(MUHIMU; Soma makala hii mpaka mwisho, kuna zawadi ya vitabu.)

Rafiki yangu mpendwa,

Kwa wale wasiojua, au wasioelewa, buku ni lugha ya mtaani iliyozoeleka kutwa shilingi elfu moja. Watu wamezoea kuambiana nipe buku au una buku hapo na kadhalika.

Upo mchezo wa bahati nasibu ambao unawaahidi watu wanaweza kubadili maisha yao kwa ‘nguvu ya buku’, lakini siyo kweli, hutaweza kuyabadili maisha yako kwa kutumia bahati nasibu au kamari.

Tafiti zote ambazo zimewahi kufanywa kwa washindi wa michezo ya bahati nasibu, miezi sita baada ya kushinda maisha yao yanakuwa hayana tofauti na yalivyokuwa kabla ya kushinda. Hata hali yao ya furaha huwa inashuka kuliko walivyokuwa kabla ya kushinda bahati nasibu.

Hivyo kitu pekee tunachoweza kusema bahati nasibu au kamari inaleta kwenye maisha yako, ni kuyavuruga.

Sasa mimi rafiki yako, ambaye nimetoa sehemu kubwa ya maisha yangu kutafuta maarifa sahihi ya kutuwezesha kuwa na maisha bora, nimekuwa nafikiria ni kwa namna gani tunaweza kuitumia vizuri nguvu ya buku katika kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

Na baada ya tafakari ya muda mrefu, nimepata jibu la jinsi unavyoweza kuitumia nguvu ya buku kuyaboresha sana maisha yako.

Kwa shilingi elfu moja pekee, unaweza kufikia ubobezi wa hali ya juu sana kwenye jambo lolote unalotaka kubobea, unaweza kuwa na furaha ya kudumu kwenye maisha yako na kwa ujumla maisha yako yatakuwa bora sana.

Je inawezekanaje buku tu likupe manufaa makubwa kiasi hicho? Endelea na mimi hapa na utaona.

buku

Lakini kabla hatujaangalia nguvu ya buku katika kuyafanya maisha kuwa bora, hebu kwanza tukumbushane ni vitu gani unaweza kufanya na shilingi elfu moja kwenye zama hizi tunazoishi sasa (mwaka 2019);

Kwa buku unaweza kupata soda moja au mbili, ukazinywa na zikaisha, na usipate manufaa yoyote zaidi ya kuujaza mwili wako sukari.

Kwa buku unaweza kupata maji ya kunywa, ambayo hayana tofauti kubwa na maji unayochota bombani na kuyachemsha.

Kwa buku unaweza kupata kilo moja ya unga, au nusu kilo ya mchele, ukaenda kula na kesho ukahitaji tena kula.

Kwa buku unaweza kununua data za mtandao wa intaneti ambazo utatumia kuzurura instagram, facebook na wasap na kupoteza muda wako.

Kwa kifupi buku au shilingi elfu moja ina matumizi machache sana kwenye maisha yetu, ni fedha ambayo kila mtu anaweza kudharau.

Lakini mimi nakuahidi kwamba hilo hilo buku unalolidharau, linaweza kuyafanya maisha yako kuwa bora mno, ukatoka hapo ulipo sasa na kupiga hatua kubwa sana.

NJIA PEKEE YA KUKUTOA HAPO ULIPO SASA.

Njia pekee inayoweza kukutoa hapo ulipo sasa na kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako ni kujifunza kupitia usomaji wa vitabu. Kitu chochote unachotaka kujua, tayari kipo kwenye vitabu. Popote ambapo umekwama sasa, kuna wengine walishakwama na wakavuka, halafu wakaandika vitabu waliwezaje kuvuka na kufanikiwa.

Hivyo unachohitaji wewe ni kupata vitabu sahihi na kutenga muda wa kuvisoma, kutafakari na kuondoka na hatua za kuchukua. Kitu ambacho ni kigumu sana kwenye zama tunazoishi, zama za usumbufu na kelele za kila aina.

Ukiweza kupata vitabu sahihi, na kukaa chini kwa utulivu kusoma, hutabaki hapo ulipo sasa.

Lakini changamoto ni kuvipata vitabu sahihi na muda wa kuvisoma, na hapo ndipo mimi Rafiki yako wa karibu, na Kocha wa maisha yako ninapokuja kukusaidia kwenye hilo.

KARIBU KWENYE CHANNEL YA TANO ZA JUMA.

Rafiki, nimekuandalia channel maalumu kwa ajili ya vitabu na uchambuzi wa vitabu. Kwa kuwa kwenye channel hii, kila wiki utapata kitabu cha kusoma, uchambuzi wake na mafunzo ya ziada kutoka kwenye kitabu hicho.

Hivyo ugumu wa wewe kupata vitabu hautakuwepo tena, maana kila wiki utapata kitabu cha kusoma.

Na pia tatizo la kukosa muda wa kusoma halitakusumbua tena, kwa sababu kila wiki nakupa uchambuzi wa kina wa kitabu nilichosoma, na hatua za kuchukua kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Yaani ni kama nimeshatafuna kila kitu, wewe ni kusoma na kuchukua hatua tu.

Yaani kwa kifupi, kwa kuwa kwenye channel hii, utakuwa na uhakika wa kupata maarifa sahihi na kuweza kuchukua hatua ili kuyaboresha maisha yako.

Na kitu kizuri kuliko yote ni kwamba gharama za kuwa kwenye channel hii ni ndogo mno, ni buku tu, lile buku ambalo unalidharau, sasa linakuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

MFANO WA KITABU, UCHAMBUZI NA #MAKINIKIA.

Rafiki, napenda nikupe mfano wa kitabu ambacho tumejifunza na kukichambua, kitabu kinaitwa PEAK; secrets from the new science of expertise ambacho kimeandikwa na  Anders Ericsson.

Kitabu hiki kinatupa sayansi na siri za kubobea kwenye kitu chochote ambacho tunataka kubobea. Ndani ya kitabu hiki (na chambuzi nilizofanya) utajifunza aina sahihi ya ufanyaji wa kile unachofanya ili kufikia ubobezi.

Ili ujifunze na uone nini utakipata kwa kujiunga na channel ya tano za juma. Hapa nimekupa bure kabisa mafunzo haya;

Makala ya tano za juma ambayo imechambua kwa kina kitabu hiki, fungua hapa kupakua; http://bit.ly/tanozajumapeak

Makala ya mafunzo ya ziada (#MAKINIKIA) kutoka kwenye kitabu kilichochambuliwa unaweza kuipakua hapa; http://bit.ly/makinikiapeak

Na kitabu ambacho tumekichambua na kujifunza unaweza kukipata pia na ukajisomea kadiri uwezavyo, unakipata bure hapa; http://bit.ly/kitabupeak

Rafiki, pakua mafunzo hayo na usome na ukiona yanakufaa na ungependa kuyapata kila wiki kwa mwaka mzima, basi karibu kwenye channel ya TANO ZA JUMA, ambapo buku litakuwa na nguvu ya kweli ya kubadili maisha yako.

Karibu sana kwenye channel hii mpya ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA.

Channel hii ipo kwenye mtandao wa TELEGRAM, ambao ni mzuri sana kwenye kuhifadhi kumbukumbu za nyuma. TELEGRAM inafanana sana utendaji kazi wake kama ilivyo wasap.

Kwa kutumia channel ya telegram, mtu mpya anapojiunga anaweza kuona mafunzo ya nyuma tofauti na ulivyo mtandao wa wasap.

JINSI YA KUSHIRIKI KWENYE CHANNEL HII.

Kujiunga na channel ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA ni bure kabisa kwa wiki moja, ambapo utapata mafunzo hayo muhimu.

Baada ya wiki ya kwanza kuisha, kama utapenda kuendelea kuwa kwenye channel ya TANO ZA MAJUMA YA MWAKA utapaswa kulipia shilingi elfu moja (1,000/=) kila juma.

Hii ni ada ndogo ambayo itakuwezesha kuendelea kupata uchambuzi wa vitabu kila juma, kupata kitabu kilichochambuliwa kila juma na pia kupata mafunzo ya ziada (MAKINIKIA) yanayopatikana kwenye kitabu cha juma kilichochambuliwa.

Ada ya kuwa kwenye channel hii unaweza kuchagua kulipa kila wiki, au ukalipa kwa mwezi, miezi mitatu, sita au mwaka mzima. Na kadiri unavyochagua kulipa ada ya muda mrefu ndivyo ada inavyozidi kupungua na kuwa nafuu zaidi kwako.

Kama unalipa kwa wiki basi siku ya kulipa ni siku ya kwanza ya wiki ambayo ni jumatatu. Kila jumatatu utalipia tsh elfu moja (1,000/=) ili kuendelea kupata mafunzo kwenye channel hii.

Kama utalipa kwa mwezi basi utalipa siku ya kwanza ya mwezi ambayo ni tarehe moja ya mwezi husika. Kila tarehe moja ya mwezi utalipia tsh elfu tatu (3,000/=) ambayo itakupa nafasi ya kujifunza kwa mwezi mzima. Ukilipa kwa mwezi unaokoa shilingi elfu moja mpaka elfu mbili.

Na kama utachagua kulipa kwa mwaka mzima ili usisumbuke kutuma kidogo kidogo kila wiki au kila mwezi, itakuwa bora zaidi kwako. Kila mwanzo wa mwaka utalipa tsh elfu thelathini (30,000/=) ambayo itakupa nafasi ya kujifunza kwa mwaka mzima. Ukilipa ada ya mwaka unaokoa tsh 22,000/= ukilinganisha na kulipa kila wiki.

NAMBA ZA KUFANYA MALIPO.

Kujiunga na channel hii ni bure kwa wiki ya kwanza, hivyo tuma ujumbe kwa njia ya telegram kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na kwamba unapenda kujiunga na TANO ZA JUMA.

Baada ya wiki ya kwanza kuisha, utachagua kama utapenda kubaki na kuendelea kupata mafunzo haya ya uchambuzi wa vitabu na tano za juma. Kama utachagua kubaki na kupata mafunzo, utachagua unalipia kwa kipindi gani na hapo unafanya malipo na kuendelea kuwa ndani ya channel.

Malipo ya kujiunga na kupata mafunzo ya channel ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA, yafanyike kwa namba zifuatazo;

MPESA; 0755 953 887.

TIGO PESA/AIRTEL MONEY; 0717 396 253.

Ukishatuma malipo, tuma ujumbe kwa telegram kwenda namba 0717396253 ukiwa na majina yako na kwamba umelipia TANO ZA JUMA.

Karibu sana kwenye channel hii ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA, hii ni channel yako ya kupata uchambuzi wa kina wa vitabu, kuondoka na hatua za kuchukua ili maisha yako yawe bora zaidi.

Kujiunga na channel ya TANO ZA MAJUKA 52 YA MWAKA, tuma ujumbe kwa kutumia TELEGRAM kwenda namba 0717396253 na utaunganishwa bure kwa wiki moja na baada ya hapo utachagua kama utalipia kwa wiki, mwezi au mwaka.

JINSI YA KUPATA TELEGRAM KWA WASIOKUWA NAYO.

Kwa wale ambao hawatumii telegram au hawajui jinsi ya kuipata, ingia kwenye playstore au appstore ya simu yako na tafuta TELEGRAM MESSENGER kisha ipakue na kuinstall kwenye simu yako. Utaandikisha namba yako ya simu na ukishaiweka nitumie ujumbe kuja namba 0717396253 wa TANO ZA JUMA na nitakuunga kwenye channel.

Pia kama nuna simu yenye uwezo wa kuweka app. Unaweza kutumia telegam kwenye kompyuta moja kwa moja. Ukiingia kwenye tovuti yao; https://desktop.telegram.org utaweza kupakua telegram ya kutumia kwenye kompyuta. ukifungua link hiyo bonyeza sehemu ya GET TELEGRAM FOR WINDOWS au mfumo mwingine unaotumia, na utaweza kuipakua na kuweka kwenye kompyuta yako. Ukishaiweka kwenye kompyuta yako unaandikisha namba ya simu na utakuwa tayari kutumia.

Karibu sana tujifunze kwa pamoja kupitia usomaji na uchambuzi wa vitabu.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge