2939; Mnatofautiana sana.
Rafiki yangu mpendwa,
Wewe na wafanyakazi uliowaajiri kwenye biashara yako mnatofautiana sana.
Mnatofautiana kimtazamo, wakati wewe unaangalia kujenga biashara ambayo itakuwa kubwa na yenye mafanikio, wao wanachoangalia ni kufanya kazi ya siku husika tu.
Mnatofautiana kiajenda, wakati ajenda yako ni kuhakikisha wanafanya kazi kubwa kwa malipo unayoweza kuwapa, wao ajenda yao ni kufanya kazi ndogo iwezekanavyo kwa malipo unayowapa.
Wakati wewe unaona unawalipa kuliko kazi wanayofanya, wao wanaona wanafanya kazi kubwa kuliko malipo unayowapa.
Mnatofautiana vipaumbele, wakati kipaumbele chako kikubwa kikiwa mauzo na faida kwenye biashara, wao vipaumbele vyao ni tofauti kabisa na mauzo na faida siyo vitu vinavyowanyima usingizi.
Kwa mfano kama huwa mnafunga biashara saa 12 jioni, saa 12 kasoro dakika 5 anakuja mteja. Ni siku ambayo hamjauza sana, wewe unafurahia mteja huyo kuja na upo tayari mzidishe muda wa kufunga ili mteja ahudumiwe vizuri. Lakini wafanyakazi wako watachukia kitendo cha mteja kuja muda wa kufunga na kuhakikisha wanaharakisha kumhudumia ili asiwacheleweshe kutoka.
Wewe ndiye ngozi yako imeingia kwenye mchezo, biashara yako ikifa leo, wewe ndiye unayebeba hasara yote, wao wataenda kutafuta kazi mahali mengine, bila mzigo wa hasara.
Hakuna ubaya wowote kwenye tofauti hizi, ni kitu ambacho kipo na hatuwezi kukikwepa.
Ubaya ni pale watu wanapojisahaulisha na kudhani wao na wafanyakazi wao ni kitu kimoja.
Unaweza kutamani sana wewe na wafanyakazi wako muwe kitu kimoja, lakini kiasili hilo haliwezekani.
Ni vyema kuukabili uhalisia ulivyo kuliko kutaka uwe vile unavyotaka wewe.
Ijue nafasi yako kwenye biashara na usimame hapo, ukihakikisha wafanyakazi wako wanasimama sehemu wanazopaswa kusimama.
Wakati mwingi inahitaji uwalazimishe wafanye kile ulichowaajiri kufanya.
Unaweza kushangaa kwa nini iwe hivyo, kazi waliomba wenyewe na sasa umewapa ila hawataki kuifanya.
Ni tofauti zilizopo kati yenu.
Weka viwango vyako vya kibiashara na hakikisha kila aliye kwenye biashara yako anavifikia.
Anza wewe mwenyewe kwa kuvifikia kisha usiwe na huruma kwa asiyevifikia.
Wafanyakazi watasukumwa kuvifikia viwango hivyo au watashindwa na kukimbia hivyo kuacha nafasi kwa wanaoweza.
Wafanyakazi wako kwenda kinyume na wewe, kukupinga, kukuibia, kukwepa majukumu na hata kukukwamisha kusikuumize. Hawana ubaya wowote na wewe, ni vile tu ajenda zenu zinatofautiana.
Wajibu wako ni kuhakikisha kuna ajenda moja tu inayofanyiwa kazi kwenye biashara yako, ajenda yako.
Wafanyakazi wako hawatafurahia kitendo cha ajenda yako kutawala na ajenda yao kukosa nafasi.
Lakini wewe unachowapa ni kazi, furaha wanapaswa kuitengeneza wenyewe.
Kama pia unataka kumfurahisha kila mtu kwenye biashara, hutakuwa na biashara na hutakuwa na furaha.
Kama ambavyo huwezi kuwabadili mwewe wasile kuku, ndivyo pia huwezi kuziondoa tofauti zilizopo kati yako na wafanyakazi wako kwenye biashara yako.
Ujue uhalisia huo na kuuishi, itakupunguzia sana msongo wa mawazo.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana Kocha Dr.Makirita Amani.
LikeLike
Asante sana Kocha nimeisoma hii makala na nimeelewa sana na nitazingatia miongozo uliyotoa. Ni kweli furaha ya wafanyakazi waitafute wenyewe, muhimu ni kuchapa kazi kwa lengo moja la mauzo na uchapakazi,
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr Makirita Amani.
Hakika nimejifunza kitu kutoka kwenye makala hii ya leo, unachoandika ni kweli kabisa.
Nimekumbuka hii point “wanaomba kazi unawapa, lakini hawataki kabisa kufanya majukumu yao” binadamu ni hatari sana.
#NidhamUpendo
LikeLike
Ni changamoto kubwa
LikeLike
Hakika tunatofautiana, muhimu ni kuweka viwango vyangu na kuvisimamia, asante Sana kocha kwa makala hii ya kuendelea kujitambua zaidi kibiashara na ukuaji kwa ujumla.
LikeLike
Nikweli tunatofautiana sana
LikeLike
Ahsante sana kocha , hakika leo nimeongeza elimu kummmbe tofauti zinazoonekana zote ni za kawaida
LikeLike
Tunatofautiana
LikeLike
Mimi na wafanyakazi wangu tunatofautina, nitahakikisha agenda yangu ndiyo inakuwa kuu.
Mimi nawapa kazi wafanyakazi ila siyo furaha.
LikeLike
Asante kocha,
Agenda zetu zinatofautiana sana na kimsingi hata nifanyneje sitaweza kuaazimisha tuwe na ajenda moja la mujimu ni watekeleze ajenda yangu ambayo ndio imewafanya watake kazi,furaha wataipata wakiwa nje ya ajenda yangu
LikeLike
Weka viwango vyako vya kibiashara na hakikisha kila aliye kwenye biashara yako anavifikia.
Anza wewe mwenyewe kwa kuvifikia kisha usiwe na huruma kwa asiyevifikia. Hii imeenda
LikeLike
Safi, tekeleza.
LikeLike