Andrew Carnegie ambaye alikuwa mtu tajiri kuliko wote duniani enzi za uhai wake, aliwahi kuandika kitabu alichokiita GOSPEL OF WEALTH, kwa tafsiri rahisi ni INJILI YA UTAJIRI.

Katika injili yake hiyo, alieleza ni jinsi gani utajiri ni mzuri na njia pekee ya mtu kuisaidia jamii ni kuwa tajiri. Lakini pia alionesha ni jinsi gani ilivyo rahisi kufikia utajiri kama umeanzia kwenye umasikini kuliko kutokea kwenye utajiri.

carnegie on gospel of wealth.jpg

Kikubwa zaidi ambacho Carnegie ametueleza kupitia kitabu chake hicho ni njia ya uhakika ya kuelekea kwenye utajiri ni kufanya biashara. Anasema ajira ni sehemu ya kuanzia, sehemu ya kujifunza na sehemu ya kutengeneza mtandao. Lakini utajiri mkubwa haupatikani kwenye ajira, bali kwenye biashara.

Andrew aliamini kama mtu angeweza kuanzisha na kuendesha vizuri biashara yake, angeweza kufanikiwa sana. Na yeye mwenyewe hiyo ndiyo njia aliyopita, alianza kama kibarua kwenye kampuni ya reli, na baadaye kuweza kuanzisha kampuni yake ya kufua vyuma ambayo ilimfikisha kwenye mafanikio makubwa.

Nimekuwa nikieleza sana kuhusu umuhimu wa kila mtu kuwa na biashara, hasa kwa zama ambazo tunaishi sasa. Kwa sababu ya changamoto nyingi kwa upande wa ajira, nimekuwa nashauri kila mtu ambaye ameajiriwa basi awe na biashara ya pembeni ambayo inamuingizia kipato cha ziada

Lakini watu wamekuwa na visingizio vingi kwa nini hawawezi kuingia kwenye biashara. Na kisingizio kikubwa kabisa kimekuwa mtaji. Watu wengi wamekuwa wanasema wanataka kuingia kwenye biashara lakini hawana mtaji. Lakini hiyo ni sababu ambayo wamekuwa wanaitumia miaka nenda miaka rudi.

Mimi binafsi nimekuwa naikataa sababu hii, mtu yeyote anaposema anataka kuingia kwenye biashara lakini hana mtaji, najua tatizo siyo mtaji, bali tatizo ni yeye mwenyewe, yeye binafsi hajawa tayari kuingia kwenye biashara na kupambana mpaka kufanikiwa.

Elia Hassani ni mmoja wa watu ambao wameweza kuanzisha biashara akiwa kwenye ajira, lakini yeye alianza na biashara ndogo sana na alianzia chini kabisa. Mtaji ambao aliwekeza kwenye biashara yake ni mdogo mno, kiasi cha shilingi elfu 5 na akatumia vifaa vingine ambavyo tayari alikuwa navyo. Lakini baada ya muda mfupi, biashara hiyo aliyoanzia chini kabisa, iliweza kumpa faida ya mpaka elfu 10 kwa siku. Kadiri alivyoendelea kuweka juhudi kubwa kwenye biashara hiyo, faida yake iliongezeka mpaka kufika elfu 30 kwa siku.

ELIA HASSANI
Elia Hassani akitoa ushuhuda wake wa kuanzia biashara chini kabisa kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.

Kwenye kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili, Elia ametushirikisha mchanganuo wa biashara aliyoianza kwa mtaji mdogo kabisa, jinsi ambavyo aliianza, vifaa vinavyohitajika na jinsi anavyotengeneza faida. Ameeleza kwa namna rahisi ambayo hata wewe unaweza kujifunza na kunufaika sana, na kisha ukachukua hatua na kuondoka kwenye changamoto za kipato ulizonazo sasa.

Rafiki, wito wangu kwako ni huu, kama mpaka sasa hujawa na biashara na una kisingizio chochote kile, basi soma kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili, kina majibu ya changamoto zote, kuanzia wazo ka biashara, mtaji, muda, usimamizi na mengine mengi.

Pia kama umeshaanza biashara lakini unapitia changamoto mbalimbali na unaona huwezi kufanikiwa, soma kitabu hicho na kitakupa maarifa mazuri ya kuvuka changamoto za kibiashara unazopitia.

Kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA Toleo la pili kinapatikana kwa nakala ngumu (hardcopy) na kwa bei ya tsh elfu 20 (20,000/=). Kitabu unaweza kukipata popote ulipo Tanzania. Kupata kitabu nakala yako ya kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, piga simu au tuma ujumbe kwenye namba zifuatazo; 0678 977 007 au 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu na kama upo mkoani utatumiwa au kuunganishwa na mawakala waliopo mikoa mbalimbali.

makirita cover 3-01

Usikubali kuendelea kubaki kwenye umasikini, mkombozi wa uhakika ni biashara, anza sasa biashara yako kwa hapo ulipo na pata mwongozo sahihi kupitia kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA toleo la pili.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha