“Do now what nature demands of you. Get right to it if that’s in your power. Don’t look around to see if people will know about it. Don’t await the perfection of Plato’s Republic, but be satisfied with even the smallest step forward and regard the outcome as a small thing.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 9.29.(4)

Ni siku nyingine nzuri, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi nyingine bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari FANYA KILICHO MBELE YAKO SASA…
Kila wakati huwa tuna kitu cha kufanya ambacho kipo mbele yetu,
Mara nyingi huwa tunakwepa kufanya kitu hicho kwa sababu mbalimbali.
Labda tunajiambia hatujawa tayari kufanya kitu hicho,
Au tunasubiri tukiamini mambo yatakuwa bora zaidi baadaye.
Lakini huko kote ni kujichelewesha.
Hakuna wakati utakuwa tayari zaidi ya ulivyo sasa,
Na mambo hayatakuwa bora zaidi ya yalivyo sasa.
Hivyo unapaswa kufanya kile kilicho mbele yako sasa,
Kama ambavyo dunia na asili vinakutaka ufanye,
Hapo ulipo sasa ndipo pa kuanzia ili uweze kufika kule unakotaka kufika.

Kuanza ni bora kuliko kutokuanza kabisa,
Kupiga hatua ndogo ni bora kuliko kutokupiga hatua yoyote kabisa,
Kufanya chochote ni bora kuliko kutokufanya chochote kabisa.
Anza kufanya leo kile kilicho mbele yako, kisha kazana kukifanya kwa ubora zaidi.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kile kilicho mbele yako, bila kusubiri ukamilifu au mambo yawe mazuri zaidi.
#AnziaHapoUlipoSasa #FanyaKilichoMbeleYako #UsisubiriUkamilifu

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1