“When you throw a ball up in the air, it doesn’t stay there but returns to the earth; likewise all your good or bad actions will return to you in another form, according to the desire of your heart, no matter which path you take.” — BUDDHIST WISDOM

Ukirusha jiwe angali, baada ya muda litarudi ardhini,
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwa matendo yetu,
Kila tunachofanya, kinarudi kwetu,
Kila tunachotoa kwa wengine, kinarudi kwetu pia.
Hivyo ukiwafanyia wengine wema, wema utarudi kwako.
Na ukiwafanyia wengine ubaya, ubaya utarudi kwako pia.
Asili haisahau wala kupendelea,
Bali inahakikisha kila mtu analipwa kwa kadiri alivyotoa,
Malipo yanaweza kuchelewa au kuwahi, lakini hayapotei kabisa.
Jikumbushe hili kabla hujafanya chochote,
Ukijiuliza je upo tayari kupokea kile ambacho unataka kutoa?
Je upo tayari kufanyiwa kile ambacho unataka kuwafanyia wengine?
Kama jibu ni ndiyo basi fanya na kama siyo usifanye.
Muhimu ni usijisahaulishe au kujiambia hujui madhara ya ulichofanya,
Halafu baadaye wakati unalipwa unaanza kulalamika kwa nini wewe.
Asili inapeleka mambo yake kwa namna ambayo ni bora kabisa,
Hivyo usijaribu kuidanganya, kwani utakuwa unajidanganya mwenyewe.
Kuwa na hakika kwamba kila unachofanya utalipwa hivyo hivyo,
Na chagua kufanya kile ambacho uko tayari kulipwa.
Maisha uliyonayo sasa ni malipo ya yale uliyofanya siku za nyuma,
Na kama unataka maisha yako yawe tofauti kesho, chagua kufanya vitu vya tofauti leo.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania