3217; Nyenzo ya juu kabisa.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuanza biashara na kuikuza ni vitu viwili tofauti kabisa.
Hapo ndipo watu wengi sana wanapokwama kwenye safari zao za kibiashara.
Wengi wanapoanza biashara huwa wanakuwa wapo peke yao na hivyo kila kitu kufanya wao.
Wanapokuwa wanashindwa kufanya kitu, wanaona ni kitu ambacho hakiwezi kufanyika kibiashara.
Wanasahau kwamba uwezo wao binafsi na uwezo wa biashara ni vitu tofauti kabisa.
Uwezo binafsi wa mtu unaweza kuwa na ukomo mbalimbali kulingana na mtazamo ambao mtu anakuwa nao.
Lakini uwezo wa biashara hauwezi kuwa na mwisho kama biashara imeachwa huru ikue.
Hivyo wajibu namba moja wa kila mfanyabiashara ni kuhakikisha vikwazo vyake binafsi haviwi vikwazo vya ukuaji wa biashara yenyewe.
Kuna ngazi tatu za mrejesho pale inapohitajika kufanya kitu cha tofauti kwenye biashara.
Ngazi ya chini kabisa ni “hicho hakiwezekani”.
Kwa sababu mtu anaona hawezi kufanya kitu, basi moja kwa moja anachukulia biashara haiwezi kufanya.
Hiki ndiyo kimekuwa chanzo cha kifo cha biashara nyingi.
Ngazi ya kati ni “kinawezekanaje?”
Hapa mtu anauliza ni kwa namna gani kitu kinaweza kufanyika.
Lakini hapo anakuwa anajiuliza kwake yeye mwenyewe.
Hapa ndipo biashara nyingi zinapodumaa na kushindwa kukua, kwa sababu mmiliki wa biashara anataka kufanya kila kitu yeye peke yake.
Ngazi ya juu ni “nani anaweza kukifanyia kazi?”
Hapa mtu anauliza ni watu gani ambao wanaweza kukifanyia kazi kile kinachohitajika kufanywa.
Hapa ndipo penye ukuaji mkubwa wa biashara na usiokuwa na ukomo.
Kwa sababu biashara haimtegemei mwanzilishi pekee.
Nyenzo ya juu kabisa kwenye biashara huwa ni NANI na siyo nini au vipi.
Unapoweza kuwapata watu wengi sahihi wa kutekeleza yale yote yanayopaswa kutekelezwa kwenye biashara, ukuaji unakuwa wa uhakika.
Watu wanaongeza muda zaidi kwenye biashara, hivyo kadiri watu wanavyokuwa wengi ndivyo kikwazo cha muda kinavyopungua.
Watu pia wanaongeza ujuzi na uzoefu muhimu unaohitajika sana kwenye ukuaji wa biashara.
Kwa sababu hii basi, unapaswa kufanya mabadiliko makubwa ya kimtazamo kwenye biashara.
Hama kutoka kufikiria NINI na VIPI na nenda kwenye kufikiria NANI.
Kwa kila kinachopaswa kufanyika kwenye biashara, usiangalie kwa nini hakiwezekani au wewe huwezi kufanya.
Bali angalia nani anayeweza kukifanya kwa usahihi.
Kwa kuwa watu ndiyo nyenzo ya juu kabisa, unapoweza kuifanyia kazi, unaondoa vikwazo vyote vya ukuaji wa biashara yako.
Weka nguvu zako zote hapo na utaweza kufanya makubwa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitaendelea kujiuliza swali la nani na sio vipi au nini ili kujihakikishia ukuaji mkubwa kabisa kwenye biashara yangu.
LikeLike
Kwa kuwa watu ndio nyenzo ya juu kabisa, unapoweza kuifanyia kazi, unaondoa vikwazo vyote vya ukuaji wa biashara yako.
LikeLike
Kweli kuwa na watu sahihi ni muhimu Sana kwenye ukuaji wa biashara zetu
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala hii nzuri ya nyenzo ya juu kabisa kwenye biashara
LikeLike
Watu ndiyo nyenzo ya juu kabisa. Nani anaweza kulifanyia kazi hili jukumu?
Asante sana
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza watu sahihi wanaiongezea biashara muda hivyo kuifanya ikue.
LikeLike
Asante kocha watu ndiyo nyezo ya juu kabisa, lakini pia kwa upande wangu watu pia ndiyo kikwazo kikuu lakini lisha ya changamoto nitaendelea kulitumia hili la nani anaweza kulifanyia kazi hili jukumu? Jukumu lakini sitaruhusu mfanya kazi ashike kwenye hela zangu kwa upande wa hela lazima mimi mwenyewe nihusike hapo lakini jukumu isiyo husika na kushika hela namugawia mwingine afanye
LikeLike
Asante kocha,Kwenye biashara sio nikate tamaa kwamba siwezi kufanya ila inabidi niangalie nani anaweza kufanya vizuri zaidi ili niweze kupata matokeo bora.
LikeLike
Tafuta watu wenye uwezo wa kufanya hiyo kazi kwa weledi na uaminifu
LikeLike
Kwa kila kinachopaswa kufanyika kwenye biashara, usiangalie kwa nini hakiwezekani au wewe huwezi kufanya.
Bali angalia nani anayeweza kukifanya kwa usahihi.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Watu ni nyenzo ya kupunguza kikwazo cha muda
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kwa kuwa WATU ndio NYENZO ya juu kabisa katika ukuaji wa biashara, nitaifanyia kazi ili kuondoa vikwazo vyote vya ukuaji wa biashara
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante sana mara zote nitajiuliza nani anaweza kufanya hili
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitaweka nyenzo zote na kuijua biashara yangu kwa kina zaidi…
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kuna baadhi ya watu nilikuwa nawafuatilia ktk kufanya kazi zao,kumbe wanawafuata vijana vyuoni na kuja kufanya nao kazi,unakuta kama vyuo vya kilimo na ufagaji nikaendelea kujua watu wazuri wapo ni kuwatafuta
Kwenye mada ya leo, tafuta watu wa kufanya kazi wape majukumu,utafanikiwa tu
LikeLike
Vizuri kwa kufuatilia na kujua watu wazuri wapo na wanapatikana.
LikeLike
Kwakuwa watu ndio nyezo ya juu kabisa, unapoweze kuifanyia kazi unaondoa vikwazo vote vya ukuaji wa biashara yako.
LikeLike
Hakika
LikeLike