Shukrani Na Hongera Kwa Wale Walioshiriki Uzinduzi Wa Vitabu Vya Elimu Ya Msingi Ya Fedha Na Tano Za Majuma 50 Ya Mwaka.

Rafiki yangu mpendwa,

Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza wote ambao waliweza kushiriki uzinduzi wa vitabu vya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA uliofanyika tarehe 03/08/2019.

Tumeweza kufanya uzinduzi huo kwa mafanikio makubwa kwa sababu ya wale wote waliopata nafasi ya kushiriki. Hivyo nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wote waliotenga muda wao na kushiriki uzinduzi huo. Ni imani yangu kila aliyeshiriki ameondoka na mambo aliyojifunza hivyo kinachobaki ni kwenda kuyafanyia kazi ili kuweza kupata matokeo bora kabisa.

Pia nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa ushiriki kwenye uzinduzi, ni kitu kinachoonesha jinsi gani mtu umejitoa kupata maarifa sahihi ili kuweza kupiga hatua kwenye maisha. Kuacha shughuli zako na wengine kusafiri kutoka mbali kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa vitabu inaonesha jinsi gani mtu unayathamini maarifa. Na kwa kuwa maarifa yana nguvu kubwa, ni wajibu wa kila mmoja wetu kuchukua hatua kwa maarifa anayopata ili aweze kupiga hatua zaidi kwenye maisha yake.

Kwenye uzinduzi wa vitabu tumepata shuhuda mbalimbali za jinsi maarifa yalivyoboresha maisha ya watu, tumejifunza nguvu ya maarifa katika maendeleo binafsi na pia kujifunza njia bora za kusoma vitabu viwili vilivyozinduliwa, ambavyo ni ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA.

Tutaendelea kushirikishana kuhusu usomaji wa vitabu na kuchukua hatua kwenye makala zinazokuja.

Hapa nimeambatanisha zawadi ya vitabu vitatu nilivyoshauri kila mtu avisome, vitabu ambavyo ndiyo vilifungua ulimwengu wangu mpya katika moja ya vipindi vigumu kabisa kwenye maisha yangu.

Lakini pia nimeambatanisha picha mbalimbali za washiriki wa uzinduzi pamoja na zoezi la kuweka sahihi kwenye vitabu ambalo lilifanyika.

ZAWADI YA VITABU.

Rafiki, kwenye uzinduzi wa vitabu niliahidi kushirikisha vitabu vitatu ambavyo vimebadili sana maisha yangu, na ambavyo nashauri kila mtu avisome.

Vitabu hivyo ni RICH DAD, POOR DAD kilichoandikwa na Robert Kiyosaki, hiki ni kitabu kilichonifungua akili kwamba mafanikio kwenye maisha hayatokani na elimu pekee. Unaweza kufanikiwa sana hata kama huna elimu kubwa.

Unaweza kupakua kitabu hiki hapa; Rich Dad, Poor Dad – Robert T. Kiyosaki

Kitabu cha pili ni THINK AND GROW RICH, ambacho kiliandikwa na Napoleon Hill, kitabu hiki kilinifungua akili kwamba mafanikio yanaanzia kwenye fikra na mitazamo ambayo tunayo. Unaanza kufanikiwa kwanza ndani yako kabla hujafanikiwa nje.

Unaweza kupakua kitabu hiki hapa; Think And Grow Rich

Kitabu cha tatu ni THE RICHEST MAN IN BABYLON, kilichoandikwa na George S. Classon, kitabu hiki kilinipa siri na msingi mkuu wa kutoka kwenye umasikini na kwenda kwenye utajiri. Msingi huo ni kwa kila kipato unachoingiza, JILIPE WEWE MWENYEWE KWANZA kabla hujawalipa watu wengine.

Unaweza kupakua kitabu hiki hapa; The Richest Man In Babylon

Pata vitabu hivyo kwa kupakua hapa na kuvisoma, na kwa hakika maisha yako hayatabaki pale yalipo sasa.

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KWENYE UZINDUZI WA VITABU.

Rafiki, hapa chini kuna picha za matukio mbalimbali wenye uzinduzi wa vitabu. Unaweza kupakua picha yako kwa ajili ya kumbukumbu.

Nimalize kwa kusema asante sana ka ushiriki wako kwenye uzinduzi wa vitabu, asante kwa kuendelea kuwa pamoja na mimi kwenye safari hii ya kujifunza na kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi. Karibu sana tuendelee kuwa pamoja, tuendelee kupata maarifa sahihi na kuchukua ili maisha yetu yaweze kuwa bora zaidi.

Kama bado hujapata vitabu ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA, piga simu au tuma ujumbe sasa kwenda namba 0678 977 007 au 0752 977 170 na utapewa maelekezo ya kuvipata. Karibu sana.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge