3119; Watu, matatizo, biashara, fedha.
Rafiki yangu mpendwa,
Hii dunia ina watu,
Watu hao wana matatizo mbalimbali.
Biashara zenye mafanikio huwa zinajengwa kwenye msingi wa kutatua matatizo ambayo watu wanayo.
Na fedha nyingi inaweza kutengenezwa kupitia biashara inayotatua matatizo ya watu.
Hayo maelezo hapo juu yamebeba kila kitu ambacho mtu anapaswa kukijua ili kujenga biashara yenye mafanikio makubwa.
Lakini watu huwa wanapenda kufanya mambo kuwa magumu na hilo linapelekea wapoteze muda na nguvu kwenye mambo yasiyokuwa na tija yoyote.
Ukiingia kwenye biashara kwa ajili ya kutatua matatizo ambayo watu wanayo, utaweza kutengeneza fedha kwa ukubwa na wingi.
Lakini ukiingia kwenye biashara kwa ajili ya kupata fedha, utaishia kuwa na matatizo.
Hii ni kanuni ambayo inafanya kazi kwa mafanikio makubwa mara zote.
Kama unataka kujenga biashara yenye mafanikio, anza na matatizo ambayo tayari watu wanayo.
Kila mara iangalie biashara yako kwenye mtiririko huu;
Anza na watu, dunia haitakosa watu.
Nenda kwenye matatizo ambayo tayari wanayo, kadiri matatizo yanavyokuwa makubwa, ndivyo manufaa yanavyokuwa makubwa pia.
Jenga biashara kwenye misingi ya kutatua matatizo ya watu uliyochagua kuyatatua. Asiwepo mwingine anayeweza kutatua matatizo uliyoyalenga kama wewe.
Kuwa na usimamizi mzuri wa mzunguko wa fedha kwenye biashara yako ili kupata mafanikio unayoyataka.
Usizidishe ugumu wa maisha yako kwa kuhangaika na vitu ambavyo huna uhakika navyo.
Rahisisha mchakato wako mzima wa kujenga biashara yenye mafanikio makubwa na fanyia kazi mchakato wako kwa msimamo bila kuacha.
Kama tayari ulishaanza biashara bila ya kuzingatia hii misingi uliyojifunza hapa, bado hujachelewa, anza sasa kufanya hivyo.
Biashara inaweza kukupa kiasi chochote cha fedha unachotaka, kama itajengwa kwenye msingi wa kutatua matatizo makubwa ambayo watu wengi wanayo.
Tuzingatie hilo kwa umakini mkubwa sana na tutaweza kufanya biashara kwa mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante kocha, nitaendelea kutatua matatizo ya watu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Biashara inaweza kukupa kiasi chochote cha fedha unachotaka, kama itajengwa kwenye msingi wa kutatua matatizo makubwa ambayo tayari watu wanayo.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Asante Kocha Kwa makala hii kweli biashara unaweza kukupa fedha zote unazotaka kama utazingatia misingi hii ya kutatua matatizo ya watu wengi
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ni kweli anza kwanza na matatizo ambayo tayari watu wanayo then toa thamani nakwa kutatua matatizo hayo na watu watakupa fedha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Biashara inaweza kukupa kiasi chochote cha fedha unachotaka, kama itajengwa kwenye msingi wa kutatua matatizo makubwa ambayo watu wengi wanayo.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante Kocha,
Msingi wa biashara yenye mafanikio ni kutatua matatizo ya watu. Fedha nyingi inatengenezwa kupitia biashara inayotatua matatizo ya watu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha, nitaendelea kutatua matatizo ya watu kupitia biashara ninayoifanya, nakumbuka hata kipindi cha Korona watu waliingiza fedha kwa kutatua matatizo yatokanayo na korona kwa kipindi hicho
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Biashara yenye mafanikio inajengwa kwa kutatua matatizo ya watu.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Dunia imejaa matatizo, tatua matatizo ya watu nawe utapata unachokitaka.
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha,Inabidi biashara ninayoifanya itatue matatizo ya watu walionao sio kuweka kipaombele kwenye fedha.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Unajenga biashara kwa kutatua matatizo ya watu,
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kama nataka kupata fedha, basi nitaanza kwa kuweka nguvu zaidi kwenye kutatua matatizo ya watu na sio kuzipata hizo fedha na hapo fedha zitaanza kuja zenyewe, asante mwandishi
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Je ni tatizo au matatizo Gani biashara yangu inatatua?
Hapa ndipo palipo na mafanikio
Biashara yangu inatatua tatizo ambalo ni njaa na ni hitaji la kila mtu kupata chakula,hakuna anayeweza kuishi bila kula
Siyo kula tuu Bali kula chakula Bora na Kwa wakati
Tatizo lingine watu walilonalo ambalo linatatuliwa na biashara yangu ni muda
Kwa kutoa huduma ya chakula Kwa wakati basi tunakuwa tumeokoa muda Wa wateja wetu ambao tutakuwa tumewasaidia sana.
Tatizo lingine ni maarifa sahihi juu ya ulaji sahihi
Hivyo biashara yangu Kwa kutoa maudhui mbalimbali juu ya ulaji sahihi basi inawasaidia watu kufanya maamuzi sahihi juu ya afya zao.
Kwetu sisi afya ya mteja wetu ndio kipaumbele chetu
LikeLike
Umeeleza vyema, tekeleza.
LikeLike
Kila mara nitaiangalia biashara kwa mtiririko huu:
1. Watu
2. Matatizo yao
3. Kujenga Biashara inayotatua matatizo yao
4. Kusimamia mzunguko wa fedha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike