Rafiki yangu mpendwa,

Mwezi Oktoba mwaka 2016 nilitoa toleo la kwanza la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA. Kitabu ambacho kilikuwa na maarifa na mwongozo sahihi kwa yeyote anayetaka kuingia kwenye biashara lakini kazi inakuwa kikwazo kwao.

IMG-20161020-WA0053 ed

Nilitoa kitabu hiki baada ya kujifunza kwa wengi ambao walikuwa wakilalamikia hilo. Wapo ambao walijaribu kuanzisha biashara wakiwa kwenye ajira lakini zikashindwa. Na wapo wengi ambao walishindwa kabisa kuanzisha biashara kwa sababu ya kukosa muda, mtaji au wazo.

Kitabu hiki kilipokelewa vizuri sana sokoni, watu walikinunua, kukisoma na kuchukua hatua ya kuanzisha biashara zao wakiwa kwenye ajira. Baada ya nakala zilizochapwa za kitabu kile kuisha, kulikuwa na maombi mengi ya watu wakitaka kupata kitabu hicho, lakini sikutaka kukichapa tena kama kilivyokuwa awali.

Badala yake nilipanga kutoa toleo la pili, toleo ambalo litajibu baadhi ya changamoto ambazo nimejifunza kwa wale walioingia kwenye biashara wakiwa wameajiriwa. Lakini pia niliona toleo hilo linaweza kupata shuhuda za wale ambao walichukua hatua baada ya kusoma kitabu.

Na leo hii ninayo furaha kukujulisha kwamba TOLEO LA PILI la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA limetoka, kitabu ni kwa nakala ngumu na unaweza kukipata na kujifunza mengi sana kuhusu biashara.

makirita cover 3-01

Kitabu kinaitwa BIASHARA NDANI YA AJIRA, lakini kina mafunzo mazuri sana kwa watu wote wanaopanga kuingia au ambao tayari wapo kwenye biashara.

Kitabu kimejaa shuhuda za wale ambao wameweza kuanzisha biashara wakiwa kwenye ajira na zikafanikiwa. Lakini zaidi kitabu kina michanganuo ya biashara unazoweza kuanza kufanya, kuanzia isiyohitaji mtaji mpaka za mitaji midogo, ya kati na ya juu.

Kama unapanga kuingia kwenye biashara au kama tayari upo kwenye biashara na unataka kufanikiwa zaidi, basi kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA hupaswi kukosa kukisoma.

Kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, Toleo la pili kina sura kumi, ambazo zote zimejaa maarifa unayohitaji ili kutoka hapo ulipokwama sasa na kupiga hatua zaidi.

Sura ya kwanza inakuonesha kwa nini umefika hapo ulipo sasa na kwa nini ajira ni sehemu nzuri kwako kuanza biashara. Kwenye sura hii utajifunza kwa nini hupaswi kuchoma meli moto na msaada wa ajira kwako wakati biashara yako ni changa.

Sura ya pili inakupa faida kumi za kuanza biashara ukiwa kwenye ajira, hapa utaona kwa nini kama upo kwenye ajira, unapaswa kuwa na biashara ya pembeni. Ukianza biashara ukiwa kwenye ajira unakuwa na manufaa kuliko anayeanza biashara na hana ajira, hapa utaziona faida hizo.

Sura ya tatu inakufundisha jinsi ya kupata wazo bora la biashara kwako, wazo ambalo linaendana na wewe na ambalo utaweza kufanya makubwa. Watu wengi wamekuwa wanakwama kwenye wazo lipi wafanyie kazi, kwenye sura hii utaweza kufikia wazo sahihi kwako.

Sura ya nne utajifunza jinsi unavyoweza kupata mtaji wa kuanza biashara ukiwa kwenye ajira. Pia itajifunza jinsi unavyoweza kuanza biashara bila ya mtaji kabisa. Kuna njia nyingi sana unazoweza kutumia kupata mtaji wa kuanza biashara yako. Lakini pia zipo biashara unazoweza kuanza bila mtaji kabisa, kwenye sura hii utajifunza kwa kina kuhusu hilo la mtaji.

Sura ya tano utajifunza jinsi ya kupata muda wa kutosha kuendesha biashara na ajira kwa wakati mmoja, hapa utaona jinsi masaa yako 24 ya siku yanatosha kufanya mambo makubwa. Hapa utajifunza dhana nzuri sana ya kuwa na siku mbili ndani ya siku moja, ninachoweza kukuambia ni hiki, una muda mwingi sana, na sura hii itakuonesha unaupotezea wapi.

Sura ya sita utajifunza jinsi ya kutengeneza mfumo wa kuiendesha biashara yako ambao utakupa wewe uhuru, kwa kuwa na mfumo, hutahitaji kufanya kila kitu kwenye biashara yako, na pia hutahitaji kuwepo muda wote. Watu wengi wanaingia kwenye biashara na kushindwa ni kwa sababu biashara zinawategemea wao kwa kila kitu, kwa kusoma sura hii utaweza kuweka mfumo wa biashara kujiendesha hata kama haupo moja kwa moja.

Sura ya saba utapata michanganuo ya biashara 12 unazoweza kuanza kufanya. Biashara hizi zinaanzia ambazo hazihitaji mtaji kabisa, kisha za mitaji midogo kama elfu 50, laki 1 mpaka milioni 1. Kisha kuna za mitaji mikubwa kuanzia milioni 10 mpaka 20. Michanganuo yote hii ni kutoka kwa watu ambao wanafanya biashara hizo, hivyo unajifunza kutoka kwa wafanyaji kabisa na ukipenda kupata ushauri zaidi unaweza kuunganishwa nao.

Sura ya nane utajifunza jinsi ya kuilinda ajira na biashara yako na wakati sahihi wa kuondoka kwenye ajira. Utakapoanza biashara ukiwa kwenye ajira, siyo waajiriwa wenzako wote watafurahishwa na hilo, yatatokea majungu na fitina, hivyo unapaswa kuwa na njia ya kujilinda. Lakini pia wengi wamekuwa wanawahi kuondoka kwenye ajira zao au kuchelewa, hapa utajifunza wakati sahihi wa kuondoka.

Sura ya tisa unakwenda kujifunza mifereji nane ya kipato ambayo unapaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yako. Huwezi kuwa tajiri kwa chanzo kimoja cha kipato kama mshahara pekee. Kwenye sura hii utaondoka na vyanzo vinne unavyoweza kuanza kufanyia kazi mara moja.

Sura ya kumi inakwenda kukufundisha wakati sahihi wa kuanza ni sasa na siyo kesho. Watu wengi waliingia kwenye ajira wakijiambia wataifanya kwa muda tu, lengo lao ni kuwa na biashara. Lakini wanajikuta wakiahirisha, miaka inaenda, majukumu yanaongezeka, mshahara ni kidogo, madeni ni makubwa na hawaanzi biashara zao. kwa kusoma sura ya kumi, utaondoka na hatua za kwenda kuchukua mara moja.

NYONGEZA; Kwenye kila sura ya kitabu hiki, kuna ushuhuda wa mtu aliyeanza biashara akiwa kwenye ajira, changamoto alizokutana nazo, mafanikio aliyoyapata na ushauri wake kwa wale waliopo kwenye ajira. Kwenye shuhuda hizi unakwenda kujifunza kwa watu waliokuwa wamekwama kama wewe, wakachukua hatua na sasa siyo walalamikaji tena.

Rafiki, kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA Toleo la pili ni kitabu ambacho kila mwajiriwa anapaswa kukisoma na kuchukua hatua ili maisha yake yaweze kuwa bora zaidi.

Kama ulisoma toleo la kwanza, basi hakikisha hukosi toleo hili la pili, kwa sababu maarifa yaliyopo kwenye toleo la pili ni mara mbili ya yale yaliyokuwepo kwenye toleo la kwanza.

Kitabu kinapatikana kwa nakala ngumu (Hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=), ila kwa sababu wewe ni rafiki yangu na napenda sana upate kitabu hiki, utaweza kukipata kwa bei ya zawadi kama utakinunua kabla ya tarehe 31/10/2019. Bei ya zawadi itakuwa tsh elfu 15 (15,000/=).

Kupata kitabu hiki cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, piga simu au tuma ujumbe kwenda namba 0678 977 007 au 0752 977 170. Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu popote ulipo, kama upo mkoani utatumiwa kwa njia ya basi.

Rafiki yangu mpendwa, chukua hatua sasa upate kitabu hiki kwa bei ya zawadi, na uweze kutoka hapo ulipokwama kwa sasa kwa upande wa kipato. Pia kama utahitaji ushauri zaidi wa jinsi ya kuanza na kukuza biashara yako, nunua kitabu na ukisome ukishamaliza tuwasiliane. Sipendi kukuona ukilalamika wakati zipo hatua unazoweza kuchukua, anza sasa kwa kusoma kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA Toleo la pili na utaweza kuziona fursa nyingi zinazokuzunguka hapo ulipo na uchukue hatua.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha