3401; Mwendo wa kasi.

Kutoka mezani kwa Kocha,

Rafiki yangu mpendwa,
Jiwe likiwa ardhini, linabaki kuwa jiwe tu, ambalo halina madhara yoyote makubwa.
Lakini jiwe hilo hilo likiwa kwenye mwendo wa kasi, linabadilika.

Jiwe ambalo lipo kwenye mwendo wa kasi haliitwi tena jiwe, bali linaitwa kimondo, sayari au nyota kulingana na kasi yame.
Vimondo vinakuwa na kasi kubwa lakini havipo mbali na dunia, hivyo huishishia kuungua na kuanguka.
Sayari ni kubwa na nje ya nguvu ya mvutano ya dunia.
Nyota ni kubwa zaidi na ikiwa umbali mkubwa sana na kasi yake kuzalisha moto unaozifanya nyota zing’ae.

Matokeo ya maisha yako yanategemea sana kasi ya mwendo wako kwenye yale unayofanya.
Unapokuwa huna kasi kabisa, yaani upo upo tu, unakuwa mtu wa kawaida na hakuna matokeo unayoyapata.
Lakini unapokuwa na kasi kubwa, matokeo unayotoa yanabadilika kabisa na kuwa yenye manufaa kwa watu wenyine.

Kila mara jitathmini matokeo unayozalisha na kasi ya mwendo wako.
Kama huridhishwi na matokeo hayo, anza kwa kuongeza kasi ya mwendo wako.
Anza kufanya mambo yako kwa kasi kubwa zaidi.
Muda wa kufanya vitu upunguze ili vitu vike vile uvifanye kwa muda mfupi zaidi.

Kila unapokuwa umekwama, anza kwa kuangalia kasi ya mwendo wako kwenye yale unayoyafanya.
Unapoongeza kasi ya mwendo, kuna mambo mengi yanayobadilika moja kwa moja na kuzalisha matokeo bora.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr Makirita Amani
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe