2968; Sizitaki mbichi hizi.
Rafiki yangu mpendwa,
Bila shaka unakumbuka moja ya hadithi ambazo tulijifunza shuleni.
Ambapo sungura aliziona ndizi, akaamua azirukie ili aweze kula.
Akaruka na kuruka sana, lakini hakuweza kuzifikia.
Akakazana kuruka tena na tena, lakini bado hakuzifikia ndizi hizo.
Mwisho akajiambia hata hivyo ndizi zenyewe ni mbichi, sizitaki.
Kwa kusoma hadithi hiyo fupi unaweza kumcheka sungura kwa jinsi anavyojidanganya baada ya kukosa kitu alichotaka.
Lakini je umewahi kukaa chini na kufikiria jinsi ambavyo wewe mwenyewe umekuwa unajidanganya pale unapokosa ulichotaka au hata tu kukutana na changamoto kwenye mchakato wa kukipata?
Unapanga kabisa unataka kupata matokeo ya aina fulani, kisha unajua hatua unazopaswa kuchukua ili kupata matokeo hayo.
Unaanza kuchukua hatua hizo na unakutana na magumu na changamoto zinazokuwa kikwazo kwako kupata unachotaka.
Katika hali ya kawaida unafanya nini pale unapokutana na magumu na changamoto hizo?
Unakata tamaa na kuona haiwezekani.
Na hapo ndipo unakuwa mjanja kuliko hata sungura.
Unaanza kujiambia ni kitu kisichowezekana.
Unajiambia hata hivyo siyo muhimu sana.
Unaona kuna mengine muhimu zaidi na kwenda kuyafanya.
Huo ndiyo mzunguko ambao wengi wamekuwa nao maisha yao yote.
Na kwa sababu hakuna kitu ambacho hakina changamoto, wengi wamekwama kufanikiwa kwa sababu ya kuhangaika na mambo mapya kila wakati.
Sasa rafiki yangu, ipo njia ya kukuzuia usijidanganye kama sungura.
Njia hiyo ni kukaa chini na kuandika kabla hujakimbilia kufanya.
Unaandika mpango wako mzima wa kile unachokwenda kufanya.
Na pia unaandika sababu za kwa nini unafikiri ni muhimu kufanya hayo uliyopanga kufanya.
Andika matokeo unayotegemea kupata katika kukifanya.
Na pia andika changamoto na magumu unayoweza kukutana nayo katika kufanya.
Kwa njia hii ya kuandika ni rahisi kurejea kwenye sababu za wewe kufanya kitu na matarajio uliyokuwa nayo.
Kwa kukutana na ugumu, hakuondoi sababu za wewe kuamua kufanya wala matarajio uliyokuwa nayo.
Maandiko yanakuzuia usijidanganye na kukimbilia kuacha ulichopanga kwa sababu tu umekutana na magumu na changamoto.
Hii inakuwezesha ukae kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu kabla hujakimbilia kwenye vitu vingine pale unapokutana na magumu na changamoto.
Hakuna chochote utakachofanya ambacho hutakutana na magumu na changamoto.
Sisi binadamu ni rahisi kusahau sababu ya kufanya kitu pale tunapokutana na magumu na changamoto.
Kwa kuwa na tabia ya kuandika sababu za kufanya kitu na matokeo unayotarajia, unajizuia usijidanganye na kuacha pale unapokutana na magumu na changamoto.
Ni heri ujiambie wazi umechoka kuzirukia hizo ndizi kwa sababu zipo mbali kuliko ulivyotegemea.
Kuliko kujiambia kwamba ni mbichi, kwani mwanzo wakati unaamua uzirukie hukuziona ni mbichi?
Kuna sababu za kila tunachoamua kufanya, tusipoziweka bayana sababu hizo, ni rahisi kuzisahau na kujifanganya ambapo hakuna manufaa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kuandika Kuna nguvu kubwa sana ya kufanya maajabu kwenye jambo lolote mtu analofanya.
LikeLike
Hakika,
Ndiyo maana mikataba tunaandika.
Tujiwekee mikataba kwetu wenyewe kwa kujenga utaratibu wa kuandika.
LikeLike
Tafuta sababu kwenye Kila unachotaka kufanya, magumu na matokeo utakayopata. Hii itakusaidia kutokukata tamaa hata pale unapokutana na magumu.
Asante sana
LikeLike
Ukijua kwa nini ulianza na matokeo gani unategemea kuzalisha, haitakuwa rahisi kukatishwa tamaa na yale unayokutana nayo.
LikeLike
Ahsante kocha, kama kuna jambo la uhakika kabisa ni magumu na changamoto wakati wa safari.
LikeLike
Hiyo ndiyo gharama halisi ambayo lazima tulipe kwenye hii safari ya mafanikio.
LikeLike
Asante naona pia nguvu iliyopo kwa kurudia rudia kuandika malengo yangu ya mwaka.
LikeLike
Vizuri sana,
Kuandika kila mara inafanya tusisahau.
Lakini pia inafungua akili kuziona fursa zinazoendana na malengo tuliyonayo.
Tufanye hivyo kila wakati.
LikeLike
Hakuna chochote utakachofanya ambacho hutakutana na magumu na changamoto
LikeLike
Magumu na changamoto ni sehemu ya maisha, tusipokuwa tayari kukabili hali hizo hakuna hatua tutakayopiga.
LikeLike
Asante Kocha,
Nitaandika sababu za kila ninachoenda kukifanya ili nikaea kwenye mchakato hata pale ninapokutana na changamoto.
LikeLike
Vizuri, ukiandika huwezi kujifanganya pale mambo yanapokwenda tofauti.
LikeLike
Kupitia kuandika malengo,sababu za kwani I nifanye na matokeo ninyo yatarajia vitanisaidia kurudi kwenye lengo kuu. Asante sana .
LikeLike
Bila kuandika ni rahisi kujifanganya pale mambo yanapokuwa magumu.
LikeLike
Changamoto zipo ili kutuimarisha na sipaswi kuzikimbia changamoto kwa kufanyajambo lingine bali napaswa kuikabidhi changamoto na kujifunza kutokana na changamoto hiyo ili niweze kupiga hatua zaid.
Asante kocha
LikeLike
Kweli kabisa,
Tukae humo.
LikeLike
Asante Kocha kwa ujumbe huu. Kama nimechoka Afadhali nipumzike na kurudi kuzirukia tena kuliko kujidanganya kuwa ndizi hizo ni mbichi
LikeLike
Zingekuwa mbichi mwanzo usingerukia.
Ndiyo maana ni muhimu tuandike, ili uchovu usitudanganye.
LikeLike
Hakika kocha maandiko yanasaidia kukaa kurudi kwenye kile ulichokua unafanya kama ulifanya utafiti wa kutosha na kuamua kukifanya.
LikeLike
Kuandika ni kuingia mkataba na sisi wenyewe.
LikeLike
Sizitaki mbichi hizi ni kukata tamaa.
LikeLike
Ni kweli ni kukaa chini na kua ndika kila unachofanya na kutafakari
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Na kukata tamaa ni dhambi kubwa sana kwenye safari ya mafanikio.
LikeLike
Kuandika mpango wa kile ninachotaka kufanya+kuandika sababu zinazonisukuma kufanya kitu hicho + kuandika matokeo ninayotarajia + changamoto ninazoweza kukutana nazo = Na kukomaa kupata matokeo licha ya magumu nitakayokutana nayo.
LikeLike
Magumu yatakuwepo, lakini tukiwa na KWA NINI KUBWA, hayawezi kutuzuia.
LikeLike
Na kwa sababu hakuna kitu ambacho hakina changamoto, wengi wamekwama kufanikiwa kwa sababu ya kuhangaika na mambo mapya kila wakati.
LikeLike
Ukiwa nje unaweza kuona upande mwingine ni rahisi, ni mpaka uingie ndiyo unagundua changamoto zipo kila mahali.
LikeLike
Najizuia nisisahau malengo na mipango yangu pale ninapokutana na magumu na changamoto kwa kuziandika. Asante Kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Najizuia nisisahau malengo na mipango yangu pale ninapokutana na magumu na changamoto kwa kuziandika.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Weka KWANINI KUBWA KULIKO MATEGEMEO Ya kufanya unachokitafuta. Hutaweza kuacha mpaka ukipate. Usikate tamaa maana kukata tamaa ni dhambi. Zijue na kuziorodhesha changamoto zote ili uweze kuzikabili bilankuweka visingizio.
Andiko Bora Sana hili.
LikeLike
KWA NINI KUBWA ina nguvu ya kuvuka chochote tunachokutana nacho.
LikeLike
Nitaendelea kuyatafuta mafanikio makubwa hata kama nitakutana na changamoto zozote!
LikeLike
Hakuna kuyumbishwa na chochote.
LikeLike
Unaandika sababu na unazirudia kuzisoma mara kwa mara wakati unaendelea na mchakato.
LikeLike
Na kurudia kuziandika pia ili usijisahaulishe pale mambo yanapokwenda tofauti na mategemeo.
LikeLike
Jua sababu ya kufanya na ukifanye kitu hicho ili uweze kulipa gharama zake
Asante
LikeLike
KWA NINI KUBWA, lazima uijue na kuitumia kama kichocheo.
LikeLike
Siraha ya kuaminika ya kukukinga na janga la kuachana na Marengo unayopambana kuyafikia ni :
Kuziandika sababu HALISI za kwanini umeamua kufanya
Jambo Hilo. Pia kuandika kwa usahihi matokeo utakayo
yapata na jinsi utakavyonufaika nayo. na pia kuandika ChangaMoto zote zinazoweza kujitokeza na jinsi utakavyozikabili. Baada ya kuziandika ni kuzisoma kila wakati , na kwa kufanya hivyo unakuwa ndani ya ulinzi wa
Kutimiza Marengo yako. Asante kocha
LikeLike
Hakika,
Mambo hayatakuwa rahisi, lakini kwa kujua kwa nini ulianza, utapambana mpama ukamilishe.
LikeLike
Njia ya kukuzuia usijidanganye kama Sungura
1. kaa chini na andika kabla hujakimbilia kufanya
2. andika mpango wako mzima wa kile unakwenda kufanya
3. andika sababu kwa nini unafikiri ni muhimu kufanya hayo uliyopanga kufanya
4. andika matokeo unayotegemea kupata
5. andika changamoto na magumu unayoweza kutana nayo wakati wa kufanya.
LikeLike
Vizuri na 6. Unapokutana na changamoto, rudi kusoma uliyoandika. Hiyo itakupa nguvu ya kuendelea na kuepusha usijidanganye na kuacha.
LikeLike
Ni heri kujiambia ukweli kuliko kujidanganya.
Kila kitu kina changamoto, muhimu ni kukabiliana na changamoto badala ya kukimbia changamoto na kujifariji.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Hakuna mtu rahisi kumdanganya kama wewe mwenyewe.
Tujiweke kwa namna ambayo hatuwezi kujidanganya.
LikeLike
Ni kupitia kuandika malengo yangu mara kwa mara nitaiona nguvu ya kuandika.
LikeLike
Kabisa, kadiri unavyorudia kuandika ndivyo yananasa kwenye akili yako.
LikeLike