3045; Afya yako ya akili.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye safari ya mafanikio, afya yako ya akili ni rasilimali muhimu sana unayopaswa kuilinda.
Safari ya mafanikio imejaa vikwazo na changamoto za kila aina.
Usipokuwa imara kuvuka hayo, yatakuchosha haraka sana na kujikuta ukikata tamaa.
Ili kuimarisha afya yako ya akili, zingatia mambo haya yafuatayo;
1. Usiwe na matarajio makubwa sana kwa watu wengine. Kadiri unavyokuwa na matarajio makubwa, ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi ya kuangushwa.
2. Usiwe na mategemeo makubwa kwenye mambo ambayo yapo nje ya uwezo wako.
3. Jua hakuna mtu aliyekamilika, kila mtu ana changamoto zake. Hivyo nenda na wale ambao manufaa wanayokupa ni makubwa kuliko changamoto zao.
4. Waamini watu, lakini wape nafasi ya kukosea au kukuangusha kwenye yale unayowaamini.
5. Jua kila mtu ana maslahi yake binafsi na kila anachofanya ni kuhakikisha anayatimiza maslahi hayo.
6. Usiseme wala kufanya chochote ukiwa na hisia kali za hasira au furaha.
7. Usiwe na kinyongo na mtu yeyote yule, hata kama amekufanyia nini. Kama kuna watu umeona hawakufai tena kwenye safari yako ya mafanikio, wafute kwenye fikra zako, ila endelea kuwaheshimu kwa utu wao. Usitake kumkomoa yeyote, peleka muda wako kwenye mambo muhimu kwako.
8. Unapoomba ushauri jiulize kama unataka kweli kusikia vitu tofauti au unataka mtu wa kukubaliana na mawazo uliyonayo.
9. Unapotoa ushauri jiulize kama unayempa anataka kusikia vitu vipya au anataka ukubaliane na mawazo yake.
10. Maneno kidogo, kazi zaidi. Watu hawasikilizi sana unachosema, bali wanaangalia sana unachofanya.
11. Tekeleza zaidi ya ulivyoahidi. Pambana sana usivunje ahadi ulizotoa.
12. Jua hakuna anayeyafikiria maisha yako kama wewe. Hakuna anayekujali kuliko wewe mwenyewe.
13. Chagua vyema watu unaoshirikiana nao, ili wawe na mchango sahihi kwako. Usichukue mtu ni mtu, kuwa na vigezo unavyotumia kuchagua watu utakaoshirikiana nao.
14. Jua kila mtu anadanganya, kila mtu, hasa wale wanaosema ni wakweli watupu. Watu ni wabinafsi na wanaweka mbele maslahi yao kwa namna yoyote ile, hata ikibidi kwa kudanganya.
15. Huoni vitu kama vilivyo, bali unaviona jinsi ulivyo wewe. Unachoona wewe ni tofauti na wanavyoona wengine.
16. Kazi ndiye rafiki wa kweli, ambaye hawezi kukuangusha. Penda sana kazi yoyote unayoifanya.
17. Epuka starehe zenye raha ya muda mfupi, vitu kama ulevi vitakuchosha sana.
18. Puuza mambo yote ambayo hayana mchango kwako kupata kile unachotaka. Weka juhudi zako kwenye mambo machache na yenye tija.
19. Kabla hujafanikiwa watu watakudharau sana, ukifanikiwa watu watakuchukia sana.
20. Kuwa na muda wa kufanya tahajudi (meditation) na tafakari mbalimbali. Hii inatuliza sana akili yako.
21. Kuwa na muda wa kuyaandika mawazo yote unayokuwa nayo kwenye akili yako.
22. Wasamehe watu hata kama hawajakuomba msamaha. Waombe watu samahani hata kama kosa siyo lako moja kwa moja.
23. Unapokuwa na hofu kwenye jambo lolote jua ni hali ya kawaida unapokuwa unakabiliana na mambo mapya, usiruhusu hofu iwe kikwazo kwako kufanya.
24. Kuwa wewe na walio sahihi kwako watakuelewa. Usitake kumridhisha kila mtu, hilo huliwezi.
25. Kuwa na subira, mambo yote mazuri yanahitaji muda kujijenga.
26. Usijilinganishe na mtu yeyote yule, hakuna unachofanana na wengine.
27. Usiruhusu watu wakajua kila kitu kuhusu wewe, hasa matatizo na changamoto zako, wengi watafurahia hali hiyo. Na hata wakijua mafanikio yako, itawajengea tu wivu.
28. Sema HAPANA kwenye mambo yote ambayo hayana mchango kwenye kuyafanya maisha yako kuwa bora.
29. Huwezi kumbadili mtu yeyote, hata ufanye nini. Watu wanabadilika kama wataamua wao wenyewe.
30. Vitu vitatu ambavyo hupaswi kuviweka wazi kwa kila mtu; afya yako, utajiri wako na mahusiano yako ya ndoa/mapenzi.
Afya yako ya akili ni kitu cha kukipa kipaumbele kikubwa sana. Kila wakati jikague kwenye afya yako ya akili, kupitia kuyaandika mawazo unayokuwa nayo na kuchukua hatua sahihi za kujenga utulivu ndani yako na kujali mambo yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ahsante sana kocha, nitayazingatia haya siku zote kwaajili yabustawi wa afyabyangu ya akili
LikeLike
Vizuri.
Kila la kheri.
LikeLike
Kabla hujafanikiwa watu watakudharau sana, ukishafanikiwa watakuchukia sana.
Hao ndio binadamu.
LikeLike
Hawaeleweki, hivyo usikazane kuwaelewa, wewe fanya yako.
LikeLike
Umuhimu wa kufuatilia Afya ya Akili
LikeLike
Ni muhimu sana kwa utulivu kwenye hii safari ya mafanikio.
LikeLike
Vitu ambavyo sipaswi kuviweka wazi kwa kila myu ni afya yangu,utajiri wangu na mahusiano yangu ya ndoa au ya kimapenzi,na haya ndio mambo ambayo watu wengi wnaapenda kuyajua hasa kwenye dunia tuliyo nayo sasa na wakishayajua watanidharau au kunichukia.
Asante sana kocha kwa kunikumbusha mambo haya muhimu na ya msingi sana kwenye maisha yangu.
LikeLike
Yazingatie hayo.
LikeLike
Hakika afya ya akili ni ya muhimu sana, nitajitahidi kulinda afya ya akili yangu. Asante kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha, nitajitahidi kuzingatia hayo kwa ajili ya afya yangu ya akili na zaidi kwa kuyarudia rudia ili kujifunza zaidi.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Shukrani Kocha kwa makala hii, ina mafunzo mengi mbalimbali yatakayonisaidia ktk safari yangu ya ubilionea.
LikeLike
Yazingatie.
LikeLike
asante kocha kwa mambo 30 muhimu ya kuzingatia wakati tunaendelea na safari ya kufikia
ubilionea.
tunahitaji sana afya ya akili mno.
god bless us.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni mambo ya msingi kabisa.Kuwa na utulivu wa akili.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani kwa mambo haya uliyoshirikisha hapa.
Afya ya akili ni muhimu sana katika safari yetu ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kweli hii ni makala yenye tiba ya akili
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
. Huwezi kumbadili mtu yeyote, hata ufanye nini. Watu wanabadilika kama wataamua wao wenyewe
Asante sana
LikeLike
Huo ndiyo ukweli.
LikeLike
Asante kocha,Mafanikio yangu yatatokana na uimara na Ubora wa Afya yangu ya Akili.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kazi ndiye rafiki wa kweli, ambaye hawezi kukuangusha. Penda sana kazi yoyote unayoifanya.
Kabla hujafanikiwa watu watakudharau sana, ukifanikiwa watu watakuchukia sana.
Huwezi kumbadili mtu yeyote, hata ufanye nini. Watu wanabadilika kama wataamua wao wenyewe.
LikeLike
Tuyazingatie haya.
LikeLike
Asante sana kwa hekima hizi ulizotushirikisha
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Usikubali kubeba kinyongo muombe msamaha hata kama hujamkosea
Kazi ndiyo rafiki wa keli
Usikubali kuweka Mambo yote wazi kwa kila mtu
Usitoe ushauri ambao hujaombwa
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Kweli tahajudi inatuliza akili.
LikeLike
Tuitumie kupata utulivu.
LikeLike
Nitailinda afya yangu ya akili kwa namna yyte ile.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana kocha.
Ni kweli, afya yangu Ya akili Ni muhimu sana kwenye Safari ya mafanikio hivyo basi napaswa kuilinda
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana Kocha afya yangu ya akili mi muhimu kuliko jambo lolote lile.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Afya yangu ya akili ni muhimu sana kila wakati tiakuwa na muda wa kuyaandika mawazo yangu yote, na kufanya tafakari na tahajudi.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike