Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAJUTO YA KESHO…
Kesho ni siku mpya kabisa ambayo hatujui ni kitu gani kitakwenda kutokea.
Lakini sisi wenyewe tumekuwa tunaiharibu kesho yetu kwa kutengeneza majuto kwenye kesho hiyo.
Kila unapoahirisha kitu leo, jua unatengeneza majuto ya kesho.
Kile ulichopanga kufanya leo, halafu ukajiambia utafanya kesho, jua umetengeneza majuto kwa ajili ya kesho hiyo.
Kwa sababu muda utakapofika, yaani hiyo kesho, utajilaumu kwa nini hukufanya jana, na ni rahisi zaidi kusema tena utafanya kesho.
Usiiharibu kesho kabla hata hujaianza,
Fanya leo kile ulichopanga kufanya leo,
Na mengi sana unayoahirisha yanawezekana sana kufanyika leo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukamilisha yale uliyopanga kufanya na kutokuahirisha lolote kwa ajili ya kesho.
#KuahirishaNiMajuto #Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha