Mpendwa rafiki,

Hebu jaribu kuvuta picha tu watu wote ambao unawajua wako katika historia ya dunia wamefanya mambo gani? natumaini jibu umepata mwenyewe hakuna mtu ambaye yuko katika historia  na kuandikwa sana katika vitabu kwa kufanya mambo madogo. Watu wote waliofanya mambo makubwa duniani ndiyo tunawaona katika historia mbalimbali na ndiyo hata mashuleni kuna somo la historia linalotukumbusha yale waliyofanya wenzetu waliotutangulia na ukiyaangalia siyo mambo ya mchezo hata kidogo.

Rafiki, unafanya nini ili kuingia katika kitabu cha historia? Na ukiangalia watu wote ambao wako kwenye historia hatuwakumbuki katika ubinafsi wao bali tunawakumbuka kwa sababu walifanya kwa ajili ya watu wengine na siyo kwa ajili ya familia zao tu. Mtu yeyote anayejifikiria yeye bila wengine ni ngumu sana kuingia katika historia yoyote ile. Je historia huwa inawapendelea watu gani?

seneca_quote

Historia huwa inawapendelea watu wote wanaocheza kushinda, ambao wanajitoa kushinda, wanaochukua hatari,wanaojihatarisha kushinda. (History favors risk- takers), sasa kama wewe unaogopa hatari historia haiwezi kukupendelea kamwe. Historia inawapendelea wale wanaochukua hatari, wanaojitoa kafara kwa ajili ya ushindi, ambao wanatafuta matokeo na siyo sababu.

SOMA; Tabia Tano Muhimu Unazopaswa Kujua Kuhusu Watu Kwenye Safari Yako Ya Mafanikio.

Huwezi kumkuta mtu ambaye yuko katika historia ya dunia na alikuwa na sababu katika maisha yake. Mara leo sijisikii au najisikia kufanya, ni watu ambao huwa hawapotezi siku hata siku moja. Watu ambao hawajali sababu yoyote iwaangushe bali wanachojali ni matokeo tu.

Unahitaji kubadilika sana ili uweze kupendelewa na historia na wala historia huwa haihitaji sababu wala rushwa wewe pata tu hata mfano ulivyokuwa unasoma kwani wali ambao wamefanya makubwa shuleni enzi unasoma walikuwa ni watu wa mchezo mchezo? Au walikuwa wanafanya mambo madogo mpaka wakaandikwa katika katika historia?

Hatua ya kuchukua leo, kama unataka kuingia katika historia basi amua kuwa mtu wa kuchua hatari. Jiwashe moto, jichochee bila kujihurumia na ikiwezekana jitoe kafara utaingia katika historia na uhakika ukifanya makubwa historia itakufuata uliko?

Kwahiyo, unafanya nini? Umeiweka wapi talanta yako? unatamani mafanikio? Ingia kutafuta kile unachokitaka kwa matendo ndiyo utaweka historia na wala usipoteze muda kwa maneno.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !