Rafiki yangu mpendwa,

Kuna laana moja nimekuwa naiona kwenye ukuaji wa biashara za wengi.

Picha huwa linaanza hivi.

Mtu anaanzisha biashara yake ndogo.
Anaipenda kweli kweli na kuifanya kwa moyo sana.

Anawajali sana wateja wake na kuwahudumia vizuri.
Wateja wanaifurahia biashara na kutoa shuhuda zao kwa wengine.

Kitendo hicho kinaleta wateja wengi zaidi kwenye biashara.
Na hapo biashara kuonekana kuwa na fursa ya kukua zaidi.

Mwenye biashara anasukumwa kuikuza zaidi biashara.
Maana wateja wamekuwa wengi, hawezi tena kuwauzia kama mwanzo.

Na hapo ndipo matatizo yanapoanzia.
Pale mtu anapojaribu kuikuza biashara yake zaidi ndipo laana inapoingia na biashara kuanguka vibaya.

Inaonekana ni laana kwa sababu wakati biashara ni ndogo mtu anaiendesha vizuri na kwa mafanikio makubwa.

Lakini biashara inapokua, matatizo yanakuwa makubwa na kupelekea kushindwa kwa biashara hiyo.

Ukweli ni hakuna laana yoyote kwenye hilo, bali kuna kosa moja kubwa ambalo wengi wanaoingia kwenye biashara huwa wanalifanya.

Kosa hilo ndiyo linakuja kuwagharimu sana baadaye wanapojaribu kuchukua hatua za kukuza zaidi biashara hizo.

Iko hivi, wakati biashara ni ndogo, mtu anakuwa mwenyewe kwenye biashara na anadhibiti kila kitu.
Biashara inapokua na kuajiri watu, mtu anakosa udhibiti aliokuwa nao mwanzo.

Mbaya zaidi, alikuwa akiendesha biashara kwa uzoefu wake mwenyewe.
Hivyo hakuweka mfumo wowote wa namna kila anayefanya kazi kwenye biashara hiyo anapaswa kufanya mambo yake.

Kinachotokea ni kila anayeajiriwa kwenye biashara, anafanya kwa namna anavyofikiria au kuweza mwenyewe.

Na hilo ndiyo chanzo cha biashara kufa pale inapokua, kwa sababu wateja hawapati tena huduma nzuri kama walivyokuwa wanapata awali.

Kama umepanga kuikuza biashara yako zaidi ya ilivyo sasa, kuna hatua moja muhimu unayopaswa kuichukua ili kivunja kabisa laana ya biashara kufa pale inapokua.

Hatua hiyo ni kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kwa kushiriki semina hiyo, unakwenda kupata dawa ya uhakika ya kutokomeza kabisa laana hiyo ya biashara kuanguka pale inapokua kwa kasi.

Dawa unayokwenda kuipata kwenye semina hiyo ni kutengeneza mfumo wa kuiendesha biashara yako. Kwa kuwa na mfumo huo, biashara inaweza kuwahudumia vizuri wateja hata kama wewe haupo moja kwa moja.

Uzuri ni kwamba unakwenda kujifunza hilo kwa vitendo na hatua kwa hatua.
Unapotoka kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 unaondoka ukiwa na mfumo wako kamili na kwenda kuanza kuutumia ili biashara yako inufaike sana.

Rafiki, semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2021 siyo kitu cha wewe kukosa kama unataka kukuza zaidi biashara uliyonayo au unayokwenda kuanza.

Njoo tujifunze pamoja Dodoma tarehe 16 na 17 oktoba 2021, na ujiwekee mikakati ya mafanikio utakayofanyia kazi mwaka mzima huku ukisimamiwa kwa karibu na Kocha.

Kama bado hujajiwekea nafasi ya kushiriki semina hii muhimu sana kwa mafanikio yako, wasiliana sasa na 0717 396 253 upate nafasi yako mapema.

Kama bado hujakamilisha kulipa ada yako ya kushiriki semina, kamilisha sasa, kwani siku zimebaki chache za kufika ukomo wa kulipa ada.

Na kama ndiyo unasikia taarifa hizi za semina kwa mara ya kwanza hapa, soma hapo chini kupata maelezo zaidi.

Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.

LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.

MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.

ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.

MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa;  0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.

MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.

HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.

Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.

Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
www.somavitabu.co.tz