Rafiki yangu mpendwa,

Ninayo furaha kubwa sana kukupa taarifa muhimu sana za semina yetu kubwa ya kwenda kuuanza mwaka 2019.

Ni semina ambayo itakuwa na maarifa yatakayoleta ukombozi mkubwa sana kwenye maisha yako.

Kwani semina hii inakwenda kugusa eneo muhimu sana kwenye maisha yako, eneo ambalo linagusa kila sehemu ya maisha yako ukiacha tu hewa unayopumua bure.

Eneo hili ni fedha. Kwa maisha tunayoishi sasa, kila kitu kinagharimu fedha, ukiacha tu hewa ambayo kila mtu anapumua bure. Na hata hewa hiyo inaweza kukugharimu fedha pale unapoumwa.

de6a0-fedha2bkwa2bblog

Fedha ndiyo kitu kinachotufanya tuamke asubuhi hata kama hatutaki kuamka.

Fedha ndiyo kitu kinachotufanya tufanye kazi ambazo hata hatutaki kuzifanya.

Na fedha ndiyo zinazotufanya tuendelee kufanya kazi chini ya watu tusiopenda kufanya nao kazi.

Hii ina maana kwamba, kama unataka uhuru kamili wa maisha yako, lazima kwanza uanze na uhuru wa fedha. Uwe na kiasi kikubwa cha fedha kiasi kwamba hakuna anayeweza kukusumbua kwa jambo lolote lile.

Katika kuuanza mwaka 2019 kwa mafanikio makubwa, nimekuandalia semina inayokwenda kwa jina TABIA ZA KITAJIRI. Katika semina hii, tunakwenda kujifunza tabia kumi ambazo matajiri wote wanazo, na katika tabia hizo kumi, tutakwenda kutengeneza ahadi ambazo tutaziishi kila siku kwenye maisha yetu. Kwa kubadili eneo hili dogo sana la tabia, tutaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yetu.

Kabla hatujaingia kwa kina kwenye semina hii, naomba nikukumbushe namba muhimu sana kwa upande wa fedha na utajiri.

Kwenye nchi yoyote ile duniani, na hata ukichukua dunia nzima, kuna namba za kifedha ambazo zimekuwa zinawashangaza wengi.

Kwa mfano, asilimia moja ya watu wenye utajiri mkubwa, utajiri wao unazidi asilimia 90 ya watu wengine wote.

Pia ni asilimia 5 pekee ya watu ndiyo wanaofikia uhuru wa kifedha, kwa maana kwamba wanaweza kuyaendesha maisha yao vile wanavyotaka. Asilimia nyingine kumi ya watu wanakuwa na maisha ya kati, na wale wanaobaki, asilimia zaidi ya 70 wanakuwa na maisha magumu sana kifedha.

Sasa namba hizi siyo bahati mbaya, na wala siyo bahati kwamba kuna waliopendelewa na wengine kupunjwa.

Nenda kwenye kila nchi, kwenye kila jamii na utakuta kuna wachache wenye utajiri mkubwa na wengi wakiwa hawana uhakika wa maisha ya kesho.

Na hapa ndipo watafiti mbalimbali wa kijamii na kimaendeleo walipotaka kujua nini kinafanya wachache wafanikiwe sana na wengine kushindwa au kuwa kawaida. Je ni umri, rangi, kabila, kiwango cha elimu, aina ya biashara, mazingira au bahati?

Kwenye kila tafiti ambazo zimewahi kufanywa kuhusu watu waliofanikiwa sana kifedha, hakuna sababu hata moja kati ya hizo hapo juu inaonekana kuwa kwa watu wote. Kuna watu wenye umri mdogo wamefanikiwa sana na wengine wenye umri mkubwa wamefanikiwa. Kuna watu wanaofanya biashara kubwa na za maana wamefanikiwa huku wengine wakifanya biashara ndogo na zinazoonekana za hovyo wamefanikiwa pia.

Kitu kimoja ambacho watafiti wamekuwa wanakiona kwa wale waliofanikiwa sana ni tabia ambazo wanazo. Kuna tabia ambazo watu waliifanikiwa sana kifedha wanaziishi kila siku, wakati wale ambao wameshindwa hawaishi tabia hizo. Ni tabia ambazo waliofanikiwa wanazisimamia kila siku kwenye maisha yao, na hizo ndiyo zinawawezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Baada ya mimi kuchukua muda na kupitia tafiti nyingi zinazoonesha tabia zile muhimu zinazowafanya watu wafanikiwe, nimekuchambulia tabia kumi muhimu, ambazo ukizijua na kuziishi kila siku, maisha yako hayatabaki hapo yalipo.

Yaani wala huhitaji kubadili kazi unayofanya au biashara unayofanya ndiyo uwe tajiri. Huhitaji hata kutoka hapo ulipo sasa. Kwa kuendelea hapo ulipo na kufanya unachofanya, unahitaji tu kubadili tabia zako na kuweka muda kisha matokeo yatajitokeza yenyewe.

Rafiki, ndiyo maana ninakuambia nina furaha sana leo kukupa taarifa za semina hii. Kwa sababu nanua ndiyo semina ambayo wengi walikuwa wanaisubiri iwatoe pale walipo sasa na kuweza kupiga hatua.

Kuna tabia kumi tu ambazo hizi ukaziishi kila siku, na ukazisimamia kweli bila ya kuzivunja, muda siyo mrefu milango ya fursa itaanza kufunguka kwako. Utaanza kupata nafasi ambazo hapo awali ulikuwa huzipati. Utaanza kuonekana na watu ambao walikuwa hawakuoni. Na kila mtu ataanza kukuuliza nini unafanya kwenye maisha yako, maana mabadiliko yatakuwa makubwa na yasiyofichika.

Hii ni semina ambayo mtu yeyote aliye hai, na anayejua kusoma na kuandika hapaswi kuikosa. Kwa sababu kuchagua kukosa semina hii, ni kuamua kufa masikini wakati umezungukwa na fursa nyingi za utajiri. Hutakuwa na tofauti na yule ambaye anakufa kwa kiu wakati yuko pembeni ya mto wenye maji safi.

Fursa zote za utajiri unazozifikiria tayari zipo hapo ulipo, unachohitaji ni maarifa sahihi ya kukuwezesha wewe kujijengea tabia sahihi zitakazovutia utajiri kwako.

KARIBU KWENYE SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI.

Rafiki, nachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye semina ya tabia za kitajiri.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo kila mtu anaweza kushiriki popote pale alipo. Huhitaji kusafiri wala kuacha shughuli zako ili kushiriki semina hii. Bali unachohitaji ni kutenga angalau nusu saa tu kwa siku ya kupata mafunzo ya semina hii.

Semina itakuwa ya siku kumi, ambapo kila siku tutajifunza tabia moja kwa kina na tutaweka mikakati ya namna tunavyoweza kuitumia kwenye maisha yetu ya kila siku. Kwa siku hizo kumi, tutaondoka na mkakati wa kufanyia kazi kila siku ya maisha yetu, ambao kwa kuufanyia kazi, maisha yetu yatabadilika sana.

Semina itaanza tarehe 03/01/2019 na kumalizika tarehe 13/01/2019.

NJIA ZA KUSHIRIKI SEMINA HII.

Kuna njia kuu mbili za kushiriki semina ya TABIA ZA KITAJIRI. Na kwa semina hii nimeweka njia mbili kwa sababu sitaki mtu yeyote aikose semina hii kwa sababu yoyote ile. Nataka kila mtu ayapate maarifa haya na kuyatumia kwenye maisha yake ili yaweze kuwa bora.

Njia ya kwanza ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwa wale ambao tayari ni wanachama na ada zao zipo hai, huhitaji kulipa ada ya ziada. Unapata nafasi ya kushiriki semina hii moja kwa moja.

Kwa wale ambao hawajajiunga na KISIMA CHA MAARIFA, basi wanaweza kujiunga na kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja. Kwa kulipa ada hiyo, utashiriki semina tatu zinazoandaliwa kwa mwaka na pia kila siku utakuwa karibu na mimi Kocha wako nikikushirikisha maarifa muhimu ya mafanikio. Tunakuwa karibu na tunajifunza kila siku ili kufanikiwa zaidi.

Njia ya pili ya kushiriki semina ya TABIA ZA KITAJIRI ni kujiunga na kundi maalumu la semina hii. Hili litakuwa kundi maalumu kwa wale ambao hawawezi kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA KWA SASA. Wale ambao kwa hali yao ya kifedha sasa, hawawezi kulipa ada ya shilingi laki moja. Najua hawa wapo wengi na hii itakuwa nafasi yao kuweza kupata maarifa yatakayowawezesha wapate ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwenye njia hii ya pili, unalipa ada ya shilingi elfu ishirini ambayo itakupa nafasi ya kushiriki semina ya TABIA ZA KITAJIRI. Kwa kulipa ada hii, utapata nafasi ya kushiriki semina hii ya siku kumi, na katika siku kumi hizo utajifunza mengi sana kuhusu maisha na mafanikio.

Rafiki, hizo ndiyo njia mbili za wewe kupata nafasi ya kuelekea kwenye utajiri mkubwa. Chagua njia ipi itakufaa kwa pale ulipo sasa, kisha ifanyie kazi.

JINSI YA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI.

Ili kupata nafasi ya kushiriki semina ya TABIA ZA KITAJIRI unahitaji kulipa ada yako kwa njia uliyochagua.

Kama umechagua kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili tuendelee kuwa pamoja kwa mwaka mzima basi unapaswa kulipa tsh laki moja (100,000/=)

Kama umechagua kujiunga na kundi maalumu la semina ya TABIA ZA KITAJIRI basi unapaswa kulipa tsh elfu ishirini (20,000/=) na utapata nafasi ya kuingia kwenye kundi hili.

Namba za kufanya malipo ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI ni MPESA; 0755 953 887, TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma fedha ya ada, tuma ujumbe wenye majina yako kamili kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253, tumia namba hii pekee kwa wasap.

Mwisho wa kulipa ada ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI ni tarehe 02/01/2019. Lakini kama nafasi zitajaa kabla ya hapo, basi hazitapatikana tena.

Hivyo ushauri wangu kwako wewe rafiki yangu, ili ujihakikishie kushiriki semina hii ambayo hupaswi kuikosa, lipa ada yako mapema.

MLIPIE MTU AJIFUNZE TABIA ZA KITAJIRI.

Rafiki, kama una watu wa karibu kwako ambao ungependa waamke na kupiga hatua zaidi kwenye maisha yao, zawadi nzuri sana unayoweza kuwapa kwa mwaka 2019 ni kuwalipia ili washiriki semina hii.

Kama una ndugu zako, watoto wako, rafiki zako, mwenza wako na hata wafanyakazi wako ambao unaona wamekwama mahali au wanakosa maarifa sahihi, nakushauri uwalipie washiriki semina hii. Watajifunza na kuwa tofauti sana.

Kitu kimoja ambacho nakiona kwa wengi wanaojifunza na kupiga hatua ni kwamba wale wanaowazunguka wanabaki nyuma na hivyo wanakuwa mzigo kwao. Sasa usikubali wanaokuzunguka wawe mzigo kwako. Walipie waingie kwenye kundi la semina na kwa siku kumi hawatatoka wakiwa watupu.

Kama kuna mtu unapenda kumlipia mpe taarifa kwamba kuna mafunzo yataendeshwa ya kujijengea TABIA ZA KITAJIRI na wewe unawalipia ili washiriki. Kisha fanya malipo na tuma majina yao ili waweze kupata nafasi.

KARIBU KWENYE KUNDI MAALUMU LA SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI.

Kwa wale watakaoshiriki semina kwa njia ya pili, yaani wale ambao siyo wanachama wa KISIMA CHA MAAARIFA, nimeandaa kundi maalumu ambalo ndiyo litakuwa la semina. Lakini kwa sasa utaweza kujiunga na kundi hili bure ili uendelee kupata taarifa za semina na ukishalipia unajiwekea nafasi za kushiriki semina.

Ili kujiunga na kundi hili maalumu la semina, bonyeza kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/JvJBnoKixGrJZpZdw3shRv na ujiunge na kundi la SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI.

Nichukue nafasi hii kukukaribisha tena rafiki yangu kwenye semina ya TABIA ZA KITAJIRI, hii ni semina yako, ni semina ya kukutoa hapo ulipo na uweze kupiga hatua zaidi.

f8dc1-fedha2bmkopo

Kwa muhtasari; SEMINA; TABIA ZA KITAJIRI.

Semina itatupa maarifa ya kujijengea tabia kumi za kuishi kila siku ambazo zitatuwezesha kufika kwenye utajiri mkubwa.

Semina itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki ukiwa popote.

Semina itaanza tarehe 03/01/2019 mpaka tarehe 13/01/2019.

Kupata nafasi ya kushiriki semina unalipa ada ya KISIMA CHA MAARIFA (tsh 100,000/=) au kama huwezi hiyo unalipia ada ya kushiriki semina tu (tsh 20,000/=)

Namba za kufanya malipo ni 0755 953 887 au 0717 396 253.

Mwisho wa kulipia ni tarehe 02/01/2019 ila nafasi zikijaa kabla hutapata tena nafasi.

Unaweza kumlipia mtu wa karibu kwako akajifunza.

Kujiunga na kundi la semina hii tumia kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/JvJBnoKixGrJZpZdw3shRv  (kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hili).

Karibu sana tupate maarifa sahihi ya kutujenge tabia zitakazotufikisha kwenye utajiri mkubwa.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge