Zimebaki Siku Chache Kujiunga Na Semina Ya Utoaji Wa Huduma Bora Kwa Wateja.

Habari rafiki?
Ni imani yangu kubwa ya kwamba unaendelea vyema na unaendelea kuweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya na maisha yako kwa ujumla ili uweze kuwa na maisha bora sana. Hongera sana kwa hili rafiki yangu.
Napenda kuchukua nafasi hii kukukumbusha ya kwamba zimebaki siku chache za kujiunga na semina ya UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA. Hii ni semina itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao, yaani wasap na email ambapo utajifunza mambo yote muhimu kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wale ambao wanategemea kile ambacho unafanya.
Semina hii inamhusu kila mtu ambaye kazi au biashara yake inamhusisha yeye kukutana na watu wengine. Iwe umeajiriwa, umejiajiri au unafanya biashara, kama kwa namna yoyote ile unakutana na watu wengine kwenye shughuli zako, basi unahitaji mbinu bora za kuenda na hao unaokutana nao vizuri. Hii ni kwa sababu kila unayekutana naye kwenye shughuli zako ni mteja wako.
Ujuzi wa kibinadamu (human skills) ni moja ya vitu muhimu sana kwa kila mtu kujua, lakini kwa bahati mbaya hupati nafasi ya kufundishwa moja kwa moja. Hivyo wengi wamekuwa wakijifunza kwa kujaribu na kukosea na hivyo kujikuta wanatumia muda mwingi kujifunza mambo muhimu kwao kuweza kusonga mbele. Wewe unaweza kufupisha muda huu kwa kujifunza kupitia semina hii nzuri sana.
Karibu sana kwenye semina hii ambayo itaanza tarehe 02/05/2016 na itaendeshwa kwa siku kumi. Kila siku utapokea somo moja, utajifunza na kutakuwa na jukumu la kufanyia kazi ili kuweza kutumia somo ulilojifunza. Pia kama utakuwa na swali utaweza kuuliza kuhusu somo husika. Mwisho wa kujiunga na semina hii ni jumamosi tarehe 30/05/2016.
Hii ni semina ambayo hupaswi kuikosa kama kweli lengo lako ni kufikia mafanikio makubwa kupitia kile ambacho unakifanya.
Katika semina hii tutajifunza yafuatayo;
1. Kila mtu anauza, je wewe unauza nini?
2. Nani ni mteja wako?
3. Mahitaji ya msingi ya mteja wako.
4. Jinsi ya kutatua hali ya kutoelewana baina yako na mteja wako.
5. Mfanye mteja kuwa rafiki yako.
6. pokea maoni ya wateja wako.
7. Kitu kimoja unachotakiwa kuzingatia sana na kitakunufaisha wewe na mteja wako.
8. Gharama za huduma mbovu kwa wateja wako.
9. Vaa viatu vya mteja wako.
10. Matumizi ya mtandao na teknolojia katika kuboresha huduma kwa wateja.
Karibu sana ushiriki semina hii ambayo itakupa mbinu bora za kutoa huduma bora kwa wateja wako na hivyo kuendelea kufanikiwa kwenye biashara na kazi yako. Kushiriki semina hii tuma ada ya ushiriki ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) kwenye namba zifuatazo; mpesa 0755 953 887, tigo pesa 0717 396 253 namba zote jina ni Amani Makirita. Baada ya kufanya malipo tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo au tuma ujumbe kwa wasap kwenye namba 0717396253 Ujumbe uwe na majina yako kamili na neno SEMINA YA HUDUMA KWA WATEJA. Pia bonyeza maandishi haya na jaza taarifa zako.
Ni wakati sasa wa kuongeza umakini kwenye biashara na kazi yako ili uweze kufikia mafanikio makubwa zaidi. Karibu tujifunze kwa pamoja.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: