Rafiki yangu mpendwa,

Napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru sana kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja, tukijifunza na kuchukua hatua ili kuyafanya maisha yetu kuwa bora zaidi.

Tumekuwa tunashirikiana kujifunza kwa njia ya makala mbalimbali ambazo nimekuwa nakushirikisha kila siku. Njia hii inakupa nafasi ya kujifunza na kuchukua hatua.

Lakini ipo njia moja ya kujifunza, ambayo huwa tunapata nafasi ya kuitumia mara moja pekee kwa mwaka. Njia hiyo ni kupitia semina ya kukutana ana kwa ana.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, jamii ambayo ni ya tofauti kabisa na jamii nyingine, tunaongozwa na msingi wa kujifunza na kisha kufanyia kazi yale tunayojifunza ili kupata matokeo ya tofauti kwenye maisha yetu.

Unapofika wakati wa kukutana kwenye mafunzo ya kukutana ana kwa ana, unakuwa wakati mzuri kwetu kujifunza na kushirikishana shuhuda zetu, kwa hatua ambazo kila mmoja wetu amekuwa anapiga.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017
SAMSUNG CAMERA PICTURES
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018
SAMSUNG CAMERA PICTURES
SEMINA YA UZINDUZI WA VITABU 2019

Leo nachukua nafasi hii kukupa taarifa kuhusu fursa hii ya mafunzo ya kukutana ana kwa ana kwa mwaka huu 2019, kupitia semina ya KISIMA CHA MAARIFA.

Tutakuwa na semina ya KISIMA CHA MAARIFA ya mwaka 2019 ambayo itafanyika siku ya jumapili ya tarehe 03/11/2019. Semina ya mwaka huu 2019 itafanyika jijini dar es salaam, eneo kamili itajulishwa baadaye. Itakuwa ni semina ya siku nzima, itakayoanza saa moja kamili asubuhi mpaka saa moja kamili usiku.

Kwenye semina hii tutapata mafunzo ya kina kutoka kwa kocha Dr Makirita Amani, pia tutapata kujifunza kutoka kwa walimu wengine. Na sehemu muhimu zaidi ya semina hii ni kwamba tutapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wanamafanikio wenzetu, kupata shuhuda halisi za jinsi ambavyo wenzetu wanapiga hatua kwenye maisha yao.

Hii ni nafasi moja ya mwaka ambayo hupaswi kuikosa kwa namna yoyote ile, kwa sababu utajifunza na kuhamasika, kisha unaondoka na nguvu ya kwenda kuweka juhudi kwa mwaka mzima na kupiga hatua zaidi.

Semina hii inawakusanya wanamafanikio wote kutoka kila kona ya Tanzania na wengine kutoka nchi jirani, ambao wanakuja pamoja na kujifunza kwa kina kwa siku moja na kuondoka na nguvu na hamasa kubwa ya kuchukua hatua ili kufanikiwa zaidi.

Kwenye semina ya mwaka huu 2019 tutakwenda kupata shuhuda nyingi sana kutoka kwa wenzetu ambao wamepiga hatua mbalimbali, kuanzia walipotoka na jinsi ambavyo wameweza kupiga hatua kupitia maarifa wanayopata pamoja na huduma nyingine wanazopata kama huduma za ukocha.

KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.

Ili kupata nafasi ya kushiriki semina ya kukutana ana kwa ana ya mwaka huu 2019, kwanza kabisa lazima uwe mwanachama hai wa KISIMA CHA MAARIFA, ambaye ada yake haijaisha.

Ukishakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unapaswa kulipa ada ya ushiriki wa semina ambayo ni tsh 100,000/= (laki moja). Ada hii itajumuisha huduma zote utakazozipata kwa siku nzima ya semina, kuanzia kifungua kinywa, chakula cha mchana, vitafunwa vya jioni, vijitabu vya kuandika na kalamu.

Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi jiunge sasa ili uweze kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kujiunga utapata manufaa mengine mengi sana, ya kujifunza pamoja na kuwa kwenye klabu za mafanikio. Kujiunga, tuma ujumbe sasa kwa wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA na utatumiwa maelekezo ya kujiunga.

MWISHO WA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI.

Mwisho wa kupata nafasi ya kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 ni tarehe 31/10/2019, hivyo unapaswa kuwa umeshalipa ada yako ya kushiriki semina hii mpaka kufikia tarehe hiyo.

Ili kuhakikisha kila mtu anashiriki semina hii natoa nafasi ya kulipa ada kidogo kidogo ili mpaka kufikia tarehe 31/10/2019 uwe umeshakamilisha malipo yako.

Unaweza kuchagua kulipa yote tsh 100,000/= kwa mara moja mapema na hapo ukajiweka uhakika wa kushiriki semina.

Unaweza kuchagua kulipa kila mwisho wa mwezi tsh 35,000/= kuanzia mwisho wa mwezi wa nane, wa tisa na wa kumi na hapo utajihakikishia kushiriki.

Unaweza kuchagua kulipa kila mwisho wa wiki, na kila wiki ukalipa tsh 10,000/= na ukawa umemaliza malipo yako ndani ya muda huo.

Lakini pia unaweza kuchagua kulipa kila siku, kwa kulipa tsh 1,500/= na ukilipa kila siku ndani ya siku zilizobaki utajihakikishia kupata nafasi ya kushiriki semina yetu ya mwaka 2019.

HATUA ZA KUCHUKUA LEO ILI USIKOSE SEMINA HII.

Rafiki, ili kuhakikisha hukosi semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi chukua hatua hii sasa, andika ujumbe wa kawaida au wasap na tuma kwenye namba 0717396253, ujumbe uwe na majina yako kamili, namba yako ya simu, barua pepe yako na maelezo kwamba utashiriki semina. Pia kwenye ujumbe huo eleza kama utalipa ada kwa siku, wiki, mwezi au mara moja, na tarehe utakayofanya hivyo.

Mfano wa ujumbe ni kama hivi; mimi Makirita Amani, simu; 0717396253, email; makirita@kisimachamaarifa.co.tz Nitashiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ada nitalipa kila tarehe ya mwisho wa mwezi.

Chukua hatua hiyo sasa rafiki yangu ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2019, kitu ambacho kitakupa msukumo mkubwa wa kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Asante sana rafiki yangu na nina uhakika tarehe 03/11/2019 tutakuwa pamoja kwenye semina, tuma ujumbe wako sasa wa kuthibitisha kushiriki ili usikose nafasi.

MUHIMU; Ili usisumbuke, thibitisha ushiriki wako mapema kwa kutuma ujumbe wenye majina yako, mawasiliano na mpango wako wa malipo.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge