3227; Kupigiwa makofi.
Rafiki yangu mpendwa,
Sisi binadamu kama viumbe wa kijamii huwa tunapenda sana kukubalika na wengine kwenye chochote tunachofanya.
Pale wengine wanapotusifia na kutupigia makofi kwenye kile tunachofanya ndiyo tunaona tunafanya kitu sahihi.
Lakini ukweli ni kwamba hakuna yeyote aliyewahi kufanya makubwa ambaye alikubalika na kusifiwa mwanzoni.
Wote walionekana kama wamechanganyikiwa kwa jinsi walivyoonekana kutaka kupata vitu vikubwa ambavyo havikuwa vimezoeleka.
Kama wangekata tamaa kwa sababu ya kutokukubalika mwanzoni, wasingeweza kufanya makubwa.
Wajibu wako mkubwa kwenye maisha ni kuyaendea maisha unayotaka kuyaishi kwa msukumo mkubwa na bila ya aibu wala kuchoka.
Hupaswi kusubiri kukubalika, kusifiwa au kupigiwa makofi.
Utakubalika sana kama utachagua kufanya mambo ya kawaida na yaliyozoeleka.
Utapigiwa makofi mengi kama utafuata mkumbo wa yale ambayo wengine wanafanya.
Lakini njia hiyo haitakufikisha mbali.
Kwani hata wanaokukubali na kukusifia, watafanya hivyo kwa muda tu.
Ukichagua njia ya kufanya makubwa kwenye maisha yako, mwanzo wengi hawatakuelewa.
Watakucheka, watakudharau, watakupinga na kukukatisha tamaa.
Kama utaweza kuyavuka yote hayo na kuendelea mpaka kupata ushindi, wote waliokuwa wanakukataa watakuwa ndiyo wanaokukubali.
Wajibu wako namba moja kwenye maisha siyo kuwaridhisha wengine kwanza, bali kuishi aina ya maisha unayotaka kuishi.
Hivyo ndivyo unavyoweza kupata ushindi mkubwa na unaopelekea ukubalike zaidi.
Ushindi mkuu na sahihi kwako ni kuyaishi maisha yako kwa ukamilifu wake.
Mengine yote yataweza kukaa sawa baada ya hilo kuwa sawa.
Usiyumbishwe na ugumu na kutokukubalika mwanzoni.
Hivyo ndivyo safari ilivyo kwa watu wote.
Haitakuwa tofauti kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
ahsante kocha
sita kata tamaa kwani kutokukubalika ndiyo safari ilivyo kwa watu wote,
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ndio safari ilivyo kwa watu wote.
LikeLike
Haiwezi kuwa tofauti kwetu.
LikeLike
Wajibu wangu namba moja kwenye maisha siyo kuwaridhisha wengine kwanza, bali kuishi aina ya maisha ninayotaka kuishi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kutokubalika siyo tatizo. Assnte sana kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Sitayumbishwa na ugumu na kutokukubalika.
shukrani kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Watakudharau mwanzo lakini,
wajibu wako namba moja kwenye maisha siyo kuwaridhisha wengine kwanza, bali kuishi aina ya maisha unayotaka kuishi.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ukichagua njia ya kufanya makubwa kwenye maisha yako, mwanzo wengi hawatakuelewa.
Watakucheka, watakudharau, watakupinga na kukukatisha tamaa.
LikeLike
Ndivyo ilivyo mara zote.
LikeLike
Nitaishi Maisha yangu kwa ukamilifu na wala sio kuwalidhisha wenge.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Asante sana kocha, sitakubali kuyumbishwa na chochote
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ahsante kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Ushindi pekee ni kuyaishi maisha yangu kwa ukamilifu
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hakuna yeyote aliyefanya makubwa ambaye alikubalika na kusifiwa mwanzoni. Sitayumbishwa na ugumu na kutokukubalika mwanzoni.
LikeLike
Vizuri
LikeLike