Unapojikuta Kwenye Wakati Mgumu Unafanyaje? Jibu Lipo Hapa.

Msomaji wa makala za Amka Mtanzania, Habari za leo? Matokeo ya Uchaguzi yametoka kama ulivyotaka? hongera sana, ni jambo la kufurahisha kwa kile ulichokitegemea ukakipata kama kilivyo. Na wewe ulitegemea matokeo ya uchaguzi huu yatoke kama ulivyotarajia, ila hayakutoka hivyo? Pole sana. Nakuomba usiendeshwe na hasira kwa kipindi hichi cha mpito kwako.

 
Zipo nyakati ambazo mtu hupita, nyakati hizo zinaweza kuwa nzuri au mbaya. Unapojikuta unapita kwenye wakati wa kufurahi na kucheka, jua kuna wakati wa kulia.
Hizi ni nyakati zinazoendana kwa ukaribu mno, yaani kinyume cha kucheka ni kulia.
Mimi nizungumzie ule wakati mgumu ambao kila mtu hupita. Miongoni mwa nyakati ngumu ambazo husababisha wengi wapoteze mwelekeo wa maisha ni pale mtu anapotarajia jambo fulani katika maisha yake, ikatokea akalikosa hilo jambo.

SOMA; Changamoto za maisha ndio zinafanya tufurahie maisha.
Siku zote za maisha yako, jua kuna mambo mawili, kukosa na kupata. Unapokosa si wakati sahihi sana wa kulaumu sana mtu. Unachotakiwa kufanya ni kuangalia wapi ulikosea, wapi hukuweka Juhudi zako vizuri, wapi ulitegea na kuingiza uzembe. Kumbuka Kuna kujisahau, kuna kuridhika, kuna kujihakikishia asilimia zote, hizi ni hali zinapogeuka ghafla nje na matarajio ya mtu, husababisha mtu apoteze msimamo wake wa kueleweka kwa lile lengo alilolitegemea kulifikia.
Hali hii, ni hali ambayo humpata kila mmoja wetu kwa maeneo tofauti tofauti, kutegemeana na matarajio ya kila mtu. Tunaona kwamba hakuna ambaye anaweza kukwepa hii hali, ina maanisha ni kitu ambacho hakiepukiki kwa akili zetu. Ila inawezekana kupata suluhisho pale unapojikuta umeingia kwenye hali hiyo ngumu.
Ufanye nini sasa ili upate kuvuka eneo hili?
Kubali hilo jambo limeshakutokea, kufanya hivyo tu ni dawa nzuri sana iponyayo akili/fahamu zako.
Utaleta nafuu kubwa sana ya kuondoa mawazo hasi, na huleta mawazo ya mpenyo wa kufikiri kisuluhisho zaidi. Lakini kama hutokubaliana na hali halisi, itakunyima fursa ya kuchukua hatua ya haraka kuokoa hata kile ulichobaki nacho.

Mfano; Una gari, ikatokea likapata ajali, hutakiwi kuchukua muda mwingi wa kuwaza uharibifu uliotokea, unachotakiwa ni kukubali hali halisi. Kisha anza kuangalia uwezekano wa hilo gari kutengenezwa upo, kama lina bima, itakuwa afadhali yako, kama halina, ila lina uwezekano wa kutengenezeka shukuru. Kisha Anza kuwaza upatikanaji wa hiyo pesa, hakuna uwezekano wa hiyo pesa kwa sasa, tuliza akili zako, lihifadhi sehemu salama, endelea na shughuli zako.
Kuna vitu vingi ukiachana na huo mfano wa mtu aliyeharibikiwa na gari lake. Inaweza ikawa kwenye biashara/kazi/ndoa/huduma, kubali kulipokea jambo ili kuokoa ule muda wa kuendelea kushindana nalo wakati unajua kabisa hapa, hata nikiendelea kulalama haitaleta msaada wowote.
SOMA; Ukweli Kuhusu Maisha Ambao Kila Mtu Anapaswa Kuujua.
Elewa kwamba sikufundishi kukubali kitu kinacholeta madhara kwenye maisha yako, bali nafundisha kulipokea jambo, ili upate nafasi ya kukabaliana nalo kwa haraka, kuliko ungepoteza muda wako kupingana nalo, halafu likaendelea kukuletea madhara makubwa.
Kabiliana na ugumu wowote kwenye eneo lolote la maisha yako, kwa kulipokea na kulichuja jambo hilo kama linafaa au halifai kuchukuliwa hatua. Hii ndio silaha nzuri na yenye nguvu ya maangamizi ya haraka, ya kuokoa maisha yako, hutakaa usikie magonjwa yanayosababishwa na msongo wa mawazo, hutakaa usikie fulani kajinyonga kwa kuingia hasara fulani, hutakaa uone unatamani kuchoma mtu kisu, hutakaa uone ukirudi nyuma kwa kikwazo chochote kile, hutakaa uone dunia yote inakucheka wewe, na hutakuwa mtu wa kuabudu matatizo.
Nikushukuru sana kwa kunipa muda wako, naamini umejifunza jambo la kufanyia kazi.
Makala hii imeandikwa na rafiki yako Samson Ernest.
Blog:
www.mtazamowamaisha.blogspot.com
Email: samsonaron0@gmail.com
WhatsApp: 0759808081.

One thought on “Unapojikuta Kwenye Wakati Mgumu Unafanyaje? Jibu Lipo Hapa.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: