Kama Umeajiriwa Na Siku Moja Ungependa Ujiajiri Mwenyewe Soma Hapa.

Ni ukweli usiopingika kwamba asilimia kubwa ya waajiriwa hawazifurahii kazi zao. Wengi wanafanya kazi hizi kwa kuwa tu zinawaingizia kipato cha kusukuma maisha. Ajira zimekuwa na changamoto kubwa na mishahara imekuwa mbali sana na mahitaji ya msingi. Kwa sababu hii watu wengi wamekuwa wakifikiri njia mbadala ya kujiingizia kipato.

  Wengi wa wanaofikiria njia mbadala wanajikuta wanaiga biashara zinazofanywa na wengine. Kutokana na kuiga wanajikuta mambo yanakuwa magumu kuliko walivyodhani. Ajira inawapa changamoto na biashara ya pembeni nayo inaongeza changamoto kubwa zaidi. Maisha yanazidi kuwa magumu na yanapelekea kupata msongo wa mawazo.

biashara7

  Kama na wewe unafikiria kuingia njia hii au umeshaingia ila umejikuta njia panda na hujui ufanyeje leo nina ushauri mzuri kwako.

  Nataka nikushirikishe biashara ambayo unaweza kuanza kuikuza kidogo kidogo kwa sasa na baadae ikakupa uhuru wa kuweza kuachana na kuajiriwa kabisa. Uzuri wa biashara hii utaweza kuamua ni wapi ufanyie kazi, iwe ni nyumbani, ofisini au hata ufukweni.

Kwa nini biashara hii inakufaa wewe muajiriwa?

Nina uhakika biashara hii inakufaa wewe muajiriwa kwa sababu kuna kitu umeajiriwa kufanya. Kuna kitu unakitoa kwenye taasisi iliyokuajiri ndio maana mwisho wa mwezi wanakupa mshahara, tatizo ni kwamba mshahara wanaokupa ni kidogo sana ukilinganisha na kazi unayowafanyia.

  Sasa nataka utumie kitu hicho kutengeneza biashara ambayo itakupatia kipato kikubwa ambacho hakina kikomo. Hata kama hujui kitu unachotoa ili kupata mshahara bado kuna vitu unapendelea kufanya au una vipaji vya ziada ambavyo kama ukiweza kuvitumia vizuri utatengeneza biashara kubwa sana.

  Biashara ninayokushauri uanze kuitengeneza ni kutoa huduma ya kile unachofanya au unachopendelea kufanya kupitia mtandao wa intaneti. Njia rahisi ya kutoa huduma hiyo ni kwa kufungua blog ambayo utaiendesha kwa bure kabisa.

  Ninaposema ufungue blog simaanishi uwe na blog ya kuanza kuripoti habari au udaku, la hasha. Namaanisha uwe na blog ya kitaaluma ambayo utakuwa ukiandika makala za kuwasaidia watu kulingana na kazi unayofanya au vipaji vyako.

  Kama wewe ni mhasibu unaweza kuandika makala za kuwasaidia watu kuandaa mahesabu yao ya biashara na vitu kama hivyo. Kama wewe ni mchumi unaweza kuandika na kuwashauri watu jinsi ya kuimarisha uchumi wao. Kama wewe ni daktari unaweza kuandika mambo ya afya na jinsi ya kujikinga na magonjwa. Kama wewe ni mwanasheria unaweza kuwa unaandika makala zenye kutoa uelewa wa kisheria kwa wasomaji wako. Kama wewe ni mwalimu unaweza kuwa unaandika kuhusu masomo unayofundisha au hata kuandika kwa ajili ya kushauri wazazi kuhusiana na masomo ya watoto wao. Kama wewe ni mfanya usafi unaweza kuwa unaandika njia mbalimbali za kusafisha nyumba na vitu vingine na kama wewe ni mpishi unaweza kuwa unaandika aina mbalimbali za mapishi na jinsi ya kuyaandaa.

  Kwa chochote kile unachofanya kuna watu wengi sana wangependa kujifunza ila hawajui wafanye nini. Kama ukitoa mafunzo yako kupitia blog watayapata pale watakapokuwa wanatafuta kupitia mtandao. Kama utakuwa na mafundisho mazuri wasomaji wako watawaambia na wengine na baada ya muda unakuwa na wasomaji wengi. Hapa ndipo unapoweza kuanza kufanya biashara na kuikuza zaidi.

  Umeona ilivyo rahisi? Unafungua blog na kuanza kuandika baadae biashara. Ni kweli ni rahisi ila sio kama unavyofikiria, kuna mbinu muhimu unatakiwa kuwa nazo ili uweze kujenga hadhira itakayokuamini kutokana na mambo unayoandika kwenye blog yako. Mbinu hizo nitazifundisha kwenye kitabu JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG

COVER

Sina muda wa kujenga biashara hii.

Najua hiki ndio watu wengi wanafikiria wanapoambiwa kitu kama hiki. Lakini kwa biashara hii huhitaji zaidi ya masaa mawili kwa siku. Unaweza kupata saa moja muda wa asubuhi na kuandika makala ya kupost na kupata saa nyingine moja jioni kujifunza vitu vya kuandika. Kama unakosa saa hii moja niambie ni masaa mangapi unatumia kwenye mtandao na mitandao ya kijamii au unayopoteza kufuatilia mambo ambayo hayana msaada kwenye maisha yako kwa siku.

Katika Kitabu hiki utajifunza vitu vifuatavyo;

1. Utambulisho wa blog na aina mbalimbali za blog.

2. Jinsi ya kutengeneza blog yako mwenyewe.

3. Njia mbalimbali za kutengeneza fedha kupitia blog.

4. Kuweka misingi ya blog yako na kuchagua mtindo wako.

5. Uandishi wa makala zenye mvuto.

6. Kujenga hadhira na kuvutia wasomaji wengi zaidi(email list).

7. Kuunganisha blog na mitandao mingine ya kijamii ili kupata wasomaji wengi zaidi.

8. Kuchagua njia ya kuingiza fedha kutumia blog.

9. Uandishi wa makala za kuuzia bidhaa au huduma na siri iliyoko nyuma ya utafutaji wa masoko.

10. Kutengeneza fedha kusiko na kikomo kupitia blog yako.

11. Kutofautisha blog yako na blog nyingine na jinsi ya kuendelea kuikuza zaidi.

  Kitabu hiki kinapatikana kwa mfumo wa soft copy(PDF) na unaweza kukisoma kwenye kompyuta au simu yenye uwezo. Pia kitabu hiki kina picha nzuri za maelekezo ambazo unaweza kufuata hatua kwa hatua na kipo kwenye lugha rahisi ya kiswahili. Gharama ya kitabu hiki ni shilingi elfu kumi za kitanzania.

  Kupata kitabu hiki tuma fedha(tsh 10,000/=) na email yako kwa mpesa au tigo pesa 0755953887/0717396253 kisha utatumiwa kitabu hiki kwa njia ya email.

   Hii ni nafasi kubwa sana kwako kuweza kutengeneza kipato cha uhakika na kisicho na kikomo. Usikubali kuendelea kuuza muda wako na kulipwa kisicholingana na juhidi zako. Anza kujenga biashara yako kupitia mtandao na baada ya muda utaona mafanikio makubwa.

  Karibu kwenye ukombozi wa maisha yako kiuchumi.

5 thoughts on “Kama Umeajiriwa Na Siku Moja Ungependa Ujiajiri Mwenyewe Soma Hapa.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: