Rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa nimekuwa nakupa taarifa za semina yetu ya KUTENGENEZA MFUMO WA BIASHARA yenye mafanikio makubwa inakwenda kuanza tarehe 04/07/2019. Lakini ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kuwa umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA mpaka kufikia tarehe 01/07/2019.

Watu wengi wameonesha nia ya kushiriki semina hii ambayo ni muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara na mafanikio ya kila mfanyabiashara, kwani inakwenda kukupa wewe uhuru mkubwa sana kwenye biashara unayofanya.

Lakini pamoja na wengi kuwa na nia ya kushiriki, kumekuwa na maswali mbalimbali ambayo yamekuwa kikwazo kwa ambao wangependa kushiriki semina hii.

Kwenye makala hii nakwenda kutoa majibu ya maswali ambayo yamekuwa yanaulizwa sana na wengi kuhusu semina hii na KISIMA CHA MAARIFA kwa ujumla.

small-biz-growth-pic

Karibu usome majibu haya na uweze kupata mwanga na kuchukua hatua sahihi zitakazokuwezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Swali; kwa nini ada ya kujiunga ni kubwa sana?

Jibu; ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kushiriki semina ya MFUMO WA BIASHARA ni tsh laki moja (100,000/=). Ni kweli ada hii ni kubwa ukilinganisha na mategemeo ya wengi. Lakini kumbuka hii ni ada ya mwaka mzima wa kuendelea kupata mafunzo kutoka kwa Kocha Dr Makirita. Hivyo ni sawa na kulipa shilingi elfu 8 kila mwezi, au shilingi elfu 2 kila wiki na ukajifunza kwa mwaka mzima. Kwa kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kuna mafunzo ya kila siku, kila wiki na semina mbili kwa njia ya mtandao kwa mwaka. Lakini pia kuna semina ya kukutana ana kwa ana, pamoja na nafasi ya kuingia kwenye Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambapo unatengeneza mtandao bora wa mafanikio kwako. Ukilinganisha thamani hii kubwa sana utakayoipata ukijiunga na KISIMA CHA MAARIFA, utaona ada hiyo ya kujiunga ilivyo ndogo.

Swali; semina kwa njia ya mtandao inaendeshwaje?

Jibu; semina hii ya KUTENGENEZA MFUMO WA BIASHARA pamoja na nyingine ambazo zitaendelea kutolewa kwenye KISIMA CHA MAARIFA zinafundishwa kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki ukiwa popote duniani na huhitaji kuacha chochote unachofanya. Semina inaendeshwa kwa siku kumi, na kila siku unatumiwa somo moja, ambalo utalisoma kwa kina na kisha kupata nafasi ya kuuliza maswali ili uelewe zaidi. Masomo yanakuwa yameandaliwa kwa njia ambayo inakufanya uelewe kwa urahisi, kunakuwa na mifano lakini pia kwenye kila somo kuna hatua ambayo utapaswa kuchukua ambayo itafanya somo lieleweke zaidi na kuleta matokeo bora kwako. Kwa mfumo huu wa semina, unajifunza mengi na kuwa bora sana.

Swali; je naweza kulipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA kidogo kidogo?

Jibu; hapana, huwezi kulipa ada kidogo kidogo, unapaswa kulipa yote kwa mkupuo, kama ambavyo ukienda kununua nguo au simu dukani unalipa fedha yote. Tulishajaribu njia mbalimbali za ulipaji wa ada kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ikiwa ya kila mwezi, lakini imekuwa ni usumbufu mkubwa kwa wengi. Ila njia ya kulipa ada mara moja inampa mtu uhuru wa kujifunza kwa mwaka mzima, na baada ya hapo ataweza kuchagua kuendelea kuwepo au kuondoka. Zipo nafasi chache sana kwa wale ambao wanaweza kulipa ada kwa awamu mbili, kwa kipindi kisichozidi mwezi. Yaani kama unaweza kulipa elfu 50 sasa na mwezi unaofuata ukamalizia elfu 50 basi kuna nafasi chache za kufanya hivyo. Tuma ujumbe kwa wasap namba 0717396253 ukieleza unataka kulipa nusu na tarehe utakayomalizia inayobaki na utapewa nafasi kama bado ipo.

Swali; sina uwezo wa kulipa ada hiyo kubwa ya KISIMA CHA MAARIFA, nawezaje kunufaika na mafunzo unayotoa?

Jibu; kama bado hujaweza kumudu kulipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA, unajaribu kuruka hatua na hilo sishauri kabisa. Mfumo wa huduma ninazotoa uko hivi.

Mtu ana shida, labda kipato hakitoshelezi, au biashara haikui au hapati mafanikio.

Anaingia kwenye mtandao wa google na kutafuta njia za kuongeza kipato au jinsi ya kukuza biashara au jinsi ya kufanikiwa.

Analetwa kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA, anakutana na makala nyingi zinazohusiana na yale aliyotaka kujua.

Anajifunza na kuyaweka kwenye matendo yale anayojifunza. Anaanza kuona matokeo mazuri kwenye maisha yake, hapo hajalipa hata senti moja, anajifunza bure, anachukua hatua na anaona matokeo mazuri.

Baada ya kuona matokeo mazuri, ikiwepo ongezeko la kipato, anataka kujifunza zaidi, anataka kukutana na Kocha, anataka kupata ushauri wa kina zaidi kutoka kwa Kocha.

Na hapo sasa ndiyo anapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili kujifunza zaidi, ili kuwa karibu na Kocha na ili kupata ushauri na majibu ya maswali aliyonayo.

Hivyo kama bado hujaweza kumudu gharama za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, maana yake bado hujafikia kiwango cha kupata huduma hiyo. Hivyo rudi kwenye AMKA MTANZANIA, soma kila makala iliyopo, fanyia kazi na ndani ya miezi 6 kipato chako kitakuwa kimeongezeka zaidi ya unachopata sasa, na hapo unaweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na safari yako ya mafanikio ikakomaa zaidi.

Swali; hali ya uchumi ni ngumu, ni vigumu kupata ada ya kujiunga.

Jibu; kama unalalamikia hali ngumu ya uchumi basi unapaswa kufanya chochote uwezacho ili upate ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Maana kitu cha kwanza ambacho utajifunza kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni kwamba maisha yako ni jukumu lako, na hupaswi kulalamika au kumlaumu yeyote. Lakini pia utajifunza kwamba kinachowarudisha watu nyuma siyo hali ya uchumi, bali mtazamo ambao watu wanakuwa nao. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA utaacha kabisa kusingizia uchumi, wanasiasa, ndugu, mwajiri na wengineo kama kikwazo cha mafanikio yako. Badala yake utabeba jukumu la mafanikio yako na hivyo kuweza kufanikiwa sana.

Hivyo omba, kopa, uza kitu ulichonacho au vyovyote vile (ila usiibe) ili kupata ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Itakusaidia sana kwenye maisha yako.

Swali; vipi kama nimelipa ada na sijanufaika na mafunzo yanayotolewa?

Jibu; kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba, hutapoteza fedha yako kwa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Mfano kama umejiunga na kisha ukaona mafunzo yanayotolewa hayana manufaa kwako, unaniambia kwamba mafunzo hayajawa na manufaa kwako na unahitaji kurejeshewa fedha yako, na bila ya swali la ziada nakurejeshea ada uliyolipa. Nimejitoa kufanya kazi hii miaka yangu yote, hivyo siangalii kile ninachopata kwanza, bali naangalia nini mtu anapata kwanza. Hivyo unaweza kulipa ada, ukakaa mwaka mzima na mwisho ukaniambia kwa mwaka mzima ambao nimekuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA sijanufaika na lolote, na mimi nitakurejeshea ada uliyolipa, bila ya swali la ziada. Niamini kwenye hilo, na ikitokea unataka kurejeshewa ada yako na ukasumbuliwa nakupa nafasi ya kuchukua hatua zozote na hifadhi maandishi haya kama ushahidi.

Swali; naomba uniunganishe nijaribu kwa wiki moja na kama mafunzo ni mazuri nitalipa ada kamili.

Jibu; ili ufanikiwe kwenye maisha, kuna vitu viwili ambavyo lazima uviwekeze, tena ni vitatu; muda, fedha na umakini wako. Kama hutawekeza vitu hivyo vitatu, hutaweza kupiga hatua. Ukipewa nafasi ya kujifunza bure, unaichukulia poa, unajua bure ipo tu, muda wowote naipata. Ukilipa ili kujifunza, ile ada uliyolipa inakuuma, na hilo litakusukuma kujifunza zaidi. Hivyo naweza kukupa nafasi ya kujiunga bure ujaribu, lakini hilo halitakuwa na msaada kwako wala kwangu. Ninachoshauri lipa ada, kaa kwenye KISIMA CHA MAARIFA kwa mwezi mmoja na kisha pima, je mafunzo yanakusaidia au la. Kama hayakusaidii omba kurejeshewa ada yako na utarejeshewa mara moja.

Swali; kama nia yako ni kuwasaidia watu kweli kama unavyoeleza, kwa nini umeweka ada juu ambayo wale wanaohitaji msaada hawawezi kuimudu?

Jibu; nimekuwa nasema mara zote na huu ndiyo msingi mkuu wa huduma ninazotoa, kwamba lengo langu kuu ni kuwasaidia watu kwanza, kuwapa maarifa sahihi yatakayowawezesha kufanya maamuzi sahihi na kupiga hatua kwenye maisha yao. Na falsafa yangu kuu ya maisha ni hii; unaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako, kama utawasaidia wengi zaidi kupata kile wanachotaka.

Kwenye AMKA MTANZANIA kuna makala zaidi ya elfu mbili, zote hizo ni bure kabisa, hulipi hata senti moja kuzisoma, na ni madini hasa. Nimechambua vitabu zaidi ya 200 sasa, na vyote vipo kwenye AMKA MTANZANIA na unavipata bure. Kila siku kuna masomo yanatumwa kwenye email, bure kabisa. Yote hayo ni kuhakikisha hakuna anayekosa masomo haya kwa sababu uwezo wake uko chini. Lakini sasa mtu atakapohitaji zaidi, basi achangie ili huduma hii iendelee.

Naweka muda na nguvu kubwa sana za maisha yangu kwenye haya ninayofanya. Kwa mfano katika kuandaa semina hii ya KUTENGENEZA MFUMO WA BIASHARA, nimesoma vitabu kumi na moja (11) katika kipindi cha mwezi mmoja ambao nimekuwa naandaa semina hii. Hii ni sawa na vitabu vitatu kila wiki, ina maana kuna vitu vingine vingi siwezi kufanya katika muda huo ninaosoma na kuandaa mafunzo haya. Nastahili kulipwa kwa juhudi hizi, hivyo wale wachache wanaolipia huduma hizi, ndiyo wanawezesha wengi zaidi kupata huduma ninazotoa bure.

Hivyo kazana kufanyia kazi mafunzo ya bure yaliyopo kwenye AMKA MTANZANIA na upige hatua ili uweze kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na uweze kuchangia huduma hizi ziendelee.

Rafiki yangu mpendwa, haya ni majibu ya maswali ambayo watu wengi wamekuwa wanauliza kuhusu KISIMA CHA MAARIFA na semina ya KUTENGENEZA MFUMO WA BIASHARA. Nina imani umepata majibu sahihi na hivyo nikuombe uchukue hatua sahihi.

Hatua ninazotaka uchukue ni moja kati ya hizi mbili;

Moja; fanya lolote uwezalo ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA sasa ili uweze kupiga hatua zaidi.

Mbili; kama imeshindikana kabisa kujiunga sasa, ingia kwenye AMKA MTANZANIA ukiwa na hasira kwelikweli, kila siku chagua kusoma makala 5 na andika chini vitu unavyokwenda kufanyia kazi mara moja na jipe miezi sita ya kukuza zaidi kipato chako. Na ninakuhakikishia, kwa miezi sita, kama utafanyia kazi yale unayojifunza, utaweza kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

IMEBAKI SIKU MOJA ILI KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI SEMINA YA KUTENGENEZA MFUMO WA BIASHARA.

Rafiki, imebaki siku moja pekee kwako wewe kupata nafasi hii ya kushiriki semina hii ambayo ni bora sana kwako. Mwisho wa kulipia ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ni kesho tarehe 01/07/2019. Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, chukua hatua ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA leo hii ili usikose semina hii bora sana kwako kuweza kuendesha biashara inayokupa uhuru mkubwa na mafanikio pia.

Karibu sana kwenye semina hii, semina ambayo itakuwa uwekezaji bora sana kuwahi kufanya kwenye maisha yako.

Maelezo zaidi kuhusu semina, kuanzia muundo wa semina hii, masomo yatakayofundishwa pamoja na jinsi ya kujiunga ili kushiriki yako hapo chini.

MUUNDO TOFAUTI WA SEMINA HII.

Rafiki, kwa semina za nyuma nimekuwa nakupa mafunzo ya semina na hatua za kuchukua. Lakini kwa semina hii kutakuwa na muundo tofauti. Tutakuwa na biashara ya mfano ambayo tutaitumia kutengeneza mfumo kwa kuanzia chini kabisa. Na pia tutakuwa na wamiliki wa mfano wa biashara hiyo, pamoja na wafanyakazi wa mfano kwenye biashara hii.

Kwa muundo hii wa kupata mafunzo kwa mfano, utakuwezesha wewe kubadili mfano huo na kuweka biashara yako na kuweza kunufaika sana.

Mfano tutakaotumia kwenye semina hii ni biashara ya nafaka, yenye wamiliki wawili, wafanyakazi watatu na vibarua wawili.

Tutaona jinsi ambavyo wamiliki wa biashara hiyo wanaweza kutoka kwenye kuendeshwa na biashara na kutegemewa kwa kila kitu mpaka kuiendesha biashara na kuweza kuondoka kwenye biashara huku ikijiendesha yenyewe.

Kwa njia hii ya mfano, utajifunza kwa uhalisia na kuweza kuchukua hatua kwa urahisi kwenye kuiboresha biashara yako.

MTIRIRIKO WA MASOMO YA SEMINA YA KUTENGENEZA MFUMO WA BIASHARA.

Yafuatayo ni masomo ambayo utayapata kwa kushiriki semina hii ya kutengeneza mfumo wa biashara.

UTANGULIZI; UMUHIMU WA MFUMO.

Kwenye utangulizi tutajifunza umuhimu wa mfumo kwenye maisha kwa ujumla na hatimaye kwenye biashara. Hapa utaondoka na picha kwamba bila ya mfumo hakuna maisha. Na kuanzia hapo utaanza kuifikiria biashara yako kwa mfumo.

SOMO LA KWANZA; WEWE SIYO BIASHARA YAKO.

Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanashindwa kujitenga na biashara zao, kwa sababu hawajui kwamba biashara zao siyo wao.

Kwenye somo hili la kwanza utajifunza kwa nini wewe siyo biashara yako, na hapo utaanza kuiangalia biashara yako kama mtu mwingine, badala ya kuiangalia kama sehemu ya wewe.

SOMO LA PILI; CHATI YA UONGOZI KWENYE BIASHARA YAKO.

Hapa tutatengeneza chati yetu ya mfano ya uongozi kwenye biashara yetu ya mfano. Tutatengeneza nafasi muhimu za kufanyia kazi kwenye biashara hiyo na kisha kuwapa watu majukumu kwenye kila nafasi.

Hapa ndipo utakapojifunza jinsi ya kutengeneza chati tako mwenyewe ya uongozi wa biashara yako. Na pia kuwapa watu majukumu ambayo utaweza kuwapima kupitia majukumu hayo.

SOMO LA TATU; MFUMO WA MASOKO NA MAUZO.

Moja ya nafasi muhimu utakazotengeneza kwenye biashara yako ni masoko na mauzo. Hiki kitakuwa kitengo muhimu ambacho kinahitaji kuwa na mfumo wake wa uendeshaji, ambao haukutegemei wewe mmiliki wa biashara.

Tutajifunza mambo muhimu kwenye masoko na mauzo na majukumu ya wale unaowakabidhi kitengo hicho.

SOMO LA NNE; MFUMO WA UENDESHAJI NA UZALISHAJI.

Nafasi nyingine utakayoitengeneza kwenye biashara yako ni uendeshaji au uzalishaji wa bidhaa au huduma zinazotolewa kwenye biashara hiyo. Hiki kinakuwa kitengo kinachojitegemea, hivyo kinakuwa na mtu anayekisimamia.

Hapa utajifunza mambo muhimu kwenye uzalishaji na uendeshaji, pamoja na majukumu na njia za kuwapima wale wanaofanya kazi kwenye kitengo hicho.

SOMO LA TANO; MFUMO WA FEDHA NA USIMAMIZI.

Fedha ni eneo muhimu sana la biashara, wafanyabiashara wengi wamekuwa hawalipi uzito unaostahili. Hivyo kwenye mfumo wako wa biashara utaweka kitengo cha fedha na usimamizi na hapa utaweza kufuatilia kwa ukaribu mzunguko wa fedha kwenye biashara yako.

Pia hapa utakuwa na kitengo cha usimamizi na uendeshaji wa biashara, ambacho kitaiwezesha biashara kukua zaidi.

SOMO LA SITA; JINSI YA KUTUMIA ORODHA KUIMARISHA MFUMO WA BIASHARA.

Sisi binadamu tuna changamoto kubwa mbili inapokuja kwenye kuchukua hatua. Changamoto hizi ni ujinga na kupuuza. Ujinga ni pale ambapo hatujui kitu, na kupuuza ni pale ambapo tunajua kitu lakini hatuchukui hatua sahihi.

Unaweza ukawa unajua vitu vingi sana kuhusu biashara yako, lakini ukawa unavipuuza na hilo likakugharimu wewe na biashara yako.

Sasa kuondokana na hali hii ya kupuuza, utahitaji kutumia orodha ya vitu vinavyopaswa kufanywa kwenye kila eneo la biashara yako. Utatumia orodha hiyo katika kujipima na kuwapima wote wanaofanya kazi kwenye biashara yako.

SOMO LA SABA; JINSI YA KUAJIRI WAFANYAKAZI WATAKAOIWEZESHA BIASHARA YAKO KUKUA.

Ili mfumo wa biashara yako uwe imara na uweze kupata uhuru kamili kutoka kwenye biashara yako, utahitaji kuajiri watu wa kukusaidia.

Na hapo ndipo penye changamoto kubwa, kwa sababu kupata watu sahihi ni kitu kigumu sana.

Kwenye somo hili tutajifunza jinsi unavyoweza kuajiri wafanyakazi watakaoiwezesha biashara yako kukua.

Hili ni somo muhimu sana kwa sababu ukishakosea kuajiri, mfumo mzima uliotengeneza hautaweza kufanya kazi vizuri.

SOMO LA NANE; JINSI YA KUTENGENEZA TIMU BORA KWA MAFANIKIO YA BIASHARA YAKO.

Mafanikio ya biashara yako hayataletwa na mtu mmoja, bali yanatokana na timu.

Hivyo kazi kubwa unapaswa kuiweka kwenye kutengeneza timu bora ya mafanikio kwenye biashara yako.

Hapa unapaswa kuwa na mbinu bora za kiuongozi za kutengeneza timu hiyo. Utajifunza yote kwenye somo hili.

SOMO LA TISA; NAMBA KUMI MUHIMU KWA UKUAJI WA BIASHARA YAKO.

Chochote ambacho hakipimwi hakiwezi kukua. Ili biashara yako ikue lazima iwe inapimwa. Na kama unataka kuwa na uhuru kwenye biashara yako, njia bora ya kuwafuatilia wale wanaofanya kazi kwenye biashara hiyo ni kuwa na namba unazozipima.

Kwenye somo hili tutajifunza namba kumi muhimu za kupima kwenye biashara yako na jinsi unavyopaswa kujipima. Kwa kutumia namba hizi, itakuwa rahisi kwako kufuatilia biashara yako hata kama upo mbali.

SOMO LA KUMI; KUPATA UHURU KAMILI KUTOKA KWENYE BIASHARA YAKO AU KUIUZA.

Hapa sasa utapata uhuru kamili wa biashara yako, na utaweza kuamua kama uiache biashara hiyo ijiendeshe yenyewe huku wewe ukifanya mambo mengine au hata kwenda kuanzisha biashara nyingine.

Na kama utapenda basi utaweza kuiuza biashara hiyo na kupata fedha zaidi.

Kwenye somo hili utajifunza jinsi ya kupata uhuru kamili au kuuza biashara yako.

HITIMISHO; BIASHARA INAYOKUFANYIA KAZI USIKU NA MCHANA.

Tutahitimisha kwa kuwa na biashara ambayo inakufanyia kazi usiku na mchana, ambayo haitegemei tena uwepo wako wala muda wako. Hapo ndiyo unakuwa mjasiriamali kamili anayemiliki biashara na siyo kumilikiwa na biashara.

Rafiki, hayo ndiyo masomo tutakayokwenda kujifunza kwenye semina hii, kama ambavyo umejionea mwenyewe, utaondoka na mambo mengi na mazuri ambayo yatakuwezesha kuikuza sana biashara yako na kununua uhuru wako kutoka kwenye biashara hiyo.

Hii siyo semina ya wewe kukosa kama kweli uko makini na biashara yako. Fanya chochote uwezacho kuhakikisha unapata nafasi ya kushiriki semina hii, kwa sababu ndiyo ukombozi pekee kwako.

Jinsi ya kushiriki semina hii imeelezwa hapo chini.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Rafiki, baada ya kuona changamoto kubwa ambazo wafanyabiashara wengi wanapitia, hasa ya kukosa uhuru licha ya kuwa kwenye biashara. Na baada ya kujifunza na kutafiti kwa kina, nimekuandalia semina nzuri ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki semina hii ukiwa popote duniani, na huhitaji kusafiri au kuacha shughuli zako za kila siku, ni kutenga tu muda ndani ya siku yako wa kufuatilia masomo ya semina.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi, ambapo kila siku utapata somo la jinsi ya kutengeneza mfumo kwenye biashara yako. Masomo haya yatakuwa na mifano halisi ya hatua unazopaswa kuchukua ili biashara yako ijiendeshe kwa mfumo. Pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi zaidi kwenye maeneo ambayo hayajaeleweka.

Semina hii itaanza rasmi tarehe 04/07/2019 mpaka tarehe 14/07/2019, kila siku asubuhi utapata somo la semina na utaweza kuuliza maswali kuhusiana na somo hilo. Masomo yote yatatumwa kwenye kundi la wasap na hivyo utaweza kuyafuatilia kwa urahisi.

Japokuwa semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao, utajifunza kwa kina sana na kuondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kuliko unavyoweza kujifunza kwenye semina ya kuhudhuria ana kwa ana. Kwa sababu semina hii ya mtandaoni inakwenda kwa kina sana kitu ambacho siyo rahisi kukifanya kwenye semina ya siku moja ya ana kwa ana.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA.

Rafiki, ili uweze kushiriki semina hii nzuri sana itakayokupa uhuru kamili wa maisha yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa moja kwa moja kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya programu za mafunzo na ukocha ninayoendesha, ambapo watu wanajifunza na kuhamasika kila siku, kisha kuchukua hatua na maisha yao kuwa bora sana.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ada yako iko hai basi tayari umeshajihakikishia kushiriki semina hii. Wewe jiandae tu, kaa mkao wa kujifunza na utaondoka na nondo za kwenda kuiendesha biashara yako vizuri.

Kama ni mwanachama lakini ada yako inaisha karibuni, lipa ada yako mapema ili usikose nafasi ya kushiriki semina hii. Hakikisha hutoki ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kunufaika zaidi na mafunzo haya na mengine mengi.

Kama wewe siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina hii ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, unapaswa kujiunga na kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Hapa unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima tangu tarehe uliyolipia. Utapata mafunzo ya semina mbili zinazofanyika mtandaoni kwa mwaka, na pia utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kocha wako, tukijifunza kwa kina. Pia tunakwenda kuwa ka Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinakupa jumuiya ya watu ulionao karibu ambao wanapiga hatua kufanikiwa zaidi.

JINSI YA KULIPA ADA.

Ili kulipa ada ya kushiriki semina hii, tuma kwenye namba zifuatazo;

TIGO PESA / AIRTEL MONEY – 0717 396 253 (Jina AMANI MAKIRITA)

M-PESA – 0755 953 887 (Jina AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa wasap  kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA.

MWISHO WA KULIPIA ILI KUSHIRIKI SEMINA.

Rafiki, mwisho wa kulipia ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kupata mafunzo ya semina hii ni tarehe 01/07/2019.

Ili ujihakikishie kushiriki semina hii na kuweza kuikuza biashara yako, lipa ada yako mapema kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.

Ninaamini unapenda sana kupiga hatua na kufanikiwa kwenye biashara yako,

Ninaamini hilo linawezekana kabisa, kwa sababu nimeona wengi wakianzia chini na kupiga hatua zaidi.

Na nina imani kubwa kwenye mafunzo niliyokuandalia, yanakwenda kukupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako, hata kama biashara yako ni ndogo sana.

Karibu sana ushiriki semina hii ya MFUMO WA BIASHARA na utaweza kupiga hatua zaidi. Kumbuka kulipa ada yako kwa wakati, kabla ya tarehe 01/07/2019 ili uweze kunufaika na mafunzo haya yatakayoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Nakusubiri kwa shauku kubwa kwenye semina hii ya MFUMO WA BIASHARA, kwa sababu najua utaondoka na mengi ya kuiwezesha biashara yako kukua zaidi. Usipange kukosa semina hii.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge