Rafiki yangu mpendwa,

Mwanga wa jua ukiwaka kawaida unatoa mwangazs tu.

Lakini ukikusanya mwanga huo sehemu moja kwa kutumia lensi, unakuwa na nguvu ya kuweza kuchoma kitu chochote kile.

Ni mwanga ule ule ambao haukuwa na madhara yoyote unapotawanyika.
Ila unapokusanywa pamoja, madhara yake yanakuwa makubwa.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye nguvu tulizonazo.
Kila mmoja wetu ana nguvu za kuweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yake.

Lakini nguvu hizo zimekuwa hazileti matokeo makubwa kwa sababu tunazitawanya sana.
Tunahangaika na mambo mengi kwa wakati mmoja ambayo hayana tija kabisa.

Moja ya faida unayokwenda kuipata kwa kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni kwenda kuzikusanya nguvu zako zote kwenye mambo machache ili uweze kupata matokeo makubwa sana.

Mwaka mmoja unaofuata baada ya semina, ambapo utakuwa chini ya usimamizi wa karibu wa Kocha, utakwenda kuachana na mengi unayohangaika nayo sasa na kuzitawanya nguvu zako.

Utakwenda kuchagua maeneo machache kabisa yenye tija na kuweka nguvu zako zote kwenye maeneo hayo mpaka upate matokeo makubwa kabisa yanayokufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Ni vigumu sana kufanya zoezi hilo ukiwa peke yako, maana vitu vizuri vikija mbele yako siyo rahisi kuviacha, utashawishika tu kuhangaika navyo.
Lakini utakaposhiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 unakwenda kuweka mpango mambo yapi utakayohangaika nayo na yapi utaachana nayo.

Utajua kabisa ni fursa zipi mpya ukikutana nazo unaweza kuzifanyia kazi na zipi utaachana nazo hata kama zinaonekana ni nzuri kabisa.

Rafiki yangu, usikubali kuendelea kupoteza nguvu zako kwa kuzitawanya kwenye mambo mengi yasiyo na tija.
Njoo tukae pamoja tarehe 16 na 17 Oktoba 2021 jijini Dodoma na uweze kuchagua maeneo machache ya kuzikusanya nguvu zako zote, ili mwaka mmoja baadaye uweze kuona hatua kubwa ulizopiga.

Kama bado hujajiwekea nafasi ya kushiriki semina hii muhimu sana kwa mafanikio yako, wasiliana sasa na 0717 396 253 upate nafasi yako mapema.

Kama bado hujakamilisha kulipa ada yako ya kushiriki semina, kamilisha sasa, kwani siku zimebaki chache za kufika ukomo wa kulipa ada.

Na kama ndiyo unasikia taarifa hizi za semina kwa mara ya kwanza hapa, soma hapo chini kupata maelezo zaidi.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz