Mpendwa rafiki,

Sehemu yoyote ile huwa ina kanuni na taratibu zake na ili mambo yaende vizuri watu hawana budi kutii mamlaka ya sehemu husika. Sehemu ambayo haina utaratibu inakuwa haina maana kwani watu watafanya vile wanavyotaka, hivyo basi, kanuni na taratibu ziko kwa ajili ya kuwaongoza watu sehemu husika.

Shule , vyuo,tulivyosoma , nyumba za ibada na sehemu nyingine zote huwa zina taratibu ambazo kama mtu unaalikwa kufuata taratibu mahalia. Na unapokwenda kinyume utaonekana kama  ni mtu wa ajabu sana.

raising positive kids

Watoto wadogo wanahitaji malezi mazuri kutoka kwa wazazi na malezi mazuri siyo tu mtoto kula,kuvaa na kumsomesha inakuwa ni zaidi ya hapo. Watoto wadogo siku licha ya kupata yote kutoka kwa wazazi wao ila kuna kitu wanakikosa ndiyo maana unakuta wengine wanapotea kirahisi.  Watoto wadogo wakikosa mwongozo au msingi kutoka kwa wazazi lazima watapotea njia, watashindwa kujua nini cha kufanya na watabaki njia panda.

Wazazi wanajisahau sana katika suala la malezi kwa watoto, watoto wanakosa kupewa misingi na miongozo mbalimbali ya kufuata ndiyo maana mtoto anakuwa hajui nini anatakiwa kufanya. Kama nyumba inavyojengwa lazima ianze na msingi vivyo hivyo hata watoto ili wawe watu bora wanatakiwa kupata misingi imara kutoka kwa wazazi wao. Ukikosa mwelekeo basi, mwelekeo wowote utakuchukua vivyo hivyo hata watoto wakikosa mwongozo, wakikosa msingi basi watachukuliwa na mwelekeo wowote ule.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; A Gift To My Children (Zawadi Ya Baba Kwa Watoto Wake, Masomo Ya Maisha Na Uwekezaji).

Ni muhimu kama  mzazi uwe na misingi katika maisha yako na mtoto wako pia unatakiwa kumfundisha misingi unayotaka wewe aiishi vinginevyo atakuwa hana msingi wowote wa kusimamia. Mzazi unatakiwa kuwa na kitu unachosimamia halafu umfundishe na mtoto wako misingi ambayo anatakiwa kufuata. Usipomfundisha mtoto misingi ya maisha yako dunia itakuja kumfundisha kwa adhabu kali baadaye hivyo ni bora mzazi kumsaidia mtoto kumpatia mwongozo bora wa maisha yake.

Changamoto nyingine ni wazazi wenyewe kukosa misingi imara katika maisha yao, kwanza wengine hawana hata kitu wanachosimamia hivyo hata watoto wanakuwa wanajiendea tu kienyeji. Kama mzazi unataka mtoto wako awe wa namna fulani anza kwanza wewe kuishi vile mtoto wako anavyotakiwa kuwa.

Hatua ya iuchukua leo, mfundishie mtoto misingi ya maisha yako, usipomfundisha uelekeo wowote utamchukua kama vile upepo. Mfundishe kweli ya dunia na kweli itamuweka huru siku zote za maisha yake.

SOMA; Usipomwadhibu Mtoto Wako Dunia Itakusaidia Kumwabibu Kikatili

Hivyo bas, inahitaji kazi kubwa katika malezi ya watoto kama vile tunavyoweka juhudi kubwa katika kazi zetu. Ukiweka juhudi katika kutafuta tu mafanikio na ukasahu familia yako utakuja kujikuta unapotea na hata kile unachokitafuta utakiona hakina maana kubwa. Kuna maana gani una mafanikio mazuri halafu familia au watoto wako wamepotea kwa kukosa malezi mazuri?

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !