Rafiki yangu mpendwa,

Moja ya vitu ambavyo vinawatofautisha wanaofanikiwa sana na wale wanaoshindwa ni maamuzi.

Wale wanaofanikiwa huwa wanafanya maamuzi mara moja na kuyasimamia maamuzi hayo na kuchukua hatua katika kutekeleza maamuzi hayo.

Wale wanaoshindwa huwa hawafanyi maamuzi, badala yake wanaendelea kutathmini wanaendelea kufikiria faida na hasara za kitu. Mpaka wanapofikia kufanya maamuzi wanakuwa wamechelewa sana. Na hata wanapofanya maamuzi, huwa hawachukui hatua kuyasimamia maamuzi hayo.

Kwa kuwa unasoma hapa, najua wewe ni mtu ambaye upo kwenye njia sahihi ya kufanikiwa na hivyo ni mtu wa kufanya maamuzi sahihi na kuyasimamia.

Nakuandikia ujumbe huu kukutaka ufanye maamuzi muhimu sana kwa mafanikio yako makubwa ya baadaye.

Maamuzi hayo ni kuhusu kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018. Hii ni semina ya kukutana ana kwa ana itakayofanyika Dar es Salaam tarehe 03/11/2018.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017

Leo nakuambia ufanye maamuzi iwapo utashiriki semina hii au la. Na kama utashiriki basi unipe taarifa ili niweze kukuandalia nafasi yako ya kushiriki semina hii vizuri.

Ili kudhibitisha kushiriki semina hii, na kujihakikishia nafasi ya kuwepo, tuma ujumbe wenye majina yako pamoja na namba yako ya simu kwenda namba 0717396253. Tuma ujumbe huo sasa hivi rafiki, ili uweze kujiwekea nafasi yako ya kushiriki semina hii ya kipekee sana kwako kwa mwaka huu 2018.

Maelezo zaidi kuhusu semina hii yanapatikana kwenye makala hii, Karibu Kwenye Semina Ya KISIMA CHA MAARIFA 2018; Mafanikio, Biashara Na Uhuru Wa Kifedha. Unaweza kufungua na kusoma, ila kwanza tuma ujumbe kama utashiriki ili maandalizi yaweze kwenda vizuri.

Nichukue nafasi hii kukukaribisha sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, ni imani yangu umefanya maamuzi ya kushiriki semina hii, kwa sababu ni muhimu sana kwako. Tuma ujumbe wenye majina yako na namba yako ya simu kwenda namba 0717396253.

Ni mimi rafiki yako katika kuelekea kwenye mafanikio makubwa sana,

Kocha Dr Makirita Amani.

www.amkamtanzania.com/kocha