Rafiki yangu nikupendaye katika falsafa ya Ustoa,
Kwenye falsafa ya Ustoa, tabia njema ni moja ya misingi muhimu sana kwenye falsafa ya Ustoa. Kila mtu anapenda kuonekana ana tabia njema na changamoto kubwa kwa watu wengi ni jinsi ya kujijengea hizo tabia njema.
Kadiri unavyojijengea na kuishi tabia njema, ndivyo unavyojitengenezea maisha bora na yenye furaha wakati wote.
Huwezi kuwa na furaha kama huna tabia njema kwa sababu tabia njema ndiyo zao la furaha.
Sasa unaweza kujiuliza je, hizo tabia njema zenyewe ndiyo zipi?
Kwenye falsafa ya Ustoa, tabia njema ni pale unapoishi na kusimamia yale yenye maana kwako na kwa wengine, na kuachana na yale yasiyo na maana.
Habari njema ni kwamba, kwenye falsafa ya Ustoa, kuna tabia njema kuu nne, ambazo ni hekima, ujasiri, haki, kiasi.
Kwenye HEKIMA; ni ubora katika maeneo mawili, moja kufikiri na na kufanya maamuzi.
Kwenye UJASIRI; ni uwezo wa kukabiliana na hatari kwa usahihi.
Kwenye HAKI; ni ubora katika mahusiano yetu na wengine au wale tunaohusiana nao.
Kwenye KIASI; ni uwezo wa kudhibiti hisia na tamaa.
Nukuu;
If you can find anything in human life better than justice, truthfulness, selfcontrol, courage […] turn to it with all your heart and enjoy the supreme good that you have found […] but if you find all other things to be trivial and valueless in comparison with virtue, give no room to anything else, since, once you turn towards that and divert from your proper path, you will no longer be able without inner conflict to give the highest honour to what is properly good. It is not right to set up as a rival to the rational and social good anything alien to its nature, such as the praise of the many, or positions of power, wealth, or enjoyment of pleasures. – Marcus Aurelius, Meditations, 3.6
Kama unaweza kupata kitu bora kwenye maisha ya mtu zaidi ya haki, ukweli, kujidhibiti na ujasiri, kishikilie sana kitu hicho. Lakini kama utakuta vitu vingine ni visivyo na maana ukilinganisha na tabia njema, usitoe nafasi kwa kitu kingine bali tabia hizo njema. Kwa sababu utakapoacha njia yako sahihi hutaweza tena kuzingatia yale ambayo ni mazuri kwako. Siyo sahihi kuleta upinzani kati ya fikra sahihi na vitu vya nje kama sifa kutoka kwa wengine, nafasi za madaraka, utajiri na kufurahia raha.
Rafiki yangu mstoa, kama alivyosema mwanafalsa Marcus Aurelius, unapaswa kuwa mtu wa kusimamia haki, unaposimamia haki utaweza kujenga na kuimarisha mahusiano yako na wengine. Kwenye haki tunapimwa na kitu kimoja tu nacho ni ubora wa mahusiano yetu na wengine. Sisi ni viumbe vya mahusiano kadiri ya vina saba (DNA) hivyo umezungukwa na watu, jua jinsi ya kutumia haki ili uweze kuwa na mahusiano bora kwako binafsi na kwa wengine.
Ubora kwenye mahusiano yetu siyo ukamilifu. Bali ubora wa mahusiano yetu ni kuweza kuishi na wale tunaohusiana nao kwa jinsi walivyo na siyo kutaka kuwabadilisha. Ukitaka kubadilisha watu, tegemea kushindwa, angalie kile ambacho unanufaika kutoka kwa mtu na kitumie hiko kufanya mahusiano yenu kuwa bora zaidi.
Ishi ukweli, kama kitu siyo kweli usiseme. Na simamia ukweli utakuweka huru.
Jifunze kujidhibiti wewe mwenyewe, UKISHINDWA kujidhibiti utakosa kiasi kwenye maisha yako. Maisha yanahitaji uwe na kiasi, na kiasi ndiyo asili ya dunia, angalia asili jinsi inavyojiendesha kwenye kila kitu ina kiasi bila kiasi tutaweza kuharibu furaha zetu. Jifunze kujidhibiti, huwezi kufa kwa kujidhibiti kwenye mahitaji ya msingi ya binadamu na kuachana na anasa za maisha.
Ukikosa kiasi, utaicha dunia mapema, endesha maisha yako kwa kiasi ni moja ya tabia njema kwenye falsafa ya Ustoa, hata kama unacho, usitumie kupitiliza bali kila wakati jikumbushe kwamba unahitaji kiasi, na ishi kwa kiasi.
Ukikutana na kitu ambacho kipo nje ya tabia njema, usitoe nafasi kwa kitu hicho. Ukianza kuishi vitu ambavyo havina maana ukilinganisha na tabia njema unaanza kukaribisha matatizo, usiruhusu matatizo mengine, yale uliyonayo tayari yanakutosha.
Hatua ya kuchukua leo; ishi tabia njema, na tabia njema ni pale unapoishi na kusimamia yale yenye maana kwako na kwa wengine, na kuachana na yale yasiyo na maana.
Sina uhakika kama itakufaa lakini pale utakapoacha njia yako sahihi hutaweza tena kuzingatia yale ambayo ni mazuri kwako.
Mara zote fanya kile kilicho sahihi na kuwa na tabia njema.
Mstoa Mwenzako,
Mwl Deogratius Kessy
Mara zote fanya kilr kilicho sahihi na fanya tabia njema
LikeLike
Ishi ukweli, kama kitu siyo kweli usiseme. Na simamia ukweli utakuweka huru.
Asante sana Mwl.Deo
LikeLike
Mara zote mtajitahidi kujijengea tabia njema bila tamaa
LikeLike