Rafiki yangu mpendwa,

Kuna kitu kimoja ambacho kimekuwa kinanishangaza sana inapokuja kwenye mafanikio. Kitu hicho ni ujuaji wa watu na kiasi cha mafanikio wanayokuwa nayo.

Katika kufanya kazi na watu, kupitia mafunzo na ukocha, nimekuwa naona picha hii; wale wanaofanikiwa huwa ndiyo wanajifunza zaidi kuliko ambao hawafanikiwi.

Unakuta kuna watu wawili, mmoja kuna hatua fulani amepiga kwenye mafanikio, wakati mwingine yuko chini sana. Lakini inapokuja kwenye kujifunza, yule aliyepiga hatua fulani anakuwa mnyenyekevu na kujifunza, hata kama vitu tayari anavijua.

Kasheshe ipo kwa yule aliye chini, anakuwa na kiburi, akiona tayari vitu unavyomfundisha anavijua. Haweki umakini kwenye kujifunza na hata akijifunza hachukui hatua.

Hapo ndipo inashangaza, ujuaji wa watu unapokuwa hauendani na mafanikio ambayo wanayo.

Rafiki, leo nina habari njema sana kwako za kukuwezesha kupata msukumo wa kuendelea kujifunza na kufanikiwa iwe unaanzia chini au umeshapiga hatua fulani.

Nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye fursa ya kujifunza kwenye tukio kubwa linalowaleta watu wote wenye kiu ya mafanikio pamoja. Tukio hilo ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024. Maelezo ya tukio hili yako hapo chini.

Karibu Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024.

Semina hii inakwenda kukupa maarifa sahihi ya KUPATA, KUTUNZA na KUZALISHA fedha kwa kutumia nguzo saba unazopaswa kuzijua.

Nguzo hizo saba za kukuwezesha kuwa imara kifedha ni kama ifuatavyo;

1. KIPATO; Kikubwa, Uhakika na Endelevu.

2. AKIBA; Dharura, Malengo na Nidhamu.

3. MATUMIZI; Mahitaji, Matakwa na Anasa.

4. MADENI; Mazuri, Mabaya na Kutokomeza.

5. MATOLEO; Sadaka, Misaada na Kodi.

6. UWEKEZAJI; Masoko, Hatifungani na Mali.

7. ULINZI (BIMA); Afya, Mali na Maisha

Kwenye nguzo hizo saba unakwenda kujifunza kwa vitendo na kutoka na hatua za kwenda kuchukua ili uwe imara kifedha.

Hupaswi kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2024 kama upo makini na fedha zako.

Semina itafanyika Mbezi Garden Hotel DSM tarehe 27/10/2024.

Ada ya kushiriki semina ni Tsh 65,000/= Kama utalipa kabla ya tarehe 01/10/2024 na kuanzia tarehe 01/10/2024 ada ya kushiriki itakuwa Tsh 100,000/=.

Kushiriki piga simu au tuma ujumbe wa kawaida au kwa wasap kwenda namba 0752977175 wenye maneno SEMINA 2024 na utapewa utaratibu mzima na nafasi ya kushiriki.

Karibu rafiki uchukue hatua sasa ili kufanya uwekezaji bora kabisa kwako, utakaoacha alama kubwa kifedha kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani, MD, CFE.

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi