Ni biashara gani naweza kufanya na nikapata faida mara mbili ndani ya miezi sita?

Ni kazi gani naweza kufanya na nikapata kipato kikubwa ndani ya muda mfupi?

Hayo ni maswali ambayo wengi huwa wanauliza pale wanapo omba ushauri kuhusu mafanikio kwenye biashara au kazi.

Jibu langu kwa wote wanaouliza maswali ya aina hii ni moja, biashara au kazi yoyote ile inaweza kukupa faida au kipato kikubwa sana ndani ya muda mfupi. Lakini kigezo cha kwanza ni umefanya kazi au biashara hiyo kwa muda gani?

Hapo ndipo wengi husahau kuangalia, na wakisikia hadithi za wale waliofanikiwa, ambazo huwa zinaonesha walipoanzia na walipoishia, lakini hazioneshi kilichotokea hapo katikati, huwa wanakimbilia kufanya walichofanya, lakini hawapati walichopata.

Uzoefu ni sehemu muhimu sana kwenye mafanikio yoyote yale, na huu unahitaji muda mrefu kuweza kujijengea.

Mafanikio hayaji kama ajali, bali ni matokeo ya kazi.

Ipo hadithi ya mtu mmoja alikutana na aliyekuwa mchoraji bora kuwahi kutokea, Pablo Picasso mgahawani. Mtu huyo akamwomba Picasso amchore, Picasso akachukua kitambaa cha mezani kwenye mgahawa huo, akamchora mtu yule. Ndani ya dakika moja akawa amemaliza. Aliyechorwa aliangalia picha iliyochorwa, na kufurahi sana, maana ilikuwa imefanana na yeye kama picha ya kupigwa. Picasso akamwambia hapo nitakudai dola elfu kumi (kwa wastani milioni ishirini na), mtu yule akastuka, yaani kitu umefanya kwa dakika moja tu ni kulipe dola elfu moja? Picasso akamjibu, imenichukua miaka 40 ya kuchora, kuweza kufikia ubobezi wa kuchora kwa dakika moja, hivyo hulipii dakika moja, bali unalipia miaka 40 ya uzoefu wangu.

Kwa wale walevi wa hadithi za mafanikio, wakisikia mtu kama Picasso alikuwa analipwa milioni 20 kwa kazi ya dakika moja, watasema uchoraji unalipa kweli kweli, na hapo watakimbilia kuchora, lakini hawajui ni jinsi gani itakuwa vigumu kwao kupata hata asilimia 1 tu ya kipato hicho kwa miaka mingi ya mwanzo.

Mmiliki wa kiwanda alikuwa na tatizo kwenye kiwanda chake, kuna mashine ilikuwa haifanyi kazi. Alileta mainjinia mbalimbali kutatua tatizo la mashine hiyo, lakini hawakuweza kuirudisha kwenye hali yake ya uzalishaji. Akiwa amekata tamaa, alisikia habari ya injinia mmoja mwenye uzoefu mkubwa, akamwita na kumpa kazi mara moja. Injinia yule alianza kazi, aliiangalia mashine kwa muda kisha akachukua nyundo na kugongagonga sehemu fulani na baada ya muda mashine ikawaka na kufanya kazi vizuri. Mwenye kiwanda alifurahi sana na kushangaa kumbe kazi ilikuwa rahisi hivyo. Injinia yule alimwambia anamdai dola elfu moja (wastani tsh milioni 2 na), mwenye kiwanda akashtuka, yaani kugongwa tu ndiyo unitoze fedha nyingi hivyo? Alimtaka amwandikie mchanganuo wa kazi aliyoifanya na jinsi inavyofikia dola hizo elfu 1. Injinia yule akamwandikia mchanganuo wa kazi; kujua sehemu ya kugonga dola 990, kugonga sehemu hiyo, dola 10.

Hapo injinia alionesha kwamba hatozi kile anachofanya, bali anatoza uzoefu ambao amejikusanyia kwa miaka mingi katika kufanya kazi na mashine mbalimbali.

Mifano hii miwili inatuonesha kitu kimoja ambacho wale waliofanikiwa wanakijua lakini ambao hawajafanikiwa hawakijui. Unahitaji muda na uzoefu mkubwa kabla hujaanza kuingiza kipato kikubwa au faida kubwa kupitia kile unachofanya.

Kwa wastani, inamchukua mtu miaka kumi ya kufanya kitu ndiyo aweze kufikia uzoefu wa kumwezesha kuingiza kipato au faida kubwa sana.

Na tunaposema uzoefu siyo wa kuhesabu miaka, bali wa kukua kila mwaka. Maana kuna watu wamefanya kitu miaka kumi, lakini wana uzoefu wa mwaka mmoja uliojirudia miaka kumi, maana kila mwaka wanafanya yale yale.

Uzoefu wa miaka kumi ni pale ambapo kila mwaka unakua zaidi ya mwaka uliopita, unapiga hatua na kuwa bora zaidi. Na hili linafikiwa kwa mambo mawili; kupata maarifa mapya na kuchukua hatua mpya kila wakati.

Mmilikiwa Amazon mwaka 1997 wakati biashara yake bado ni changa. Leo hii ndiye mtu tajiri kuliko wote duniani, akiwa na utajiri unaozidi dola bilioni 130 (zaidi ya tsh trilioni 300)

Tafiti nyingi za wale waliofanikiwa, zinaonesha kwamba wengi walianza kupata mafanikio yao makubwa baada ya kuwa kwenye kile wanachofanya kwa miaka 10. Iwe ni sanaa, michezo, taaluma mbalimbali au biashara, muda ni kitu muhimu katika mafanikio.

Lakini wengi hawapendi kusikia hili, wengi wanapenda zile hadithi za lima matikiti heka moja, ambapo utagharamia milioni mbili na miezi mitatu baadaye ukishavuna unapata milioni 12. Unakimbilia kufanya na unaishia kuumia. Ni kweli wapo wanaoingiza kiasi hicho kwa kilimo kama hicho, lakini siyo ambao ni mara yao ya kwanza kufanya, au mwaka wao wa kufanya. Bali wale ambao wamefanya kwa muda, wamejifunza kwa kina kuhusu kilimo hicho, kuanzia mazingira, hali ya hewa, wakati mzuri wa soko na mengine mengi. Huwezi kulima kwa misimu michache ukajifunza yote hayo.

Hivyo rafiki yangu mpendwa, kama unataka mafanikio makubwa kwenye chochote ulichochangua kufanya, basi muda ni kitu ambacho huwezi kukikimbia, muda ni kitu unachopaswa kukiweka upande wako na kuwa na subira, huku kila wakati ukijifunza vitu vipya kwenye eneo hilo na kuchukua hatua mpya.

Unahitaji miaka kumi ambayo utaweka kazi kweli kweli, lakini hakuna atakayekuona wala kukuzungumzia. Halafu siku moja kila mtu atakuwa anakuongelea na kusema huyu alitoka chini kabisa na sasa yuko juu, lakini hawataangalia miaka 10 uliyowekeza, miaka ya kujifunza na kujaribu na kukosea mpaka ukafika kwenye kilele hicho.

Kadhalika, unaposikia hadithi za wengine wamefanikiwa sana kwenye kazi au biashara wanazofanya, kabla hujakimbilia kufanya ukiamini na wewe utafanikiwa haraka, angalia muda ambao imewachukua tangu wameanza kufanya mpaka walipofikia mafanikio makubwa, utagundua waliowahi sana kufanikiwa ni miaka kumi na, lakini wengi imewachukua miaka zaidi ya 20.

Karibu tusafiri pamoja kwa miaka kumi ijayo.

Rafiki yangu mpendwa, muongo huu ambao tumeuanza mwaka huu (2020 – 2030) ni muongo ambao nimeuchagua wa kufanya makubwa sana kwenye maisha yangu.

Hivyo nakukaribisha kama na wewe unataka kufanya makubwa kwenye maisha yako, basi njoo tusafiri pamoja.

Kwa mafanikio yoyote unayotaka kufikia, kwa ndoto zozote ambazo umewahi kuwa nazo utotoni, njoo nazo ili tusafiri pamoja kwenye muongo huu.

Ninachoamini kwa hakika ni hiki, kama utaweka miaka 10 kwenye kufanya kitu, bila ya kuyumba, bila ya kukata tamaa, basi kwa hakika utafanikiwa mno. Utafanikiwa kwa viwango ambavyo wengine watashangaa sana, ila hawataona miaka 10 uliyowekeza.

Nakualika tusafiri pamoja kwa sababu ni vigumu sana kwenda safari hii peke yako. Na kama huamini hilo, waambie watu ndoto kubwa ulizokuwa nazo utotoni na kwamba sasa umeamua uzifanyie kazi. Watakucheka na kukuambia acha utoto, watakuambia ishi maisha ya kawaida, achana na hayo. Utawasikiliza na kurudi kwenye maisha ya kawaida.

Laini utakapokubali tusafiri pamoja, tutakuwa kwenye jamii ya wale ambao wanaamini kwenye ndoto zao na kuchukua hatua, bila ya kujali ndoto hizo zinawezekana au la. Wanachojua watu hawa ni wanataka nini na wanachukua hatua sahihi za kupata wanachotaka. Ukizungukwa na watu wa aina hii, wewe pia utachukua hatua kwenye ndoto zako kubwa na hutakata tamaa hata kama mambo hayaendi kama unavyotaka.

Miaka 10 ni mingi, ukisafiri peke yako utaishia njiani, karibu sana twende pamoja kwenye muongo huu wa kipekee ambao tumeshauanza.

Njia pekee ya kuweza kusafiri pamoja ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kuwa ndani ya jamii ya tofauti kabisa, jamii ya wasaka mafanikio, ambao wanajua wanachotaka, wanachukua hatua na wana subira ya kufikia mafanikio hayo. Jamii hii inakujenga vizuri na kukuwezesha kukabiliana na kila aina ya vikwazo unavyokutana navyo kwenye safari yako ya mafanikio.

Rafiki, jua kabisa kwamba safari ya mafanikio siyo rahisi, na peke yako utakutana na vikwazo vingi. Unahitaji kuwa eneo ambalo litakupa nguvu ya kupambana na vikwazo hivyo. Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa maelezo yanayopatikana hapo chini, yasome mpaka mwisho.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania