. Kiasili kila mtu ni mfanyabiashara na kila mtu kuna kitu anauza na hivyo basi kama kila mtu kuna kitu anauza basi lazima anamwitaji mteja ili aweze kumuuzia.

Kila biashara ina wateja wake na mteja mara nyingi huwa anafanya maamuzi ya kuamua kununua kule anakotaka kwenda. Yeye ni mfalme katika biashara yoyote ile wala huwezi kumlazimisha bali anahitaji kitu cha ushawishi ili aweze kuja kwako na asiende kwa mwingine kama huna kitu cha ziada kwako mteja anaamua kwenda kule ambako atapata kile anachokitaka.

KWA NINI SIYO TAJIRI

Njia pekee ya kumtuliza mteja katika biashara unayofanya ni kumpatia mteja huduma bora ambayo hatoweza kuipata sehemu yoyote ile ila kwako tu. Kama mteja unampa kile anachotaka basi ataendelea kuwa mteja wako, utamtuliza na atabaki. Kwa mfano wewe rafiki, kuna mahitaji ambayo unapenda sana kununua sehemu fulani yaani hata iweje utajikuta unaenda palepale licha hata ya sehemu nyingine kuwepo. Unaweza kujiuliza ni kwanini unaenda kila siku pale na siyo sehemu nyingine? Huenda kwa sababu unapenda kwenda pale kwa sababu unapewa kile unachokitaka na huduma hiyo huipati sehemu nyingine.

SOMA; Changamoto Kuu Tano Za Biashara Kwenye Zama Tunazoishi Sasa Na Kitu Kimoja Muhimu Kufanya Ili Kuvuka Changamoto Hizo.

Muda mwingine mazoea ya huwa yanaua biashara kwani wale wafanyabiashara wakishamzoea mteja wanamuona ni mtu tu wa kawaida hivyo wanamchukulia poa wala haweki tena juhudi ya kuendelea kumtuliza hivyo mteja akishaona mazoea yamezidi na hapati huduma bora kama ile ya mwanzo anakimbia. Natumaini unamjua ndege je ulishawahi kumuona ndege anakaa katika mti mmoja siku nzima? Kwanza anaruka katika mti aupendayo na akikaa kidogo akiona hakuna kinachompendeza anaishia zake na kwenda mti mwingine.

Kazi kubwa ambayo unayo kama mfanyabiashara ni kuhakikisha unamtuliza mteja wako kwa kumpa kile anachokitaka, kumpa huduma bora ambayo hatoweza kuipata sehemu nyingine yoyote ila kwako tu.

SOMA; Kosa Moja Kubwa Ambalo Wafanyabiashara Wengi Wanafanya Kwa Wateja Wa Biashara Zao.

Hatua ya kuchukua leo, kama unataka kumtuliza mteja katika biashara yako basi mpatie huduma bora ambayo hatoweza kuipata sehemu nyingine yoyote ila kwako tu.

Kwahiyo, unapokuwa katika kufanya kitu chochote kile usifanye kwa mazoea fanya kama vile ndiyo mara yako ya kwanza na muone kila mteja ni mpya kwako lakini ukishamuona mteja ni mtu wa kawaida tu kwako atakukimbia mara moja. Kila siku muone mpya kwa kumpa kitu kipya ili uendelee kumtuliza katika biashara yako na awe wako siku zote.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !