Habari rafiki yangu mpendwa,

Kwa siku za hivi karibuni nimekuwa nakutumia jumbe nyingi kuhusu kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, ili usikose semina muhimu ya ukuaji wa biashara tutakayoiendesha mwezi julai 2018.

Wapo wengi ambao nimeona maarifa haya yanawahusu sana, lakini kama wana wasiwasi hivi.

Wapo ambao kwa sababu wanajifunza mengi sana kupitia AMKA MTANZANIA basi wanaona hakuna kipya wanaweza kujifunza kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ni yale yale tu.

Wapo wengine pia wanapata wasiwasi kwamba kulipa ada ya elfu 50 ili kupata mafunzo tena kwa njia ya mtandao ni kitu kigeni kwao. Labda wamewahi kutapeliwa huko nyuma na sasa wana wasiwasi wa kulipia maarifa, tena kwa kiwango hicho kikubwa cha fedha.

Nimeshakueleza sana rafiki yangu, kila utakachojifunza na hata utayari wangu wa kukurudishia ada uliyolipa, na fedha ya ziada kama utajiunga na usipate manufaa yoyote ndani ya mwaka mmoja.

Lakini bado wapo ambao hawajaamini sana. hivyo nimewaomba wale ambao tayari wameshajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, ambao mwanzoni walikuwa na wasiwasi, lakini baada ya kujiunga wamepata thamani kubwa sana.

Na hapa chini kuna baadhi ya shuhuda nyingi za wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwa maneno yao wenyewe, utakwenda kupata sababu kubwa kwa nini unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA LEO.

Soma shuhuda hizi na chukua hatua, maana tunaelekea mwisho kabisa wa kujiunga ili kuweza kushiriki semina ya ukuaji wa biashara.

Karibu sana kwenye shuhuda;

Mimi nimejiunga na kisima cha maarifa mwaka Jana 2017. Kabla ya hapo Nilikuwa napata email za kocha Makirita Kwa muda mrefu Kwa hiyo ningekuwa nimeshajiunga siku nyingi sana, ila kilichonichelewesha ni suala la kulipia elfu hamsini.

Sio kwamba sikuwa na uwezo wa kulipa, ila nilipuuza Kwa muda mrefu nikiamini ni kupoteza pesa yangu kubwa mno kwakuwa niliamini kuwa hakuna jipya nitakalovuna, kama napata email nakuingia Amka Mtanzania bure na kupata masomo mengi, inatosha uko nitaenda kuibiwa pesa yangu tu.

Sababu iliyonipelekea kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ni Semina ya mwaka Jana. Baada ya kocha kunishawishi na kunikumbusha Mara Kwa Mara kuhusu semina, nikasema ngoja tu nijiunge nikaangalie kuna nini, nikaona kama natoa sadaka ile pesa. Lakini baada ya kujiunga sikujutia ila nilijilaumu Kwanini sikujiunga siku zote,

Ni hatua kubwa niliyopiga hasa katika ukuaji binafsi, nilianzisha biashara nikiwa kisimani na pia nilianzisha blog yangu yakuandika kitu ambacho sikuwahi kuwaza katika Maisha yangu. Japokuwa biashara ilipata Changamoto, ila naamini nitaanzisha nyingine, kwa sababu kupitia kisima nimegundua kuwa hakuna kushindwa ila kuna Kutafuta namna tofauti Za kuliendea jambo.

Elishad Bashiru

Asante Kocha.

Kusema kweli kisima cha maarifa kimenisaidia sana katika yafuatayo;

 1. Kuweza kuwa na mpangilio wa siku.
 2. Kuanza siku na kauli chanya
 3. Kuelewa kwa undani maana ya tahajudi na kuifanya
 4. Kufanya mazoezi walau mara chache kwa juma.
 5. Kusoma vitabu vya hamasa ya maisha na maendeleo. Mimi nilikuwa sisomi vitabu nje ya vitabu vya kiada yaani vya masomo ya darasani. Baada ya hapo basi nimemaliza.
 6. Kuhamasika kuwekeza kwa vitendo. Nimekuwa mwekezaji UTT AMIS yaani mfuko wa umoja, nimewekeza kwenye ardhi, kilimo cha miti kwa sababu ya maarifa ninayoyapata kwenye kisima cha maarifa.
 7. Nimepata marafiki wanamafanikio wenye mtazamo chanya
 8. Nimepunguza sana upenzi wa kusikiliza radio, TV na kusoma sana magazeti
 9. Nimeelewa sana biashara kiuhalisia ingawaje bado sijachukua hatua kubwa lakini ninayo imani, matumaini na hamasa kubwa ya kufanya hivyo.
 10. Nimejifunza namna bora ya kuweka lengo kuu na malengo madogomadogo kwaajili ya kuweka kwenye matendo na kurudia rudia kila mara.
 11. Nimeachana na marafiki wenye mtazamo hasi.

Ahsante kocha na ubarikiwe sana.

Felix MUSHI

Asante sana kocha, Binafsi kabla sijajiunga na kisima cha Maarifa niliweza kukufahamu kupitia kwenye website ya AMKA MTANZANIA, baada ya kusearch kwenye Google na kutaka kujua hatua zipi za watu waliofanikiwa huzitumia ili kifikia mafanikio Makubwa hapo Ndipo nilipo kutana na Amka Mtanzania ikiwa na makala nyingi za kuhamasisha, kujifunza na kuchukua hatua sahihi ili kupata mafanikio na kuboresha maisha kwa ujumla, kusema ukweli mwanzoni sikuwa makini sana katika kuyafanyia kazi Yale niliyokuwa najifunza ingawaje yalikuwa ya muhimu na ya msingi.

Baada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA  kwa kusoma lile tangazo La semina ya Elimu ya Msingi ya fedha hapo ndipo safari yangu ya kuanza kupiga hatua za maendeleo ilipo anzia kwanza nilikuwa sijui lolote kuhusu uwekezaji, ila kupitia semina ile nimeweza kufungua account kwenye taasisi ya uwekezaji UTTAMIS kupitia kwenye mfuko wa Umoja, Kwangu Mimi naweza kusema ni hatua kubwa sana kwa sababu sikuweza kufanya hivyo kabla na pia sikuwa napata mawazo bora ya kiuwekezaji kama niliyoyapata kwenye semina hii.

Ni mengi sana nimejifunza Tangu nimejiunga na kisima cha maarifa na wala sijutii kwa ada ya sh.50,000/=Niliyoitoa ukilinganisha na Maarifa ninayoyapata kila Siku kupitia KISIMA CHA MAARIFA: Mwenyezi Mungu akubariki sana na Aendelee kukujalia Afya Njema Kocha wangu Dk. Amani Makirita Ili niweze kujifunza Mengi zaidi Kutoka kwako.

Datius Deus

Kwanza kabisa kabla ya kujiunga na kisima cha maarifa nilikuwa napata jumbe nyingi sana kutoka kwa kocha Makirita na wala nilikuwa simjui, nikasema huyu naye ni nani anaweza kunifundisha kweli? nilikuwa napuuzia muda mrefu sana sababu nilikuwa tayari nipo kwa kocha mwingine ambaye alikuwa ananipa madini mazito kwa hiyo sikuhangaika na kocha mwingine yoyote. Ila siku moja nikakuta kwenye email yangu kuna tangazo la semina inayosema mafanikio bila malengo ambayo ilifanyika jan 2016 nikasema ngoja nijaribu kulipia nione kuna kitu gani kwa kocha Makirita maana muda mrefu ananitumia jumbe nyingi lakini sichukui hatua .

Mara baada ya kulipia 50000 na kuudhuria hiyo semina niliona kama nimechelewa kujiunga kwenye kisima cha maarifa maana madini ninayopata kwenye kisima hiki hakuna sehemu ninayoweza kupata zaidi, huyu jamaa amejipanga  na zaidi sana nia yake ni kusaidia watu wawe na mafanikio na kama anavyosema mwenyewe akimnukuu zig zigler falsafa yake inayosema “ili upate chochote unachotaka duniani ni lazima uwasaidie watu wengi duniani wapate wanachotaka” mwisho wa kunukuu. Na falsafa hii kocha Makirita anaitendea haki ni kweli huyu anajitoa sana kwetu na ana maono makubwa sana na kama kila mtu angejua karama alizonazo kocha Makirita hakuna mtu asingeambatana naye. Mi ni mmojawapo wa watu waliofaidika na masomo yake na mpaka sasa naona ndoto zangu zikianza kutimia kutokana na kuambatana naye.

Ernest Paschal

semina 2017 4
Sehemu ya wahudhuriaji wa semina ya KISIMA CHA MAARIFA iliyofanyika oktoba 2017

Kocha wangu Dr. Makirita. Asante sana kwa ombi hili ulilonitumia.

Kwa kifupi mimi napenda kutoa shukurani zangu kwako kwa huduma hii adhimu unayoitoa kwa wale wote ambao tumebahatia kujiunga na Kisima cha maarifa

Kwa uchache niseme tu kuwa nikubaliane na wewe kwamba nilikuwa mmoja wa wale waliokuwa na wasiwasi juu ya ubora wa maarifa niliyoyatarajia kuyapata hapa ndani kulinganisha na thamani ya fedha niliyotakiwa kulipia.

Hadi sasa nakiri kwa dhati ya moyo wangu kuwa elimu na maarifa niliyoyapata hapa kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu itoshe tu kuwa nimehitimu kozi ya maarifa ya juu ambayo ingenigharimu ada ya masomo ya kiwango cha Diploma ya juu sana.

Aidha thamani ya maarifa niliyopata hailingani na kile ambacho nimetoka kama ada, naamini ile haikuwa ada kwangu bali ilikuwa ni kiingilio (Registration fee) na wala si Ada ya masomo.

Dr. Mimi nimejifunza mengi:-

1.Kukufahamu mtu wa aina kama yako kwangu ni somo na fundisho pia.

2.Maarifa makubwa niliyoyapata katika vitabu vyako kama kile cha Pata masaa mawili ya ziada, Biashara  Ndani ya ajira, Mimi ni mshindi vimenijengea moyo wa kujiamini na kuthubutu

 1. Kujituma katika kazi kupitia nidhamu ya kuamka mapema pamoja na kutekeleza majukumu yangu kwa hatua kila siku nimejikuta nikiwa na mafanikio makubwa sana. Kwa mfano katika kujiongezea kipato nimefanikiwa kuwa mfugaji mzuri wa kuku  wa kienyeji/chotara na kupitia mimi kimeweza kuwahamasisha watu wengine wapatao 8 wameingia katika tasnia hii ya ufugaji kuku na wanafanya vizuri sana chini ya maongozi na mashirikiano kutoka kwangu.
 2. Kupitia Hamasa za kila siku nimeweza kufanya adjustment ya mfumo wa maisha yangu kwani hata pale ambapo nimejikuta nataka kushindwa au kukata tamaa inakuwa kinyume chake kwa kuwa ndiyo kwanza napata nguvu mpya ya kusonga mbele.

Hakika ni mengi Dr. Ila kwa kuwa mimi si mzuri sana katika kuandika, itoshe tu kusema ninaomba wale ambao wana hofu juu ya thamani ya maarifa yapatikanayo humu ndani  kulinganisha na mchango wao au kiingilio wanachokitoa, wasihofu hapa ni mahali sahihi kwa wakati tulionao.

Nakushukuru sana Dr. Makirita

Naitwa Ahamadi Selemani Lalikila.

 

Kocha Amani Makirita,

Kocha Amani Makirita kupitia mtandao wako wa KISIMA CHA MAARIFA umebadilisha maisha yangu kwa kiwango kikubwa sana. Gharama ya shilingi 50,000/= ya  kujiunga hapa ni sawa na bure kabisa ukilinganisha na faida lukuki nilizozipata tangu nijiunge hapa. Shilingi 50,00/= ni sawa na shilingi 4100/= kwa mwezi, au shilingi 138.8/= kwa siku. Hiki ni kiwango ambacho hata mwanafunzi wa shule ya msingi anakimudu, cha muhimu ni kuamua. Faida na maarifa niliyoyapata hapa kwa kweli tulipaswa tulipe zaidi ya hapa. Kabla sijajiunga na KISIMA CHA MAARIFA nilikuwa na maswali mengi ambayo sikuwa na majibu yake. Hivi sasa sio tu nimeboresha maisha yangu kiuchumi, kikazi, kiafya, kimahusiano na hata kiroho lakini sasa nina majibu ya masuala mengi kuhusu nyanja mbalimbali za maisha.

Mara ya kwanza niliposikia kwamba ada ya kujiunga ni shilingi 50,000/=, kwa kweli nilikuwa na mashaka kama kweli nitakachopata kina manufaa yoyote, lakini thamani ya niliyofunza na niliyonufaika nayo ni kubwa mno kulinganisha na shilingi 50,000/=. Hivi sasa sio tu nimejijengea utamaduni wa kusoma vitabu mimi binafsi na familia yangu, bali pia nina miswada miwili ya vitabu nimeshaiandika ambayo muda wowote nitatoa vitabu, yaani nimekuwa sio tu msomaji wa vitabu bali ni mwandishi pia. Nimeweza kuanzisha tovuti/blog yangu binafsi ninayojivunia sana, kitu ambacho nilidhani hakiwezekani. Nina uwezo wa kuwashauri na kuwasaidia wengi kuhusu masuala mbalimbali ya maisha, yote haya yasingewezekana bila kuwepo KISIMA CHA MAARIFA.

Asante sana Kocha wangu

Hamisi Msumi

 

Asante kocha kwa nafasi hii pia. Nipende tu kukufahamisha mimi ni mmoja kati ya wachache ambao hawajawahi kuwa na wasiwasi kabisa na faida za kujiunga na kisima cha maarifa.

Kabla ya kujiunga na kisima cha maarifa nilikuwa napokea email kutoka katika mtandao wa Amka Mtanzania na kwa wakati huo niliona maarifa yanayopatikana katika Amka Mtanzania yananitosha kabisa. nakumbuka nilikutana na wewe ofisini kwako pindi nilipokuja kununua audio books na hapo ndipo uliponifafanulia zaidi juu ya kisima cha maarifa na faida zake. Wakati wengine hofu yao ilikuwa hela mimi hofu yangu ilikuwa muda kwakuwa nilijua kabisa kuwa kwenye group la wasap kunakuwa na chating nyingi na mimi huwa sipendi kuzima data kutokana na nature ya kazi yangu so huwa najitahidi sana kutokuwepo kwenye magroup ya wasap. Lakini niliamua kujiunga na kisima cha maarifa kwakuwa nilikuwa sina mashaka na wewe kwani licha tu ya uwezo wangu wa kuchuja kitu kizuri na kibaya nilikuwa nakufahamu tangu ukiwa sekondari so sikuwa na shaka yoyote na hela yangu.

Nimepata manufaa mengi sana kuwa ndani ya kisima maana pamoja na kwamba mimi naweza kuwa miongoni mwa watu wachache kwenye kisima wenye njia moja tu ya kuingiza kipato kwani nilisimamisha kila kitu nilichokuwa nafanya kwa ajili ya kuja kusoma, maarifa niliyoyapata mpaka sasa juu ya biashara na uwekezaji yatanisaidia sana pindi nitakapoanza upya maana sitafanya yale makosa ya kijinga tena kwenye biashara na uwekezaji.

Raphael Macha

 

Kocha salama?

Nashukuru sana kwa email hii  darasa kubwa sana kwetu mpaka hapa tulipo, maana wakati najiunga kisima cha maarifa nilikuwa nasoma tafakari na kukushukuru mara moja baada ya kusoma. Lakini kwenye kurasa sikufanya hivyo, ndipo nilipokutana  na mambo mawili ulioshirikisha maarifa na kuchukua hatua, mara moja nikajiambia Kocha hata asante zangu bali anataka matokeo, nikaingia kazini Leo hii hati ya nyumba ninayo nyumbani,

-A/a ya mpango inachanja mbuga.

-Biashara ilidumaa sasa nimechoma moto watu wanashangaa.

-nafanya useremala ambao sio kama malabeja alioshikisha kwenye kitabu ninachopenda kusoma sana (Mimi ni mshindi)

-muda sio kama zamani nilivyokuwa natumia wakati sipo wewe, fomu uliotupa kwenye semina Oct inajaa jioni au asubuhi mapema.

-mahusiano yamekuwa bora tofauti na awali. Kwa machache naomba nikushukuru kwa hapa nilipo ni juhudi zako na mungu akupe UBILIONEA na URAIS WA TANZANIA uwakomboe wengi. –

 1. Mwijage.

 

Habari Kocha Dr. Makirita Amani

Naomba nikutumie ushuhuda wangu tafadhali.

USHUHUDA WA JINSI KISIMA CHA MAARIFA KILIVYOBORESHA MAISHA YANGU.

Mimi kwa majina naitwa Emmanuel K. Zabron, kwa taaluma ni Mfamasia. Ni baba wa watoto watatu. Mwezi Desemba mwaka 2016 niliacha kazi kwa hiari kutoka Halmashauri moja hapa nchini nilikokuwa nimeajiriwa kwa takriban miaka kumi. Nilikuwa na hamasa kubwa kuhusu kujiajiri kwani nilidhani muda niliokaa katika ajira ulikuwa umenitosha. Baada ya kuacha kazi nilianzisha na kuendeleza miradi sita ya kijasiriamali sehemu mbali mbali katika mikoa tofauti tofauti.

Nilidhani nina uwezo na uelewa wa kutosha kuisimamia miradi yote hiyo. Hali ilikuja ikawa tofauti na mategemeo yangu. Hadi kufikia mwezi Mei mwaka 2017, nilikuwa nimekwisha pitia changamoto nyingi kubwa na ndogo. Mfano shamba langu la miti ya mbao lililopo Mafinga mkoa wa Iringa lote liliteketea kwa moto. Shamba lilikuwa na ekari ishirini na tano na miti ilikuwa na umri wa miaka minne. Miradi mingine iliyobaki ilikuwa ikijiendesha kwa hasara na sikuweza kumudu kuiokoa hata mmoja. Ni mengi yalitokea lakini kwa kufupisha habari ni kwamba nilipata hasara kubwa sana, nilipoteza kiasi cha zaidi ya shilingi milioni ishirini na moja za kitanzania. Hakika nilikuwa katika wakati mgumu mno.

Siku moja, tarehe za mwishoni mwa mwezi Juni mwaka 2017 nilikutana na makala mbili zilizoandikwa na mwandishi Makirita Amani, moja wapo ilihusu Uwekezaji. Mwandishi alinigusa kwa mengi lakini alinifungua akili zaidi pale alipobainisha kuwa “uwekezaji wa uhakika kwa asilimia mia moja ni kwenye kujiendeleza kielimu na kiujuzi”. Ujumbe huu kwa hakika ulinibadilisha fikra na mtazamo wangu kabisa. Sio hivyo tu, ujumbe huo ulinipa nguvu lakini zaidi sana ulinifikirisha kwamba, kama umri wote niliokuwa nao sikuweza kujua hilo ina maana kuna mengi ambayo siyajui na huenda ndio sababu iliyopelekea nifike kwenye hali mbaya kiuchumi namna ile. Nikapata shauku ya kujua zaidi kutoka kwa mwandishi huyu. Pale pale nikaingiwa na wazo la kujiunga Kisima cha Maarifa. Tatizo likawa kwenye pesa. Nilikuwa sina pesa za kutosha wakati huo. Nikajikusanya kwa nilichokuwa nacho mfukoni, ikapatikana elfu hamsini, nikaituma. Baada ya kutuma pesa nikapata mashaka kidogo kwamba huenda nisipate ninachokitaka. Lakini nikajipa moyo kuwa potelea mbali, nimepoteza mamilioni ya shilingi sembuse hii elfu hamsini, liwalo na liwe. Bahati nzuri nikaunganishwa Kisima cha Maarifa. Mpaka hii leo nipo Kisima cha Maarifa na sitarajii kuondoka kirahisi.

Tangu wakati huo maisha yangu yalibadilika na yanazidi kuwa bora kila kukicha. Kitendo tu cha kujiunga Kisima cha Maarifa kulinirudisha kwenye mwelekeo sahihi wa maisha na kuniondolea machungu yote ya nyuma. Kwa sasa najitambua, najua ninachokitaka, najua ninakokwenda, najua gharama ya vyote ninavyovitaka na naendelea kulipa gharama hizo kwa furaha na amani kwani najua nipo sehemu salama.

Ni faida nyingi ninazipata, nyingi mno, ile elfu hamsini siioni kuwa ni thamani halisi ya ninachokipata kisimani. Baadhi ya faida hizo ni kama ifuatavyo;

 1. Nimefanikiwa kuboresha sana mahusiano yangu na familia yangu, nashangaa sasa hivi nimekuwa si mgomvi kama zamani.
 2. Nimefanikiwa kuanzisha duka la bidhaa za nyumbani ambalo halina muda mrefu ila kwangu mimi ni hatua kubwa nimepiga tayari.
 3. Nimefanikiwa kujijengea tabia ya kuboresha lishe yangu na ya familia yangu kwa ujumla.
 4. Nimefanikiwa kuwa na malengo kumi na manne niliyoyaandika kabisa ambayo nimepanga kuyatimiza  ndani ya    miaka mitano ijayo.
 5. Nimefanikiwa kuwa na tabia ya kupenda sana kusoma vitabu, kwa sasa nimeongeza idadi ya vitabu ninavyosoma kufikia vitabu vitatu hadi vinne kwa mwezi.
 6. Nimefanikiwa kuwa bora sana kwenye suala la kutoa maamuzi hasa kwenye matumizi na usimamizi wa pesa ninazozipata, malezi ya watoto na maisha kwa ujumla.
 7. Nimefanikiwa kuwa na desturi ya kuomba msamaha kwa ninaowakosea na kusamehe kwa wanaonikosea.
 8. Kwa sasa najua hasa nini nataka, nimetulia kuzifanyia kazi fursa mbili tu ninazozipenda, siku za nyuma nilikuwa na tabia ya kukurupukia sana fursa nyingi bila subira wala kufanya tafiti za kutosha.
 9. Nimefanikiwa kujijengea tabia ya kutenga fedha asilimia tano ya kipato changu cha mwezi kwa ajili ya maendeleo yangu binafsi na ununuaji vitabu vya kujisomea.
 10. Nimefanikiwa kuwa na akiba ya fedha za dharura kiasi na zile ninazojilipa mwenyewe kwanza kwa ajili ya uwekezaji zaidi.

11.Nimefanikiwa kujijengea tabia ya kutunza kumbukumbu ya mapato na matumizi, sasa hivi kila pesa ninayopata najua ilipo au ilikokwenda.

12.Nimefanikiwa kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya viungo kwa muda wa nusu saa karibu kila siku asubuhi.

13.Nimefanikiwa kujijengea tabia ya kuamka mapema, saa kumi alfajiri, hii inafanya ratiba zangu ziende vizuri sana.

Naomba nihitimishe kwa kusema, ni bahati sana kuwa ndani ya Kisima cha Maarifa. Mungu anipe nini tena?

Nashukuru sana Kocha Amani Makirita.

Naamini tutafika mbali sana.

Mungu akubariki.

semina 2017 1
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA OKTOBA 2017

Habari rafiki yangu Dr. Makirita, yaani kwa kweli namshukuru sana mungu kwa kunikitanisha na wewe kwani, hapo awali nilijua ni utapeli wa kawaida kama wengine wafanyavyo.

Mara baada ya kusoma meseji zako katika Amka Mtanzania kupitia email, nilipoona matangazo ya semina na kuona ili uhudhurie ni lazima Uwe mwanachama tena wa kulipia kwa kweli nilijishauri sana nikajaribu kushirikisha na wafanyakazi wenzangu wakaniambia “hao wanataka hela tu hamna lolote maisha ni akili yako tu” ile semina ikapita muda wake, nikawa naumia lakini nikiwaza 50000 nasema hapana. Lakini nilipokata shauri la kujiunga niliona nimejichelewesha vingi sana, yaani nimekuwa mtu wa ajabu ni tofauti na yeyote kwenye kundi la watu, haijawahi tokea, sitamani tena kutokuwepo KISIMANI.

Ahsante sana kocha na Mungu akujaalie kheri na afya njema.

Naitwa Amidah Wa Kwimba-Mwanza.

 

Habari za leo mpendwa wangu kocha Dr. Makirita Amani,

Namshukuru Mungu kwa kukutana na wewe kupitia Kisima cha Maarifa.  Kamwe sijutii kuwa katika mtandao huu.

Kabla ya kujiunga na kisima cha maarifa nilikuwa mtu niliyejawa na hofu, kukata  tamaa  na changamoto nyingi za kifedha. Sikujua chochote kuhusu kuweka akiba, kutenga fedha ya dharura na hata kutoa kwa wengine. Nilikuwa mtu asiyejua namna ya kuweka malengo na kisha kuyasimamia.

Maisha yangu yalikuwa magumu huku kipato changu kikiwa kidogo na nisijue namna ya  kukiongeza.

Nilikuwa mtu niliyeamini kuwa ajira ndio sehemu salama ili kupata mafanikio kama ambavyo nilikuwa nimeaminishwa toka nilipokuwa mdogo. Muda mwingi niliutumia kulalamikia wazazi na serikali kuwa ndio wamechangia hali ngumu ya maisha niliyokuwa nayo.

Niliamini kuwa kuna siku labda nitalala masikini na kuamka tajiri na hilo halikuwahi kutokea. Kuna siku rafiki yangu alinishawishi kuwa kuna biashara ya mtandao ambayo unaweka fedha kisha kila siku unakuwa unapokea faida ya 7% ya fedha uliyoiwekeza , nikahamasika na kuweka laki moja. Hapo niliishia kutapeliwa tu.

Nikiwa katika hali hiyo ndiyo nikakutana na kocha Dr. Makirita kwenye mtandao wa Fecebook. alikuwa na Ujumbe unaosema Kama unatumia simu ya Smartphone na hujaweza kuitumia kutengeneza fedha unafanya makosa makubwa sana. Kwa kuwa nilikuwa katika changamoto kubwa za kifedha niliona kama ndo napata suluhisho la matatizo yangu.

Hivyo, niliamua kuchukua mawasiliano yake nikaanza kutafuta. Nilijiunga na mfumo wa email wake ambao ni AMKA MTANZANIA nikaanza kupata mafunzo yake kila siku. Pamoja na kwamba alikuwa akinipatia mafunzo mengi bado nilikuwa na wasiwasi mwingi sana.

Nakumbuka kutuma  email zinazohusu semina ya elimu ya msingi ya Fedha. Hapo nilijikuta njia panda, kwanza nilipenda kushiriki semina ile na pili niliogopa kutapeliwa tena. Maana ilikushiriki semina ile nilitakiwa kulipa ada ya uanachama wa kisima cha maarifa ambayo ni sh. 50,000. Elfu hamsini tu. Kwa hiyo katika hali hii nikasema hata nikiacha kulipa hiyo elfu hamsini bado matatizo yangu ya kifedha hayatakuwa yameisha maana ni kidogo, basi liwalo na liwe nalipa kama nilipa halafu nikatapeliwa basi, na kama itakuwa salama na mimi kupata nafasi hiyo kushiriki semina ile basi nitashukuru kwa hilo. Hapo niliamua kujitoa muhanga kama kupoteza nipoteze tu.

Kweli maamuzi Yale ndiyo maamuzi bora kuwahi kufanya kwenye historia ya maisha. Maana baada ya kujiunga na kuhudhuria semina ile niliweza kuwa mtu wa tofauti kuanzia kiuchumi, kimahusiano na wengine, tabia na mwenendo wangu hata namna ya kufanya kazi vilibadilika. Ndani ya muda mfupi nilipata matokeo makubwa ambayo sijawahi kuyapata Katika maisha yangu.

Sasa ni mwaka umepita tangu nijiunge kwenye kisima cha maarifa lakini mafanikio niliyoyapata siwezi hata kulinganisha hata na hiyo fedha niliyoitoa.

Kwa kupenda Yale niliyojifunza kwa kocha niliweza kulipa ada ya semina ya kuhudhuria ambayo ilifanyika tarehe 28/10/2018 Dar es salaam, nilifurahi kuonana na kocha na wanamafanikio wengine.

Na wiki hii nimelipa kabisa ada yangu ya mwaka wa pili na sina mpango wa kuondoka kwenye kisima cha maarifa. Manufaa ninayoyapata katika kisima cha maarifa ni mengi naweza kuandika hata nisiweze kumaliza yote. Maana hiki ni kisima chenye chemichemi ya Maarifa isiyokauka.

Nashukuru sana kocha kwa Nguvu kubwa unayoweka katika kuhakikisha unatupatia maarifa sahihi yanayotuwezesha kuishi maisha bora kwetu na wengine pia.

Ninaona kufikia ndoto yangu kuwa BILIONAIRE  ifikapo mwaka 2038.

Ni rafiki yako, Tumaini Anthony.

Mwalimu/Mjasiriamali na Mhamasihaji.

 

Naitwa Moses Mahenge,

Kabla ya kujiunga na kisima cha maarifa haya ndio yalikuwa maisha yangu;

 1. Nilikuwa sina utamaduni wa kasoma Vitabu
 2. Nilikuwa na madeni makubwa na Nilikuwa nashangaa kwa nini nakuwa na madeni na nilikuwa sijui nitatoka vipi au kuachana na madeni
 3. Nilikuwa nafikiria kama kuanza biashara ya kufanya basi niwe na kila kitu na nianzie kikubwa na sio kuanza kidogo
 4. Nilikuwa sina msimamo wa lipi nifanye na lipi niache au lipi lianze na lipi lifuate na hii ni kutokana na kila fursa niliyosikia nilitaka kufanya.
 5. Neno kesho nalo nilikuwa nalo sana; nikipata hela nitafanya hili au lile linapoibuka jambo la kutumia hela natumia na kusema lile lengo nitafanya kesho au nikipata tena hela.
 6. Sikujua uwekezaji huanzia na hela ndogondogo.
 7. Sikuwa  na blog japo nilikuwa natamani kuwa na yangu.
 8. Sikuwa na elimu ya fedha au kujua kuwa elimu ya fedha ni tofauti na masomo ya darasani

BAADA YA KUJIUNGA NA KISIMA CHA MAARIFA

 1. Nimeanza kujenga tabia ya kusoma vitatu
 2. Nimefanikiwa kupunguza kabisa madeni lililopo nilikopa na nimefanyia kitu kitakachookoa fedha yangu kwa siku zijazo.
 3. Sasa hv nimepanga kuanza na kidogo kidogo kwa nidhamu ya hali ya juu
 4. Sasa hivi nimeweza kupunguza kabisa mlolongo wa mambo ya kuyafanyia kazi na kama kuanza biashara basi nitaanza na 3 tu kwanza
 5. Nimeanza kuachana na kusema kesho najitahidi kufanya pasipokughairisha
 6. Nimeona umuhimu wa uwekezaji hasa kupitia UTT AMIS
 7. Kupitia kisima cha Maarifa nimeweza kufunga blog www.mtaalamu.net/fumbuamacho
 8. Kwa mara ya kwanza nimepata elimu ya msingi ya fedha na kujua nifanye nini na fedha zangu.

Ahsante, Moses.

 

Dear kocha ,

Naomba nitoe ushuhuda wangu tangu niingie kisima cha maarifa kwa kipindi cha mwaka mmoja nimeweza kufanya mambo ya tofauti na kuongeza thamani kubwa kwa kuweza kuchukua hatua kubwa kila mara nisomapo jambo jipya. Hatua kubwa ambazo nimepata kuwepo kwenye kisima cha maarifa

 1. Nidhamu ,tangu niingie kisima cha maarifa nidhamu katika kuchukua hatua  imeongezeka maradufu jambo kama haliko sawa kuachana na nalo na kufanya jambo zuri
 2. Kuanzisha biashara tangu huko nyuma nilikua na mawazo ya kuanzisha biashara lakini moyo wa uthubutu na kuogopa ulikua ukinizuia kupitia kisima cha maarifa nimeweza kufungua duka na kuajiri mfanyakazi mmoja ambapo kila siku ninazidi kupiga hatua na kulitanua kitu ambacho sikuwahi kukifanya
 3. Kuweka akiba mfululizo kupitia semina ya kocha ya elimu ya fedha nimeweza kuweka kiasi cha kati 5% to 10% ya kipato changu kila mwezi kwa muda wa mwaka mzima sasa ambapo huko nyuma nilijiunga na UTT mwaka 2014 ambapo niliweka na kuacha kabisa na kusahau
 4. Kutoa sadaka na wengine, kabla ya kujiunga kisima cha maarifa ilikua kazi sana kutoa sadaka kwa wengine na kwenye ibada ya kiwango kikubwa sikuwahi hata shs 10000 ya pamoja tangu nimejiunga kisima cha maarifa nimepata kujua umuhimu wa kutoa na kusaidia wengine na wahitaji
 5. Kusoma vitabu ,tangu nimeingia kisima cha maarifa nimepata nguvu ya kusoma vitabu na kuokoa muda mwanzo nilipojiunga kisimani nilianza kusoma vitabu kutumia kompyuta nilikua nakaa siti ya mwisho ya daladala kwa sasa natumia tablet ufanisi umeongezea nasoma minimum vitabu viwili kwa mwezi huko nyuma sikuwahi kufanya hilo
 6. Kusimamia jambo sahihi hata kama watu wanaokunguzuka wakaona  wakafanya kinyume na ww hii ni kutokana na maarifa ya kusimamia jambo

7.Kusali kabla ya kulala na baada ya kuamka kusoma neno la Mungu ni jambo ambalo sikuwahi kulifanya huko nyuma likinishinda sana kwa sasa nimeweza kufanya mwaka mzima mfululilzo.

 1. Kufanya mazoezi na kuamka muda uleule siku zote ,huko nyuma sikuweza kuamka saa kumi na nusu au 11 kwa sasa nimeweza na kuweza kufanya mazoezi ya kuruka kamba kila siku  push na mazoexi ya viungo, Jumamosi na Jumapili kwenda uwanjani kwa kuamka muda uleule wa kwenda kazini

9.Kufanya yote ,huko nyuma nilikua nikipata pesa mfano kwa sasa naendelea  na ujenzi ninapeleka pesa ya yote nikipata dharura inakua tabu kwa sasa nimeweza kuthibiti kwa kufanya mambo kwa hatua na kuweza kubaki na akiba

 1. Kua na kibubu nilikua naona kama kitu hakina maana lakini kupitia kusoma vitabu kitabu kimoja kiliezea matajiri wote wana vibubu ndani tarehe 1,Jan 2018 nimeanza rasmi kuweka akiba pia kwenye kibubu
 2. Kuwashirikisha watu kwenye magroup tofauti ujumbe maarufu kama quotes of the day hii imenipa hamasa kubwa ya kusoma vitabu kila siku ili kupata jumbe mbalimbali za kushare kwa watu badala ya kusharea vitu visivyo na maana whatsapp group ambapo mwanzoni watu wengi walipinga na kudhani nakopi mahali lakinj baada ya kuona nashare mfululizo imenipa hamasa kubwa sana ya kuendelea kujifunza

12.Kurekodi kwenye kitabu matumizi ya kila siku ambapo imenisaidia kuondoa vitu visivyo na maana

Naomba niishie hapo kwa shuhuda ni hatua kubwa sana nimepata kwa kuwepo kisima cha maarifa maarifa ni mengi tunatamani hata kulipia zaidi sijutii kuwa sehemu hii bora zaidi ya maarifa

Asante kocha na kazi njema

Ni mimi  mwanamafanikio Martin Tindwa

 

Habari za jioni..
Ufuatao ni ushuhuda wangu wa mwaka mmoja ndani ya Kisima cha Maarifa..

Nilijiunga na Kisima cha Maarifa mwezi wa saba mwaka 2017, wakati kocha Makirita A. akiitangaza semina ya ELIMU YA MISINGI YA FEDHA.. Wakati huo nilikuwa namfuatilia kocha kupitia blog ya AMKA AMTANZANIA ambayo nilikuwa ninaifahamu tangu 2015..

Nilichelewa kidogo kujiunga nikiamini blogu hii na bei yake ya elfu 50 kwa mwaka ni harakati za mtu kuganga njaa.. Hasa ukizingatia kwamba siku hizi mitandaoni kumekuwa  na utaratibu huo sana wa mtu kutangaza bidhaa kwa juhudi na kukwambia ujiunge kumbe anataka akufanye mteja wa bidhaa zake tu ambazo hazina kiwango bora wala manufaa..
Lakini baada ya kuendelea kujifunza sana kwenye Amka Mtanzania mwisho nikahisi kuna kitu nakosa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ndipo rasmi nikajiunga kwaajili ya semina…

Kwa mwaka huu mmoja nimejifunza vitu vingi mno ambavyo ndani ya miaka karibu 18 ya shuleni sikujifunza kabisa..
Nitayataja baadhi tu ..

MAARIFA KWA UJUMLA
Kama blogu inavyoitwa kisima cha maarifa, hii ni zaidi ya shule, ndani ya mwaka nimejifunza maarifa lukuki kwenye kila kona ya maisha yangu.. Kuanzia maarifa ya kunijenga mimi namna ya kufikiri, kuchukua hatua, kujibadili kuwa vile unataka hadi malezi ya familia.. Kwa kifupi blogu na kundi la wasapu la KCM hakuna kitu kinaacha..
Nimejifunza vingi sana kupitia TAFAKARI, KURASA, BIASHARA LEO, USHAURI N.K
NILICHOJIFUNZA
Maarifa ni muhimu kwa mwenye elimu na asiye na elimu.. Pale unapojiona unajua kila kitu na huna la kujifunza ndipo unapoanza kushuka kuelekea chini..

Binafsi nianza siku yangu kwa ibada fupi, kisha nasoma makala za KCM kisha naanza mazoezi.. Na hayo yote nayafanya kabla ya saa 1 asubuhi.. Kabla sijaingia humu nilikuwa siwezi hata kuamka saa 1 ila saa nimejizoesha tabia za kimafanikio ikiwemo kuwahi kuamka kupitia maarifa haya..

SEMINA
Ukihudhuria semina za KCM, Madara ya Wiki, Tano za Juma nk… Unaweza ukajikuta unaweza ukahisi walezi wako walikosema kwenye kukwambia ukweli wa mambo fulani.. Ni semina zenye mafunzo ya kiwango cha dunia zenye uhalisia na maisha yetu halisi.. Siwezi kusahau mafunzo adhimu kupitia semina za ELIMU YA MISINGIN YA FEDHA (Elimu muhimu ambayo kila binadamu anayejihusisha na masuala ya utafutaji fedha anapaswa kuijua), Semina ya MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO ( elimu ambayo kila anaehitaji kufanikiwa anatakiwa aijue)… Madarasa ya wiki ndio yamejaa mafunzo ya kutosha.. Tano za juma zimesheheni kila kitu na hizi ni kila mwisho wa juma, ama kwa hakika hapa  ni kisimani..
NILICHOJIFUNZA
Kuna mambo mengi sana hatujui kuhusiana na maisha ya mafanikio.. Kuna elimu fulani hatukuwahi kupewa kwenye malezi na hata shuleni.. Ili uweze kuwa na maendeleo endelevu basi elimu hizo ni vyema sana tukazijua..
Binafsi nimebadili sna mitazamo yangu mbalimbali kuhusu fedha na maisha ya mafanikio kupitia elimu hizi za ndani ya KCM..

USOMAJI WA VITABU
Kama unapenda kusoma vitabu ila unashindwa basi kitu pekee cha kufanya ni kuingia ndani ya KCM, utajikuta ushakuwa mteja wa kusoma vitabu tena kwa spidi ya ajabu.. Uzuri mwingine ni kuwa unapata uvhambuzi wa vitabu kutoka kwa wanakisima wengine..
NILICHOJIFUNZA
Kila mtu anaweza kusoma kitabu.. Kwa kutumia fomula ya KURASA KUMI ZA KITABU KWA SIKU basi naweza kusema kusoma kitabu ni rahisi kuliko kuangalia muvi…
Binafsi hadi sasa nishafanikiwa kusoma vitabu zaidi ya 20 kuanzia vile vya kiingereza hafi vya kiswahili na kitu kizuri zaidi ni kwamba ndani ya KCM vitabu (vya soft copy) vinapatikana kirahisi mno.. Hapo mwanzo nilikuwa napenda kusoma vitabu ila sikuwa najua nitavipata wapi..

Hayo ni kwa ufupi tu ila yapo mengi mno…
Jambo pekee la kuhitimisha nalo ni kwamba naweza kusema KCM inatoa tiba ya matatizo yetu ya nyanja zote za kimaisha (kiuchumi, kijamii, kimaisha, kazi, biashara na kila kitu), ambayo mengi yanaanzia kwenye akili, kwa kushindwa kufikiri sawasawa kutokana na uongo mwingi uliojazwa kwenye dunia ili kukufanya kuwa mteja na mtumia huduma za watu, huku ukibakia kuwa ngazi ya kuwapeleka wengine juu na sisi kubakia chini..

Mwisho kabisa niseme asante sana kocha MAKIRITA AMANI, ama kwa hakika Mungu amekuleta duniani kwa kazi maalum..

Mungu Akubariki Kocha..

Felix Rumisha.

 

Habari kocha naitwa Johnbosco Bonephace

Kwa ujumbe huu napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwako kwa kazi zako za kutuelimisha maarifa sahihi KISIMA CHA MAARIFA ,binafsi nimeweza kujua mambo mengi ambayo kwa muda mfupi tangu nimejiunga nimeweza kupiga hatua katika  ulimwengu wa mafanikio na nimeweza kufanikiwa katika mambo yafuatayo

 1. Nimeweza kufanikisha zaidi katika biashara zangu ninazozifanya kwa kuongeza wateja na mauzo

2.elimu kuhusu fedha ,hakika katika upande huu wa sili,  tabia na mienendo ya Ku handle na  ,kumiliki fedha ,uwekezaji na matumizi sahihi ya fedha, kwani baada ya kuwa kisimani cha maarifa akiba yangu imekuwa ikiongezeka kila wakati ,, na katika hili elimu ya msingi wa fedha (basic financial education )baada ya kuipata imekuwa ni msaada makubwa ilinifanya nijiamini sana na changamoto za hasara, kudhulumiwa na imani potofu juu  ya fedha vyote viliisha Mara moja

 1. Nidhamu ya muda nidhamu ya kujisomea vitabu ,nimejikuta nakuwa na majibu ya maswali mengi niliyokuwa najiuliza kuhusu maisha na mafanikio kwa ujumla

4.kupitia tafakari za kila siku darasa LA jumapili na mengine mengi nimejikuta nakuwa na hamasa na kuweza kuchukua hatua za hatari zaidi bila hofu kubwa nimeongeza malengo Mara dufu na makubwa zaidi ya  ambayo nilikuwa nayo kabla na  kwa hatua nilizoanza kuchukua na kwa maarifa zaidi ninayoendelea kupata kisima cha maarifa Nina imani nitayafikia bila wasiwasi  wowote

Ni faida nyingi sana ninazozipata kisima cha maarifa ni maarifa sahihi muhimu MTU kuwa nayo kwa ujumla namushukuru mungu kukufahamu wewe  kocha na kazi zako Nina imani kubwa sana na wewe binafsi maarifa unayotushirikisha kisimani cha maarifa  sijawahi kuona pa kuedit ,sijutii fedha ya ada niliyoitoa  nitakuwa kisimani cha maarifa  maisha yangu yote  kadri mungu  atakavyojalia ,

Wito wangu kwa watanzania wote wanaopenda kufanikiwa kisima cha maarifa ni mahali sahihi mtu kuwepo , ili kuishi maisha ya mafanikio ,

Nakutakia kila LA kheri katika kazi zako za kutushirikisha maarifa sahihi na muhimu sana kwa mafanikio yetu ,mungu akubariki.

Rafiki yangu, hizi ni shuhuda chache kati ya nyingi ambazo wanachama zaidi ya 250 wa KISIMA CHA MAARIFA wanakiri kunufaika sana na huduma hii.

Nichukue nafasi hii kukupa taarifa za semina ya ukuzaji wa biashara ambayo itaanza siku siyo nyingi. Na ili usikose semina hii, jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii.

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha