2515; Maswali yanayoulizwa mara kwa mara.
Kwa shughuli yoyote unayofanya, iwe ni kazi au biashara, kuna maswali ambayo wale unaowahudumia huwa wanayauliza mara kwa mara.
Kwa kiingereza huwa wanaita FAQ (Frequently Asked Questions).
Haya ni maswali yanayoweza kukukera na kuona kwa nini watu hawaelewi vitu vidogo na vya kawaida kiasi hicho!
Lakini ni fursa nzuri kwako kuweza kutoa ufafanuzi mzuri na kupunguza maswali ya aina hiyo.
Kwa kila swali ambalo watu wanarudia rudia kuuliza, jua kuna kitu ambacho hakijaeleweka hapo.
Hivyo toa maelezo ya kina kwenye kitu hicho ili kupunguza maswali hayo.
Pia unaweza kuandaa majibu ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara ambayo watu watayapitia kabla hawajauliza maswali yao.
Kwa vyovyote vile, watu wanapouliza maswali ya kujirudia rudia ni fursa nzuri kwako kutoa ufafanuzi wa kina ili uweze kueleweka vizuri.
Hatua ya kuchukua;
Kwa kazi au biashara unayofanya, orodhesha maswali ambayo watu wamekuwa wanayauliza mara kwa mara. Yajibu maswali hayo kisha weka majibu hayo kwenye njia ambayo watu hao wanaweza kuyasoma. Inaweza kuwa ni kuyachapa kwenye karatasi, au kuyaweka kwenye tovuti/blog ili waingie na kusoma. Ukishayaandaa, waelekeze watu kuyasoma ili kuelewa zaidi.
Tafakari;
Kama kitu kimoja kinaulizwa na mtu zaidi ya mmoja, tatizo halipo kwa wanaouliza, bali tatizo lipo kwa anayeulizwa. Kila unapokutana na fursa hii ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara, itumie kutoa ufafanuzi wa kina ili watu waweze kuelewa.
Kocha.
嗯嗯
LikeLike