“Frame your thoughts like this—you are an old person, you won’t let yourself be enslaved by this any longer, no longer pulled like a puppet by every impulse, and you’ll stop complaining about your present fortune or dreading the future.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 2.2
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo,
Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MTAZAMO SAHIHI WA AKILI YAKO…
Tumekuwa tunaruhusu akili na mawazo yetu kutufanya sisi kuwa watumwa wa mambo ya nje.
Kila wakati tunaruka ruka na yale yanayoendelea, tusiweze kutulia hata na jambo moja ambalo ni muhimu kwa muda.
Unapaswa kubadili hali hiyo na kuanza kuotawala akili yako badala ya akili kukutawaka wewe.
Mtazamo sahihi wa akili yako ni kujifikiria wewe kama mtu mzima ambaye hutakubali kuyumbishwa na kila aina ya fikra zinazokuingia.
Utaacha kulalamika kuhusu hali uliyonayo sasa na kuacha kutamani sana yale yajayo.
Ukishaweza kuidhibiti akili na fikra zako, utakuwa na uhuru mkubwa kwenye maisha yako na kuweza kufuatilia yale ambayo ni muhimu zaidi kwako, badala ya kupelekeshwa tu na mambo ambayo hata siyo muhimu.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kushika udhibiti wa akili na fikra zako na kuacha kuyumbishwa kama mtoto.
#DhibitiFikraZako, #AchanaNaKulalamika, #IshiLeo
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha