3156; Hakuna ‘ni mara moja tu’.
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa tunaweka malengo na mipango mbalimbali ya mambo gani tutafanya na yapi ambayo hatutayafanya.
Tunafanya hivyo kwa nia njema kabisa ya kuweza kupiga hatua ambazo tumepanga kupiga.
Lakini inapokuja kwenye utekelezaji, mambo ndiyo huwa magumu sana kufanya kama ulivyopanga.
Mtu unashawishika kwenda kinyume na utaratibu ambao alijiwekea yeye mwenyewe.
Mtu anafanya hivyo akijiambia ni mara moja tu anafanya au kutokufanya tofauti na alivyokuwa amepanga.
Kitu ambacho mtu anakuwa hazingatii ni kwamba kama mtu akiweza kufanya mara moja, ni rahisi kufanya kwa mara nyingine na nyingine na nyingine zaidi.
Na hapo ndipo mtu anapovunja malengo na mipango aliyokuwa amejiwekea, kwa sahabu tu ya kuanza mara moja.
Ni rahisi sana kusimamia kitu kwa asilimia 100 kuliko kusimamia kwa asilimia 99.
Ukiwa hujavunja yale uliyojipangia inakupa nguvu ya kuendelea bila kuvunja.
Lakini ukishavunja hata mara moja, unashawishika kuvunja tena na tena.
Ukishapanga yale utakayofanya au kutokufanya unapaswa kufuta sababu zote nzuri zinazokushawishi kwenda kinyume na malengo na mipango yako.
Usikubali hata kidogo kwenda kinyume na ulivyopanga.
Kwa sababu ukishavunja mara moja, ni rahisi kuvunja tena na tena.
Hayo tuliyojifunza ni kwa upande binafsi ambapo unapanga na kutekeleza kama ulivyopanga bila kuruhusu sababu zozote kwenda kinyume na mipango yako.
Inapokuja kwenye upande wa kushirikiana na wengine, utaratibu ni huo huo.
Chora mstari ambao hakuna mtu anaruhusiwa kuuvuka.
Unapaswa kuweka mipaka ambayo hakuna yetote anayeruhusiwa kuivunja.
Hapo hutafanya mambo kwa kuruhusu mtu yetote kuvuka mipaka uliyojiwekea.
Watu huwa wana tabia ya kujaribu kuvuka mipaka uliyoweka ili kuona utachukuliaje hilo.
Hivyo kama hujaweka mipaka imara na kuweka madhara pale mtu anaposhindwa kuizingatia, fujo zinakuwa nyingi sana.
Hakuna chochote kikubwa kitakachoweza kufanyika kwa kila mtu kujiamulia vile anavyotaka yeye mwenyewe.
Ukiwaruhusu watu kuvuka mipaka uliyoweka, hata kama ni kidogo tu, wataenda zaidi ya ulivyowaruhusu.
Na hapo unakuwa huna tena ujasiri wa kuwazuia kwa sababu umeshakubali kuvunja kile ulichoweka wewe mwenyewe.
Hapa tena kusimamia kitu kwa asilimia 100 ni rahisi kuliko kusimamia kwa asilimia 99.
Inakuwa na nguvu sana pale unapokuwa kwenye mwendo wa ufanyaji ambao hujavunja vile ulivyopanga.
Kuendeleza msimamo ni rahisi, kwa sababu unatunza sifa ambayo tayari unayo.
Lakini ukishavunja hata mara moja tu, unavunja sifa uliyokuwa umeshajenga kwa msimamo uliokuwa nao.
Baada ya kuvunja sifa na msimamo, mambo yanaanza kwenda hovyo kuliko ilivyokuwa awali.
Mara ya pili kufanya kitu huwa inakuwa rahisi kuliko mara ya kwanza.
Hivyo kama kuna vitu ambavyo hutaku kufanya, hakikisha unajenga sifa imara ya kutokuwahi kufanya vitu hivyo.
Hakikisha hujawahi kufanya kabisa na simamia kuendeleza sifa hiyo bila kuivunja.
Tekeleza yote uliyopanga kwa namna ulivyopanga bila kuruhusu sababu zozote ziingilie.
Tekeleza yale yote uliyowaahidi wengine bila ya kuruhusu sababu zozote zikufanye uvunje ahadi hizo.
Hata kama itakuingia gharama kubwa kukamilisha kama ulivyopanga au kuahidi, fanya tu hivyo kwa sababu ya sifa unayotaka kuendelea kujenga na kulinda.
Usiwe rahisi kuvunja mambo yako uliyopanga au kuahidi wewe mwenyewe.
Usiwaruhusu watu kuvuka mipaka ambayo umewawekea.
Jenga msimamo mkali kwenye maisha yako yote na yale unayofanya na utaweza kufanya makubwa sana.
Ndiyo kwa kusimamia misimamo yako kuna vitu unaweza kukosa, lakini vinakuwa vidogo kuliko unavyokosa kwa kutokusimamia misimamo yako au kwa kutokuwa na msimamo wowote.
Ukishapanga kinachofuata ni utekelezaji, usiruhusu kuvunja hilo kirahisi sana.
Iwe ni wewe binafsi au wengine, hakikisha yote uliyopanga yanaheshimiwa na kutekelezwa bila sababu zozote kuzuia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kweli ukisimamia misimamo kuna vitu utakosa lakini kuna manufaa makubwa zaidi kuliko kuyumba kwenye msimamo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
ahsante
ni rahisi kusimamia kitu kwa asilimia 100 kuliko kwa asilimia 99. nitasimamia mipango yangu kwa asilimia 100 pasipo kuruhusu sababu.
LikeLike
Vizuri na kila la kheri.
LikeLike
Simamia kufanya yale uliyopanga kufanya bila kuvunja taratibu zako na pia bila kuruhusu mtu kuvuka mstaru hata mara moja ulioweka .haijalishi utakosa mengi lakini ni muhimu kufanya yale uliyokusudia maana yana mafanikio makubwa zaidi ya yale ungepata kwa kuruhusu mpaka kuvukwa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitapanga na kutekeleza bila kuruhusu chochote kuingilia mioango niliyoweka
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ninatekeleza yale niliyopanga kufanya bila kuruhusu sababu yoyote inikwamishe
LikeLike
Vizuri, zingatia.
LikeLike
Asante sana kocha,hapa tulipo ni sawa na kuwa kambini, Elimu na Falsafa tunazojifunza zinaweza kurudisha kufanya makubwa.
Muhimu kwangu ni
Kuwa na nidhamu kali ya kuamua na kufanya kwa msimamo bila kuacha au kuangalia wengine wanasemaje maana haya ni maisha yangu.
Asante!!!
LikeLike
Hakika, tukae humo.
LikeLike
Nitaendelea kuwa na msimamo mkali na kuweka mpaka imara kwenye mambo yangu.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Msimamo,
Kupanga kufanya na kufanya kweli
Kutokuvunja mnyororo
Asante sana kocha
LikeLike
Hakika, tufanye kwa msimamo bila kuacha.
LikeLike
Nitajitahidi kufanya kama nilivyopanga kwa asilimia mia. Asante sana kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ukiamua kufanya fanya kwa asilimia 100 . Kujaribu Kuacha hata kwa asilimia 1 ni kupelekea kushindwa kufanya.
LikeLike
Ukiruhusu tu asilimia 1, umekwisha.
LikeLike
Tekeleza yote uliyopanga kwa namna ulivyopanga bila kuruhusu sababu zozote ziingilie.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ukiruhusu kufanya kitu fanya na usiwe na sababu Bali fanya TU
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ukijiruhusu tuu kuacha Mara moja kufanya yale ya msingi umefungulia Bomba la kuacha,
Hakuna kufungulia Bomba la kuacha!
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nimeamua kuweka msimamo kwa siku 120 kufanya saa kwa saa nikisindwa NAJIFUKUKUZA KAZI
LikeLike
Nimesoma msimamo wako, uko vizuri, usimamie bila shaka.
LikeLike
Nimeamua kuweka msimamo kwa siku 120 kufanya saa kwa saa nikisindwa NAJIFUKUKUZA KAZI na hii ni ahadi yangu
LikeLike
Nitasimia mipaka na maneno niliyoahidi yaani nikiahidi kinacho baki nikutekeleza
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nasimamia na kutekeleza yote ninayopanga.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Sitafanya kile ambacho nimeahidi sitafanya hata mara moja.
LikeLike
Nadhani unahitaji kuhariri haya maoni yako.
LikeLike
Usikubali hata kidogo kwenda kinyume ulivyopanga.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nikishapanga kinachofuata ni utekelezaji. Asante sana Kocha.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Lakini ukishavunja kitu mara moja unashawishika kuvunja tena
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kusimamia na kutekeleza mipango yangu yote kwa msimamo bila kuyumbishwa na chochote.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike