2578; Huhitaji kutumia nguvy nyingi.

Kupumua ni kitu ambacho huwa hakihitaji nguvu kubwa.
Unapojikuta ukitumia nguvu kubwa kupumua, hapo unajua wazi kwamba kuna shida kwenye mfumo wa upumuaji.

Kadhalika kwenye kula na mengine yanayoendelea kwenye mwili.
Huwa yanakwenda yenyewe kwa urahisi kabisa bila kuhitaji nguvu zako kubwa.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye safari ya mafanikio.
Kama unachofanya inabidi utumie nguvu kubwa kujishawishi, kujihamasisha na kujisukuma kufanya ni vigumu kufanikiwa kupitia hicho.

Hiyo ni kwa sababu kinakuwa hakijatoka ndani yako kweli. Na nguvu unazotumia kujisukuma na kujilazimisha kufanya ni nguvu unazozipunja kwenye kukifanya kitu hicho.

Sasa pata picha unashindana na mwingine ambaye nguvu zake zote ameziweka kwenye kufanya na siyo kujilazimisha kufanya.
Hapo unajionea wazi nani atakayeshinda na kufanya makubwa.

Hatua ya kuchukua;
Angalia kila unachofanya, kama inabidi utumie nguvu nyingi kujisukuma na kujilazimisha kufanya, jua siyo sahihi kwako kukifanya.

Tafakari;
Nguvu zina ukomo na uhaba, kuzitumia kujilazimisha kufanya ni kuziondoa nguvu hizo kwenye kufanya, kitu kinachopunguza ufanisi.

Kocha.