Habari za leo rafiki yangu mpendwa,

Heri ya mwaka mpya 2019, ni nafasi nyingine nzuri tena kwetu kuendelea na safari yetu ya mapambano ya kufikia mafanikio makubwa.

Nasema ni mapambano kwa sababu safari hii siyo rahisi, lakini kwa kujitoa na kuweka juhudi, inawezekana.

Tuanze kwa kila mmoja wetu kutoa shukrani kubwa sana kwa kuona nafasi hii nyingine, siku mpya ya mwezi mpya na kwenye mwaka mpya.

Kwa wale ambao wapo kwenye KISIMA CHA MAARIFA wanajua ya kwamba mwaka mpya huu kwetu ni mpya kikalenda, lakini mwaka mpya wa mafanikio 2018/2019 tulishauanza yangu novemba 2018.

Kwenye makala hii fupi sana ya leo, nakwenda kukuorodheshea vitu 19 ambavyo kama utaweza kuvifanya kila siku kwa mwaka 2019 basi maisha yako yatakuwa bora na ya mafanikio makubwa sana.

2019

Karibu uondoke na vitu hivi 19 na mwisho nitakupa zawadi kubwa sana kwako ya kuuanza mwaka 2019.

  1. Amka asubuhi na mapema sana, angalau masaa mawili kabla ya muda wako wa kuanza kazi.
  2. Unapoamka cha kwanza kufanya shukuru, kwa sala au tahajudi.
  3. Andika malengo yako makubwa kila siku unapoamka, malengo ya mwaka, miaka 5, miaka 10 na hata miaka 50. Lazima uwe na malengo ya aina hii.
  4. Ipangilie siku yako kabla hujaianza, weka vipaumbele vyako kwa siku husika, viwe kati ya 3 mpaka sita. Andika kabisa nini utafanya na kwa muda gani wa siku hiyo.
  5. Soma kitabu au pata maarifa yoyote chanya na ya hamasa kabla hujaianza siku yako. soma angalau kurasa kumi za kitabu kila siku.
  6. Fanya mazoezi ya viungo kabla ya kuianza siku yako, mazoezi bora kabisa ni kukimbia.
  7. Epuka habari au kitu chochote hasi muda wa asubuhi. Usisikilize redio, wala kuangalia tv au kusoma magazeti.
  8. Unapoingia kwenye kazi au biashara yako, fuata vipaumbele ulivyoweka vya kufanya kazi, na unapokamilisha jukumu weka alama ya vema kisha nenda kwenye jukumu jingine.
  9. Fanya jambo moja kwa wakati, usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja, unapoteza nguvu na umakini.
  10. Unapofanya kazi, akili na mawazo yako yote yawe kwenye kile unachofanya, usiwe unafanya kazi huku unafikiria vitu vingine.
  11. Kula kwa afya, punguza sana vyakula vya wanga na sukari, kula matunda na mbogamboga kwa wingi na kunywa maji mengi zaidi, angalau lita tatu kwa siku nzima.
  12. Ondoka kwenye mitandao yote ya kijamii unayotumia kama haikuingizii fedha moja kwa moja. Sheria ya kutumia mitandao ya kijamii iwe hii, iwe inakuingizia fedha moja kwa moja. Kama hakuna fedha inayoingia kupitia mitandao hiyo, achana nayo mara moja.
  13. Acha kabisa kutumia kilevi cha aina yoyote ile, kuanzia pombe, sigara, madawa ya kulevya na hata viburudisho kama kahawa.
  14. Kwenye kila kipato unachoingiza, sehemu ya kumi ya kipato hicho usitumie kwa namna yoyote ile, hicho ni kipato ulichojilipa na utakitumia kwa kuwekeza kwa ajili ya baadaye.
  15. Imarisha sana mahusiano yako na watu wote wa karibu kwako, kuanzia familia yako, ndugu, jamaa na marafiki na pia wale unaohusiana nao kwenye kazi au biashara.
  16. Imalize siku yako kwa kutafakari yale uliyofanya, matokeo uliyopata, makosa au changamoto ulizokutana nazo na namna unavyoweza kufanya kwa ubora zaidi siku inayofuata.
  17. Lala mapema ili uweze kuamka mapema, kama hufanyi kazi za usiku, saa nne inapaswa kukukuta kitandani ukiwa umeshalala.
  18. Tumia neno HAPANA mara nyingi uwezavyo, neno hapana ndiyo litakupa uhuru wako. Kama kitu hakikuwezeshi kufika kule unakotaka kufika, sema hapana bila ya kuona aibu.
  19. JIUNGE NA KISIMA CHA MAARIFA. Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi zawadi kubwa na bora kabisa unayoweza kujipa mwaka 2019 ni kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kama tayari umeshajiunga basi unamjua ndugu, jamaa au rafiki ambaye kwa mambo anayopitia kwenye maisha yake, KISIMA CHA MAARIFA kingemfaa sana, basi mshawishi mtu huyo ajiunge na kama hawezi kulipa ada basi mlipie ada na mwambie ajifunze kwa mwaka mmoja tu, kisha achague kama ataendelea au la. Utakuwa umemsaidia sana mtu huyo kujikomboa kwenye maisha.

Rafiki yangu, hayo ndiyo mambo 19 ambayo nakusihi sana uyafanye kila siku ya maisha yako kwa mwaka huu 2019 na utaweza kupiga hatua kubwa sana. pale ulipo sasa ni kutokana na hatua ulizopiga huko nyuma, na ili uweze kwenda mbele zaidi unahitaji kupiga hatua kubwa zaidi leo.

Nimekuahidi kukupa zawadi kubwa sana ya mwaka mpya 2019, na maelezo ya zawadi hiyo yapo hapo chini;

KARIBU KWENYE SEMINA YA TABIA ZA KITAJIRI.

Nachukua nafasi hii kukukaribisha na kukukumbusha kuhusu semina ya TABIA ZA KITAJIRI.

Kwenye semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI, utajifunza tabia kumi za kuishi kwenye kila siku ya maisha yako ambazo zitakuwezesha kufikia utajiri na mafanikio makubwa.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo unaweza kushiriki ukiwa popote.

Semina hii itaanza tarehe 03/01/2019 na kumalizika tarehe 13/01/2019 zitakuwa siku kumi za kupata nondo kumi za moto ambazo nitaweka msingi muhimu sana wa mafanikio makubwa na utajiri kwenye maisha yako.

Kuna njia mbili za kuweza kushiriki semina hii;

Njia ya kwanza ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, hivyo kama tayari wewe ni mwanachama moja kwa moja unapata nafasi ya kushiriki semina hii. Na kama bado hujawa mwanachama, unaweza kujiunga sasa kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=) na kupata nafasi ya kushiriki semina pamoja na kuendelea kupata mafunzo mengine kwa kipindi cha mwaka mzima.

Njia ya pili ni kujiunga na kundi maalumu la semina hii, hili ni kundi kwa wale ambao siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na kwa sasa hawawezi kulipa ada na kujiunga. Hawa watapata nafasi ya kushiriki semina hii kwa kulipia tsh elfu 20 pekee (20,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kupata mafunzo haya ya semina ya TABIA ZA KITAJIRI.

Ili kufanya malipo ya kushiriki semina, iwe ni kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA au kujiunga na kundi maalumu, lipa ada yako kwa namba zifuatazo; mpesa 0755 953 887 au tigo pesa/ airtel money 0717 396 253. Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukishatuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kwa njia ya wasap namba 0717396253.

Kama kuna zawadi moja unayoweza kujipa kwa mwaka 2019 ambayo miaka mingi ijayo utajishukuru sana, basi ni wewe kushiriki semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI.

Pia unaweza kumlipia mtu wa karibu kwako akaweza kujifunza na kuyabadili kabisa maisha yake kwa mwaka 2019. Mlipie tsh elfu 20 ili aweze kuingia kwenye kundi maalumu la semina hii na ajifunze.

Kamilisha malipo yako leo ili uweze kupata nafasi hii ya kipekee sana ya kupata maarifa sahihi ya kujijengea tabia sahihi zitakazokufikisha kwenye utajiri na mafanikio makubwa.

Rafiki yangu, nakusisitiza tena, usipange kukosa semina hii, nimekupa kila njia ambayo itakuwa rahisi kwako kushiriki semina hii, ni wewe tu kuitumia.

MUHIMU; Imebaki siku moja pekee ya kupata nafasi hii muhimu sana, ili kuepuka usumbufu ambao huwa unajitokeza siku za mwisho, nakushauri uchukue hatua ya kukamilisha malipo leo ili ujihakikishie nafasi ya kushiriki semina hii. Kamilisha malipo yako leo.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge