“The raw material for the work of a good and excellent person is their own guiding reason, the body is that of the doctor and the physical trainer, and the farm the farmer’s.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.3.1

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari WEWE NI MRADI…
Wewe ni mradi unaoendelea na rasilimali kuu unayopaswa kuifanyia kazi kila siku kwenye mradi huu ni akili yako.
Hii ndiyo rasilimali unayopaswa kuiboresha kila siku.
Kama ambavyo mkulima analima shamba lake, na mchezaji anauweka mwili wake kwenye mazoezi, ndivyo unavyopaswa kuifanyia kazi akili yako.

Akili yako ndiyo inayokuletea kila kitu kwenye maisha yako,
Akili hiyo ina nguvu kubwa ya uumbaji, kile unachofikiria ndiyo kinachotokea.
Akili hiyo inakuonesha kile unachotaka kuona na kukuepusha na usichotaka kuona.
Akili hiyo ndiyo inayoweza kukupa hamasa kubwa ya kuchukua hatua zaidi au kukukosesha hamasa na ukashindwa kuchukua hatua.

Ukiweza kuifanyia kazi akili yako, na ukaweza kuidhibiti kwa kiwango kikubwa, wewe kama mradi utapiga hatua zaidi. Kwa kuwa hakuna linaloshindikana kwa akili iliyo bora, inayofanyiwa kazi na kudhibitiwa.

Ifanyie kazi akili yako kila siku kwa kuwa na mawazo ya kile unachotaka kwenye maisha yako, kufikiri chanye na kwenye uwezekano.
Idhibiti akili yako kwa kuondokana na hisia zote hasi na za kukata tamaa.
Akili ikiwa sawa, na maisha yako yanakuwa sawa.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanyia kazi na kudhibiti akili yako ili uwe mradi bora kabisa.
#AkiliRasilimaliKuu, #WeweNiMradi, #DhibitiAkiliYako

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha