Mpendwa rafiki,

Kila eneo la maisha yetu lina hitaji kazi, na kumbuka kuwa kazi bila kazi hiyo siyo kazi. Ndoa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.

Kama umechagua kuingia kwenye wito wa ndoa basi jua umeingia kwenye kazi, na siyo wito wa ndoa tu bali wito wowote ule, unahitaji kazi kama zilivyo kazi nyingine.

Kinachowafanya wandoa wengi kuchokana mapema  ni mazoea. Mwanzoni kila mwanandoa alikuwa na hamasa ya wenzake lakini kadiri ya muda unavyokwenda kila mtu anaanza kumchukulia mwenzake poa.

Hakuna kitu kibaya sana kama kumchulia mwenzako wa ndoa poa, hii inauwa ndoa, wengi ambao ndoa zao zimekuwa na shida walianza kuchukuliana poa, haweki tena juhudi kama za mwanzo wala kumjali mwenzake kama mwanzo.

Unafikiri ni kwanini wanandoa wakichepuka nje yaani kutoka nje ya ndoa wanakuwa wanavutiwa sana nje na kusahau ndoa zao?

KAVA IJUE NJAA YA WANANDOA

Ngoja nikuambie ukweli rafiki yangu, mara nyingi wandoa wanakuwa ni wanafiki sana, wakiwa na wenza wao wanajifanya kama wajinga hawajui kitu, anamuona mume au mke wake kama adui na siyo rafiki anashindwa kumshirikisha baadhi ya mambo kama rafiki yake wa karibu.

Sasa ikitokea mwandoa amejikutana na mchepuko wa nje, yule mchepuko anakuwa anajitoa kweli, haoneshi mazoea anakuwa mbunifu wa hali ya juu, anajitoa katika kazi anajua akijitoa vizuri utarudi tena. Anaweka kazi na ubunifu na sasa mtu akiwa kwenye ndoa yake anafanya mazoea unafikiri ataacha kukukimbia?

Ndiyo hivyo, ukiona mwenzako anatoka nje ya ndoa jua kabisa tatizo liko kwako, hujampa kile anachotaka, unajua huyo ni mteja wako hivyo usipompa kile anachokitaka ataendelea kukaa na wewe? Lazima ataenda sehemu ambayo atapata kile anachokitaka.

Wewe kama ni mwanandoa, hakikisha unajitoa kwa mke au mume wako, kuwa mbunifu, mwenzako anachepuka kwa sababu ya wewe kutokuwa mbunifu, kila siku ni mazoea yale yale.

SOMA; Ushauri Kwa Kijana Yeyote Anayetaka Kuingia Katika Mahusiano Ya Ndoa

Nikuambie kitu, akili ya binadamu inachoka mazoea, inapenda kuona mambo mapya kila siku, lakini ukiwa ni mtu wa mazoea, utamfanya mwenzako kuboreka.

Hebu niambie, kama unapata kila kitu kwenye ndoa yako, mke au mume wako anakupa kile unachotaka utathubutu kuangaika na watu wan je?

Hatua ya kuchukua leo; mke au mume shibisha njaa ya mwenza wako, kuwa mbunifu na mpe kile anachokitaka. Na kumbuka, kumhudumia kwa ubunifu wa hali ya juu kiasi kwamba hata akikutana na watu huko nje akikukumbuka jinsi unavyojitoa kwake hawezi kukubali kwenda kwa mwingine.

Kwahiyo, kuoa au kuolewa siyo mwisho wa safari, unatakiwa kujifunza sana. soma vitabu vinavyohusiana na ndoa, na kitabu kizuri cha kusoma kinachohusiana na ndoa ambacho hata mwandishi Dr. Makirita ameshauri ni kitabu cha IJUE NJAA YA WANANDOA. Kukipata, Kitabu hicho tuma ujumbe kupitia namba tajwa hapo chini ya makala

Makala hii imeandikwa na

Mwl. Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa  http://kessydeo.home.blog vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com //kessydeoblog@gmail.com

Asante sana