Katika kundi la SAA KUMI NA MOJA ALFAJIRI TANZANIA, ambalo ni kundi la watanzania walioamua kuchukua hatua juu ya maisha yao, mtanzania mwenzetu Christopher Kapungu alitushirikisha habari juu ya makosa aliyowahi kufanya maishani mwake. Kuna kitu kikubwa cha kujifunza kutoka kwa mwenzetu huyu, hivyo nimeona ni vyema kuwashirikisha watanzania wengi ili nao wajifunze kitu. Hayo hapo chini ndio maelezo yake mwenyewe.
“Kitu muhimu unapoanza maisha, kuwa makini sana na kila mia unayopata. Iogope pesa unayopata. Usitumie katika mambo yasiyofaa. Kumbuka kama umeanzisha biashara, inaitajika ikue ili uweze kushindana na kumudu kuwahudumia wateja wako watakaokua wanaongezeka. Unapofungua biashara yoyote ile lazima itakua, utakua umefanya vyema kama utakua makini na kuweka akiba zaidi kiliko kutumia unachopata katika mambo ambayo sio ya msingi. Mambo ya msigi hayawezi kukuweka pabaya hata siku moja.
  Mfano ukifungua biashara zinazotumia mashine. Kumbuka baada ya muda mashine hizi zitaanza kukusumbua. Kama utakua hujaweka akiba zaidi na ulikua unatumia pesa yako kwa anasa utashindwa kuwekeza tena na kutengeneza mashine zako.
  Tafadhali, kumbuka sana kuwa makini. Kwa mara ya kwanza miaka minne iliyopita nilianza biashara. Nilikua nafanya vizuri sana. Na nilikua nafanya vizuri sana kwenye mambo yasiyofaa. Lakini hata hivyo kwa kuwa nilikua naingiza pesa nyingi sikuona athari zake mara moja. Nina duka la simu na baadae nikafungua karakana ya useremala, kama nilivoanisha hapo yuu, nilikua ni miongoni mwa wasiokua makini.
  Sasa mambo yamekua magumu kwa kua kiasi kikubwa nilichokua napata nilikitumia katika anasa. Jamani napoona watu wanatapanya pesa zao, natamani kushika kipaza sauti. Jamani mnaobahatika kusoma haya usirudie makosa.
Ilifika wakati mbaya. Nilikata tamaa kabisa nilitaman ardhi ipasuke na inimeze. Ni mwezi tu wa kumi mwa huu 2013, katika pitapita yangu kwenye mtandao ndipo nilipokutana na AMKA MTANZANIA. Ndipo nilipo amka nakuona na matumaini mapya.
  Nina madeni makubwa, sasa natumia kila nachokipata kulipa madeni. Ndipo nijipange upya. Najua nitashinda na nitatimiza ndoto zangu. Kwa kua nimbunifu sana na kikubwa nimeamka upya.
Big up MAKIRITA AMANI.
Najua wataamka wengi. Ukipoteza utapata tena kama ukiamka”.

  Kama na wewe una jambo lolote ambalo unahisi ukiwashirikisha watanzania wenzako litawasaidia tafadhali wasiliana nami ili tuweze kuliweka hapa.

  Karibuni sana na kila la heri katika safari ya mafanikio. Kumbuka mafanikio ni jinsi unavyoianza na kuimaliza siku yako kama ulivyoipanga.

tz