3159; Maokoto.
Rafiki yangu mpendwa,
Fedha ndiyo kitu ambacho huenda kina majina mengi ya utani kuliko kitu kingine chochote.
Fikiria majina mbalimbali ya fedha kama mshiko, mapene, ngawira, fuba au shekeli.
Yote hayo ni majina ya fedha yamekuwa yakitumika katika nyakati mbalimbali.
Na kwa wakati wa sasa, jina maarufu la fedha ni maokoto.
Binafsi nimelipenda jina hili kwa sababu lina mtazamo chanya na sahihi kabisa kuhusu fedha.
Watu wengi wamekuwa wanatumia kauli ambazo zinaashiria mtazamo hasi kuhusu fedha na hivyo kujizuia kuzipata kwa wingi.
Mfano mtu anasema nikipata fedha, nita …
Kauli hiyo inaashiria kwamba kuna uwezekano wa kupata au kutokupata.
Na hivyo mtu asipopata ni sawa tu.
Kuita fedha maokoto inaashiria kwamba fedha ni kitu cha kuokota, kwa sababu kimezagaa tu.
Na huo ndiyo ukweli, fedha zimezagaa kila mahali na wale wanaokuwa nazo kwa wingi siyo kwa sababu wana chochote cha tofauti.
Bali ni kwa sababu wanaamua kuziokota.
Watu hao fedha kwao ni kama udogo au mchanga.
Ukikuta mtu ana udogo mwingi, huwezi kumuuliza ameutengenezaje, unajua ameukusanya tu kutoka kwenye ardhi.
Unaona inavyokuwa rahisi kuifikiria fedha, kwa kuipa jina la maokoto, kwa maana kwamba ni kitu unachokusanya tu, maana kimezagaa kila mahali.
Huenda bado unafikiria unaokotaje fedha, basi tuendelee kurahisisha zaidi.
Njia pekee ya kupata fedha (maokoto) ni kupitia mauzo. (Najua zipo njia nyingine kama za wizi, tushwa, ulaghai, urithi, kushinda bahati nasibu n.k. Lakini unajua mwisho wa njia hizo, hivyo hatuzihesabii kama njia).
Lazima uwauzie watu kitu ndiyo wawe tayari kukupa fedha walizonazo.
Kwa maana hiyo basi, unaokota au kukusanya fedha kupitia mauzo.
Kwenye kuokota fedha kwa mauzo kuna vipengeke vinne, ambapo fedha ndiyo kipengele cha nne, ambacho ni matokeo zaidi.
Vipengele vingine ni kama ifuatavyo.
Cha kwanza ni kuwa na kitu chenye thamani ambacho watu wengine wanakihitaji sana.
Lazima uwe na kitu cha thamani unachouza, ambacho wengine wanataka sana kuwa nacho.
Hitaji hilo la wengine ndiyo linawafanya wawe tayari kukupa fedha ili wapate thamani unayouza.
Cha pili ni watu wa kuwauzia thamani uliyonayo. Watu ambao wana uhitaji mkubwa wa thamani hiyo na wanaweza kumudu kulipia ili wawe nayo.
Wengi wanaweza kutaka thamani uliyonayo, lakini kama hawawezi kumudu kulipia, hutaweza kukusanya maokoto.
Na hatupo kwenye shughuli ya kuwasaidia wasiojiweza. Bali tupo kwenye biashara ya kubadilishana fedha kwa thamani.
Cha tatu ni kuwashawishi watu hao wakubali kununua thamani uliyonayo. Unaweza kuwa na thamani ambayo watu wanaihitaji na wanaweza kuimudu, lakini wasinunue kama huna ushawishi mzuri kwao.
Na ushawishi kwenye mauzo huwa unaanza kwa urafiki na kuaminika. Hivyo unawajibika kujenga urafiki na kuaminika na wale unaopanga kuwauzia thamani uliyonayo ili wakubali kununua.
Kumbuka njia ya mauzo ya kukusanya maokoto inahusisha watu kukubali wao wenyewe kukupa fedha zao na siyo kuzichukua kwa nguvu.
Vitu hivyo vitatu vikija pamoja ndiyo vinazalisha kitu cha nne ambacho ni maokoto.
Wengi wanakwama kukusanya maokoto kwa sababu wanaanzia mwisho badala ya kuanzia mwanzo.
Ni lazima upande kabla hujavuna.
Mahali pa wewe kukusanya maokoto.
Biashara uliyonayo sasa ndiyo mahali sahihi kwako kukusanya maokoto mengi kadiri unavyotaka.
Unachohitaji kufanya ni kuongeza thamani ya kile unachouza, kuwafikia wengi zaidi (usakaji), kuwashawishi kununua (ukamilishaji) na kuwapa huduma bora sana ambazo hawawezi kuzipata mahali pengine (uhudumiaji).
Biashara yoyote inayofanyia kazi maeneo hayo matatu kwa fokasi kubwa, kwa msimamo bila kuacha na kwa muda mrefu, lazima itakusanya maokoto mengi.
Lakini pia siyo njia rahisi, ina vikwazo na changamoto za kila aina. Hivyo lazima mtu ajitoe kisawasawa na kamwe kutokukata tamaa na kuishia njiani.
Umakini mkubwa unahitajika, maokoto huwa yana wivu, yakiona huyapi umakini yanakukimbia.
Unayapa maokoto umakini kwa kuzijua namba zako na kuzifuatilia kwa umakini mara zote.
Usilete uzembe, uvivu au mazoea kwenye kufuatilia maokoto yako.
Jua kila namba kila wakati ili uweze kuboresha kwa kukuza zaidi.
Vitu vingine unavyoweza kuuza ili kukusanya maokoto.
Moja ni fedha, ukiwa na fedha, unaweza kuzitumia kama nyenzo ya kupata fedha zaidi. Kwa mfano kwa kuziwekeza vizuri fedha, unaweza kuzalisha fedha zaidi.
Mbili ni ujuzi/uzoefu uliojijengea. Pale unapokuwa na vitu vya thamani unavyoweza kufanya ambavyo wengine hawawezi kufanya, watakuwa tayari kukulipa ili uwafanyie au uwafundishe kufanya.
Tatu ni muda. Kama huna fedha wala ujuzi/uzoefu, unakuwa na muda mwingi. Unaweza kuuza muda huo kwa wengine wenye uhitaji nao na katika kufanya hilo ukajenga ujuzi/uzoefu ambao utaweza kuuza kwa thamani kubwa zaidi na kupata fedha ambazo pia utauza kwa kuwekeza.
Naamini unapata picha hapo jinsi mambo yanavyopaswa kwenda, nenda nayo hivyo.
Muhimu ni maokoto, na popote ulipo, tumia kile ulichonacho kuongeza maokoto zaidi.
Pamoja na kwamba mauzo ndiyo njia bora ya kukusanya maokoto, bado mauzo hayafanani.
Kuna mauzo yana maokoto makubwa na mauzo yenye maokoto madogo.
Mauzo yenye maokoto makubwa ni yale yanayotibu maumivu makubwa ambayo tayari watu wanayo na hawawezi kuyavumilia.
Watu huwa wanachukua hatua haraka sana kuondokana na maumivu wanayokuwa nayo.
Mauzo yenye maokoto madogo ni yale yanayozuia maumivu yasitokee. Kimantiki hayo yalipaswa kuwa mauzo bora, lakini ni kazi ngumu sana kumshawishi mtu kuzuia maumivu ambayo hata hana.
Hivyo wape watu kile wanachokitaka hasa, tibu maumivu yanayowanyima usingizi.
Mwisho kwenye eneo hili la maokoto, ni lazima uwe vizuri sana kwenye majadiliano.
Kwenye maisha hupati kile unachostahili, bali unapata kile unachokipambania.
Kuwa vizuri kwenye majadiliano na mapatano ili kuwashawishi watu wakupe kile unachotaka kutoka kwao.
Hapa tumekumbushana mambo yote muhimu tunayopaswa kuzingatia ili kukusanya maokoto mengi zaidi.
Tuendelee kuyafanyia kazi kwa umakini mkubwa, msimamo na kwa muda mrefu bila kuacha na ushindi utakuwa wetu kwa uhakika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwenye maisha hupati kile unachostahili bali unapata kile unachopambania.
Ni kuwa vizuri kwenye majadiliano na mapatano ili kuwashawishi wakupe kile unachotaka kutoka kwao.
LikeLike
Hakuna mbadala.
LikeLike
ahsante
majina mengine (chapaa,doo,mkwanja)
– model ni ( bidhaa – wateja- ushawishi(ufatiliaji) – maokoto)
– hapo kwenye ushawishi ndio panahitaji jitihada zaidi – maana hapo ndo tunamtenganisha mtu na maokoto yake kuwa yetu.
LikeLike
Hakika, tukae humo.
LikeLike
Pesa ni maokoto,neno zuri sana. Unaokota kile ulichopanda. Hivyo ni muhimu kupanda Kwa wingi Ili maokoto nayo yawe mengi zaidi
Asante sana kocha.
LikeLike
Umeongeza vyema, tupande kwa wingi ili kuokota kwa wingi pia.
LikeLike
Umakini mkubwa unahitajika, maokoto huwa yana wivu, yakiona huyapi umakini yanakukimbia.
Unayapa maokoto umakini kwa kuzijua namba zako na kuzifuatilia kwa umakini mara zote.
Usilete uzembe, uvivu au mazoea kwenye kufuatilia maokoto yako.
Jua kila namba kila wakati ili uweze kuboresha kwa kukuza zaidi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Umakini mkubwa unahitajika, maokoto huwa yana wivu, yakiona huyapi umakini yanakukimbia.
Unayapa maokoto umakini kwa kuzijua namba zako na kuzifuatilia kwa umakini mara zote.
Usilete uzembe, uvivu au mazoea kwenye kufuatilia maokoto yako.
Jua kila namba kila wakati ili uweze kuboresha kwa kukuza zaid
LikeLike
Kazi nzuri sana Kocha Dr Makirita Amani. Asante sana juu ya maokoto
LikeLike
Asante na karibu sana.
LikeLike
Maokoto,fanya kila kinachowezekana kuhakikisha maokoto yanapatikana na kuongezeka, kupitia biashara yangu nahitaji kuhakikisha maokoto yanapatikana na kuongezeka.asante.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha,Muhimu ni maokoto,nitajitahidi kutumia kila mbinu na njia ya kujiongezea maokoto zaidi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mauzo ni njia ya kupata maokoto.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
ahsante sana kuhusu dhana ya fedha kuwa maokoto
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nitazingatia mambo yote muhimu ili nikusanye maokoto mengi zaidi kwenye biashara yangu. Asante Kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mwishowe kwenye enjoy hili la maokoto ni lazima uwe vizuri kwenye majadiliano
LikeLike
Hakika
LikeLike
Maokoto. Nitajitahidi kuwa na vitu vya thamani na kuwa na ushawishi kwa watu wenye uwezo wa kununua vitu hivyo vya thamani ili niweze kukusanya maokoto mengi kupitia mauzo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana kocha nitatoa thamani kwa Watu wengi ili niwe na maokoto mengi
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Usipo yapa maokoto muda yanaondoka kwako
Inabidi kuweka kazi ya kutibu maumivu ya watu, Tena maumivu yanayo waumiza vichwa, swala la service kwa wateja wetu ni eneo ambalo hatujaweka nguvu ya kutosha.
Tunakazi kazi ya ku focus hapa maokoto yaje.
LikeLike
Safi sana, fanyeni hivyo.
LikeLike
Maokotoo
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Katika maokoto unamtenganisha mtu na maokoto yake. Hili si rahisi hata kidogo. Njia ni moja tu, kubobobea kwenye MAUZO.
Asante Kocha.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Maokoto
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Vizuri . Unapata maokoto kwa kuwapa watu kile wanacho kitaka j
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kweli ukitoa thamni kubwa utapata maokoto mengi na kuwashinda wale wanaotoa thani ndogo
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nataka nitoe thamani kubwa na kuwa na ushawishi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Kuwa na kitu chenye thamani ambacho wengine wanakihitaji , washawishi kukinunua nahapo utakuwa umetengeza muokoto.
maokoto
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kuna mauzo yana maokoto makubwa na mauzo yenye maokoto madogo.
Mauzo yenye maokoto makubwa ni yale yanayotibu maumivu makubwa ambayo tayari watu wanayo na hawawezi kuyavumilia.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kuita fedha MAOKOTO inaashiria kwamba fedha Ni kitu Cha kuokota, kwa sababu kimezagaa tu.
Nitaokota kwa bidii kupitia kuuza
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
popote nilipo, nitatumia kile nilichonacho kuongeza maokoto zaidi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitaepuka sana uzembe, uvivu na mazoea ili niweze kukusanya maokoto ya kutosha.
Asante sana
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Maokoto ndiye mwanamke mrembo kuliko wote na kila siku ana ninyima usingizi mpaka nimpate. Asante sana kocha.
LikeLike
Safi sana, pambana naye.
LikeLike
Hakika pesa zipo zimezagaa ni kuokota tuu
Kuongeza ushawishi kwenye mauzo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike