Habari za leo rafiki yangu mpendwa?

Leo ninayo furaha kubwa kukupa taarifa za semina mpya ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO. Hii ni semina ya pili kwenye KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka huu 2019 na ndiyo semina ya mwisho kabla ya kuelekea kwenye semina kuu ya mwaka ya kukutana ana kwa ana.

Kila mwaka, wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, tumekuwa na semina mbili ambazo zinaendeshwa kupitia mtandao wa wasap na semina moja ya kukutana ana kwa ana.

Semina ya kwanza ya mtandaoni ya mwaka 2019 ilikuwa semina ya TABIA ZA KITAJIRI, na watu walijifunza na kuondoka na hatua za kuchukua ili kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi.

Sasa ni wakati wa semina ya pili, ambayo itahusu kutengeneza MFUMO WA KUENDESHA biashara yao ambao utaiwezesha biashara hiyo kufanikiwa sana.

business system

Kama upo kwenye biashara au unapata kuingia kwenye biashara, kuna kitu kimoja muhimu sana unachopaswa kukijua. Kitu hicho ni kwamba kinachoikwamisha biashara yoyote kukua ni mwanzilishi wa biashara hiyo.

Watu wengi wanapoanza biashara, wao huwa ndiyo kila kitu, kitu ambacho siyo kibaya. Biashara inafanya vizuri mwanzoni, wanatoa huduma nzuri na wateja wanaridhika na kuwaleta wengine. Na kadiri biashara inavyokua, ndivyo matatizo yanakuwa makubwa, ambayo mtu mmoja hawezi kuyafanyia kazi.

Hivyo kinachotokea ni mtu huyo aliyeanzisha biashara kuamua kuajiri mtu atakayemsaidia kwenye majukumu yake. Awali alikuwa anaendesha biashara yake kwa uelewa wake mwenyewe, sasa analeta mtu mpya ambaye hana uelewa kama wake lakini anategemea afanye kama yeye. Ni pale mtu huyo anaposhindwa kufanya kama yeye ndipo matatizo mengi huanzia.

Matatizo ya biashara nyingi huanza pale mtu anapojaribu kuajiri, badala ya biashara kupiga hatua, inaanza kurudi nyuma.

Matatizo mengine pia huwa yanaanza kabla hata mtu hajaajiri, pale majukumu yake kwenye biashara yanazidi uwezo wake wa kuyatekeleza kwa wakati.

Matatizo yote hayo ya biashara, ukomo ambao mtu anauweka kwenye biashara yake sababu yake kuu ni moja; KUKOSA MFUMO.

Kuendesha biashara kwa mazoea, bila ya kuwa na mfumo au mwongozo wowote ambao mtu anaufuata ni njia ya uhakika ya kushindwa kwenye biashara.

Mafanikio ya biashara yoyote ile hayatokani na ubora wa bidhaa au huduma, hiyo ni sehemu moja. Sehemu kubwa ya mafanikio inatokana na mfumo ambao unaendesha biashara hiyo.

Nikupe mfano ili tuelewane vizuri hapo, kama umewahi kula maandazi yanayotengenezwa na kampuni kubwa kama Azam, utakubaliana na mimi kwamba kuna watu mtaani ambao wanatengeneza maandazi mazuri na matamu kuliko ya Azam. Tena mnayapenda sana maandazi hayo. Lakini kwa nini mtu wa mtaani anayetengeneza maandazi mazuri na matamu anashindwa na kampuni ya Azam ambayo ina maandazi ya kawaida? Unaweza kusema Azam ni kampuni kubwa na ina fedha nyingi, lakini ukweli siyo huo. Ukweli ni kwamba Azam ana mfumo mzuri wa utengenezaji na usambazaji wa maandazi yake, hivyo anaweza kuwafikia watu wengi kwa uhakika.

Hivyo ndivyo mfumo unaiwezesha biashara kuzalisha bidhaa au huduma kwa kiwango kile kile na kuweza kuisambaza kwa wateja wake.

BIASHARA YAKO INAHITAJI MFUMO.

Nimekuwa nakuambia kitu kimoja rafiki, kama unataka uhuru kwenye maisha yako, unapaswa kuwa na biashara. Unapaswa kuwa na njia ya kukuingizia kipato ambayo maamuzi ya mwisho hayapo kwa mtu mmoja.

Leo nakuongezea kitu cha pili, ili kuwa na maisha yenye uhuru, unapaswa kuwa na biashara inayojiendesha kwa mfumo sahihi.

Kwa sababu kuwa na biashara ambayo haijiendeshi kwa mfumo siyo kuwa huru, bali ni kuwa mtumwa wa biashara yako mwenyewe.

Watu wengi waliopo kwenye biashara, wanafikiri wapo huru kufanya mambo yao, lakini ukweli ni kwamba hawana uhuru kabisa, wamefungwa ndani ya biashara hizo.

Wamefungwa kwa sababu hawawezi kuondoka kwenye biashara hizo kwa muda na biashara zikaenda vizuri zenyewe. Wao ndiyo biashara na biashara ni wao, wakipata changamoto kidogo na biashara zao zinapata changamoto pia.

Suluhisho litakalokupa uhuru kamili ni kuendesha biashara yako kwa mfumo, mfumo ambao utaiwezesha biashara kusimama yenyewe na kuweza kujiendesha hata kama wewe hupo.

MFUMO HAUANGALII UKUBWA WA BIASHARA.

Kuna kitu kimoja ambacho watu wamekuwa wanajidanganya sana kuhusu kuendesha biashara kwa mfumo. Wengi hujiambia wataweka mfumo kwenye biashara zao baada ya biashara kukua. Na hapo ndipo wanapojichelewesha, kwa sababu mpaka pale biashara inapokuwa imeshakua kubwa, inakuwa imeshamtegemea sana mwanzilishi wake kiasi kwamba uwekaji wa mfumo unakuwa mgumu.

Wakati mzuri wa kutengeneza mfumo wa kuendesha biashara yako ni wakati biashara hiyo ni changa, hapa unaweza kuipangilia vizuri na inapokuwa inakua, inakuwa kwa mfumo.

Wakati mzuri wa kuweka mfumo kwenye biashara yako ni pale unapoianza, na wakati mwingine sahihi ni sasa, baada ya kugundua kwamba kukosa mfumo kwenye biashara yako ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya biashara hiyo.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Rafiki, baada ya kuona changamoto kubwa ambazo wafanyabiashara wengi wanapitia, hasa ya kukosa uhuru licha ya kuwa kwenye biashara. Na baada ya kujifunza na kutafiti kwa kina, nimekuandalia semina nzuri ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki semina hii ukiwa popote duniani, na huhitaji kusafiri au kuacha shughuli zako za kila siku, ni kutenga tu muda ndani ya siku yako wa kufuatilia masomo ya semina.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi, ambapo kila siku utapata somo la jinsi ya kutengeneza mfumo kwenye biashara yako. Masomo haya yatakuwa na mifano halisi ya hatua unazopaswa kuchukua ili biashara yako ijiendeshe kwa mfumo. Pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi zaidi kwenye maeneo ambayo hayajaeleweka.

Semina hii itaanza rasmi tarehe 04/07/2019 mpaka tarehe 14/07/2019, kila siku asubuhi utapata somo la semina na utaweza kuuliza maswali kuhusiana na somo hilo. Masomo yote yatatumwa kwenye kundi la wasap na hivyo utaweza kuyafuatilia kwa urahisi.

Japokuwa semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao, utajifunza kwa kina sana na kuondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kuliko unavyoweza kujifunza kwenye semina ya kuhudhuria ana kwa ana. Kwa sababu semina hii ya mtandaoni inakwenda kwa kina sana kitu ambacho siyo rahisi kukifanya kwenye semina ya siku moja ya ana kwa ana.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA.

Rafiki, ili uweze kushiriki semina hii nzuri sana itakayokupa uhuru kamili wa maisha yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa moja kwa moja kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya programu za mafunzo na ukocha ninayoendesha, ambapo watu wanajifunza na kuhamasika kila siku, kisha kuchukua hatua na maisha yao kuwa bora sana.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ada yako iko hai basi tayari umeshajihakikishia kushiriki semina hii. Wewe jiandae tu, kaa mkao wa kujifunza na utaondoka na nondo za kwenda kuiendesha biashara yako vizuri.

Kama ni mwanachama lakini ada yako inaisha karibuni, lipa ada yako mapema ili usikose nafasi ya kushiriki semina hii. Hakikisha hutoki ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kunufaika zaidi na mafunzo haya na mengine mengi.

Kama wewe siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina hii ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, unapaswa kujiunga na kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Hapa unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima tangu tarehe uliyolipia. Utapata mafunzo ya semina mbili zinazofanyika mtandaoni kwa mwaka, na pia utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kocha wako, tukijifunza kwa kina. Pia tunakwenda kuwa ka Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinakupa jumuiya ya watu ulionao karibu ambao wanapiga hatua kufanikiwa zaidi.

JINSI YA KULIPA ADA.

Ili kulipa ada ya kushiriki semina hii, tuma kwenye namba zifuatazo;

TIGO PESA / AIRTEL MONEY – 0717 396 253 (Jina AMANI MAKIRITA)

M-PESA – 0755 953 887 (Jina AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa wasap  kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA.

MWISHO WA KULIPIA ILI KUSHIRIKI SEMINA.

Rafiki, mwisho wa kulipia ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kupata mafunzo ya semina hii ni tarehe 01/07/2019.

Ili ujihakikishie kushiriki semina hii na kuweza kuikuza biashara yako, lipa ada yako mapema kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.

Ninaamini unapenda sana kupiga hatua na kufanikiwa kwenye biashara yako,

Ninaamini hilo linawezekana kabisa, kwa sababu nimeona wengi wakianzia chini na kupiga hatua zaidi.

Na nina imani kubwa kwenye mafunzo niliyokuandalia, yanakwenda kukupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako, hata kama biashara yako ni ndogo sana.

Karibu sana ushiriki semina hii ya MFUMO WA BIASHARA na utaweza kupiga hatua zaidi. Kumbuka kulipa ada yako kwa wakati, kabla ya tarehe 01/07/2019 ili uweze kunufaika na mafunzo haya yatakayoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Nakusubiri kwa shauku kubwa kwenye semina hii ya MFUMO WA BIASHARA, kwa sababu najua utaondoka na mengi ya kuiwezesha biashara yako kukua zaidi. Usipange kukosa semina hii.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge