Habari rafiki yangu mpendwa,

Napenda kuchukua nafasi hii kukupa maendeleo muhimu kuhusu maandalizi ya tukio letu kubwa la mwaka, tukio muhimu sana kwa mafanikio yetu.

Tukio hili ni SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ambayo ni semina ya kukutana ana kwa ana inayofanyika mara moja kila mwaka.

Mwisho wa juma lililopita nilikuwa nafanya makubaliano na hoteli ambayo tutafanyia semina hii kwa mwaka huu 2018. Na baada ya kupitia kumbi mbalimbali ambazo hoteli ile inazo, nilifikia maamuzi ya kuchukua ukumbi unaobeba watu 100 pekee.

Hivyo napenda kukujulisha kwamba nafasi za kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ni 100 pekee, na hakuna nafasi hata moja ya ziada. Ni nafasi 100 za kukutana pamoja na kujifunza pamoja na kuhamasika ili kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yetu.

Mpaka sasa, watu ambao wamedhibitisha kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ni watu 89, hivyo nafasi zilizobaki ni 11 pekee ili kukamilisha idadi ya nafasi 100 zinazopatikana kushiriki semina ya mwaka huu.

semina 2017 3
Kocha Makirita Amani akifundisha

Hivyo nachukua nafasi hii kukutaarifu wewe rafiki yangu kwamba kama umepanga kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 na bado hujadhibitisha kushiriki, basi dhibitisha sasa. Na njia ya kudhibitisha ni kutuma ujumbe wenye majina yako, namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki semina. Ujumbe unatumwa kwenda namba 0717396253.

Rafiki yangu mpendwa, nafasi ni chache na hivyo watakaozipata ni wale ambao watadhibitisha na kufanya malipo yao mapema. Yaani wale wanaowahi ndiyo wanapata nafasi hizi za kipekee.

Hivyo nikusisitize sana, kama unataka usikose nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 usiache kudhibitisha leo.

Pia kwa wale ambao wamedhibitisha kushiriki semina, unapaswa kuwa umeanza kulipia ada yako ya kushiriki, kwa sababu kama utadhibitisha pekee na ukachelewa kulipa ada, nafasi yako atapewa mwingine atakayedhibitisha na kuanza kulipa ada yake.

KWA NINI NAFASI 100 PEKEE?

Swali moja ambalo najua utakuwa unajiuliza kwa nini nimetoa nafasi 100 pekee, kwa nini niweke ukomo, kwa nini nisiruhusu idadi kadiri ya watu wanavyotaka wenyewe?

Rafiki, chochote ninachofanya kwenye maisha yangu, kitu cha kwanza kabisa ninachoangalia ni thamani kiasi gani naongeza kwenye maisha ya wengine. Na huwa napenda thamani hiyo iwe kubwa kuliko kiwango ambacho mtu analipia. Kiwango watu wanacholipia kwa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA huwa kimekuwa ni kukubwa ukilinganisha na semina za aina nyingine ambazo watu wamezoea kushiriki. Hivyo thamani ambayo mtu anaondoka nayo inapaswa kuwa kubwa pia.

semina 2017 7
Picha ya pamoja na baadhi ya mafanikio

Hivyo huwa nimekuwa najipa kazi moja kubwa, kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA huwa najipa jukumu la kuhakikisha naongea ana kwa ana na kila mshiriki wa semina. Huwa napenda kujuana na kila anayeshiriki semina hii, na ikiwezekana kujua nini anafanya na hata changamoto anazokutana nazo.

Sasa kwa semina ya siku moja, idadi ya juu kabisa ya watu nitakaoweza kuongea nao ana kwa ana na kuwajua kwa kiasi kikubwa ni watu 100.

Hivyo karibu sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, siyo tu kwamba utashiriki semina, bali pia tutapata nafasi ya kuongea japo kwa muda mfupi, mimi na wewe.

MAELEZO ZAIDI KUHUSU SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 itafanyika jumamosi ya tarehe 03/11/2018 kwenye hoteli moja jijini dar es salaam. Ni semina ya siku nzima, kuanzia saa 1 asubuhi mpaka saa 1 jioni.

Ada ya kushiriki semina ya mwaka huu ni tsh 100,000/= ambayo itajumuisha huduma zote ambazo utazipata kwa siku ya semina, isipokuwa malazi kwa wale wanaosafiri.

Mwisho wa kulipa ada ya kushiriki semina hii ni tarehe 31/10/2018.

Nafasi za watu wa kushiriki semina hii ni 100 pekee, na ili kujihakikishia nafasi yako unapaswa kutuma ujumbe wenye majina yako pamoja na namba ya simu na kuanza kulipa ada yako.

Malipo ya ada yanafanyika kwa njia ya mpesa 0755 953 887 au tigo pesa/airtel money 0717 396 253 majina ya namba hizo ni Amani Makirita.

Unaweza kulipa ada yako kidogo kidogo ili mpaka kufikia tarehe 31/10/2018 uwe umeshakamilisha ada yako.

Kwa wale watakaosafiri kutoka mikoani, malazi yatapatikana kwenye hoteli tutakayofanyia semina, lakini malipo ya malazi ni ya kujitegemea, hayapo ndani ya malipo ya semina. Lakini pia siyo lazima kuchukua malazi yanayopatikana kwenye hoteli tutakayofanyia semina.

Nichukue nafasi hii kukualika kwenye semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2018, semina ambayo tunakwenda kukutana kwa pamoja, wale wote ambao tupo kwenye safari ya mafanikio makubwa na tuweze kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima unaofuata baada ya semina.

Tuma ujumbe wa kudhibitisha kushiriki semina hii leo kwenda namba 0717396253 na kisha anza kulipa ada yako ili usikose semina hii muhimu sana kwa mafanikio yetu kwa mwaka huu 2018 na mwaka unaokuja 2019.

Karibu sana rafiki yangu, nina imani tutakuwa pamoja tarehe 03/11/2018.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; http://eepurl.com/dDZHvL