Mpendwa rafiki yangu,
Zama ambazo vijana wengi wanahangaika kumpata mtu sahihi ni zama hizi kwa sababu watu wengi wanakuwa wanavaa barakoi yaani mask katika nyuzo zao hivyo ni ngumu kumjua yupi ni mtu sahihi kwako kama ukiingia kichwa kichwa. Watu wamekuwa ni wa kufanya maamuzi kwenye eneo la mahusiano kwa kutumia hisia badala ya kutumia akili.
Huwa watu wanafanya maamuzi kwa hisia halafu baadaye wanakuja kuamua kwa akili baada ya kufanya maamuzi. Tunakuwa na kesi nyingi ambazo ukizichunguza utagundua ni watu wanafanya maamuzi bila kufikiri, fikra zinakuwa chini pale wanapofanya maamuzi yao na wanajikuta wanakosea sana katika maamuzi kwa sababu hakuna anayeweza kubaki salama kama akiwa ni mtu wa kufanya maamuzi pale fikra zake zinapokuwa chini na hisia ziko juu.
Vijana wengi wanajikuta wanatumia muda mwingi kumtafuta mtu sahihi kwao ambae wanaweza kuwa pamoja katika maisha ya wito wa ndoa. Tunasahau ile falsafa ya kuwa huwezi kumpata mtu sahihi katika maisha yako kama wewe siyo mtu sahihi. Mtu ni mlevi wa kupindukia halafu anamtafuta mtu ambaye amatulia ni mchaMungu kwa hali kama hiyo ni sawa na kusubiri meli uwanja wa ndege, na utasubiri bila mafanikio miaka yako yote.
Kama unataka kumpata mtu sahihi kwanza unatakiwa kuwa mtu sahihi wewe mwenyewe, yaani sifa za yule unayemtaka kuwa naye anza kuwa nazo wewe na kama unajua sheria ya nguvu ya uvutanao itakukutanisha na yule anayeendana na tabia zako.
Kwa kijana yeyote anayetaka kuingia katika wito wa ndoa anatakiwa kufanya yafuatayo; kwanza kuwa na vigezo kabisa unataka kuwa na mtu wa namna gani? wengi wanatafuta wenza wa kuishi nao lakini changamoto kubwa wanatafuta wakiwa hawana vigezo hivyo kama unavyojua unapotafuta bila vigezo ni rahisi kupata hata kile usichostahili hivyo yoyote anayekujia mbele yako kwa sababu umri umeenda wazazi, marafiki wanakusema sana kwanini hauoi basi unajikuta unafanya maamuzi ya fasta unaoa hata usimyetarajia ili kuwafurahisha watu ambao hata hawataenda kuishi naye.
SOMA; Hii Ndiyo Dalili Ya Ndoa Isiyokuwa Na Uhai
Hivyo basi, kama wewe uko kwenye ndoa au unataka kuingia kwenye ndoa nimekuandalia maarifa sahihi ya kukuwezesha wewe kukufanikiwa katika eneo la mahusiano kwa ujumla. Nimekuandalia kitabu ambacho kipo tayari kinachoitwa Ijue Njaa Ya Wanandoa.
Kitabu ni kizuri mno na mwandishi wa Dibaji ya kitabu hiki ni Dr. Makirita Amani na yeye baada ya kukisoma aliyaandika haya ‘’ kama upo kwenye ndoa au unapanga kuingia kwenye ndoa basi unapaswa kusoma kitabu hiki. Kama upo makini na maisha yako na unataka kuwa na mahusiano bora na watu wengine hakikisha unasoma kitabu hiki. Na kwa kuwa tunajua hakuna binadamu ambaye ni kisiwa, wote tunahusika na wengine. Hivyo basi, kusoma kitabu hiki ni moja ya hitaji muhimu la kuwa na maisha bora.’’
Rafiki, nakuhakikisha kama uko njia panda katika mahusiano yako jipataie nakala yako ya kitabu cha Ijue Njaa Ya Wanandoa. Kitabu kinauzwa shilingi elfu Kumi lakini nimekitoa kwa bei ya ofa ya shilingi elfu tano ambayo inaishia tarehe tano ya mwezi juni mwaka 2019. Okoa shilingi elfu tano kwa kununua kitabu hiki kwa bei ya ofa ili uweze kukisoma na kuchota maarifa ambayo yatakusaidia kuwa na ndoa bora na mahusiano kiujumla.
Jinsi ya kupata kitabu hiki, tuma malipo kwenda namba 0717101505 kwa wale wa tigo pesa,airtell money na kwa wale wa mpesa tuma malipo 0767101504. Kisha tuma na email yako ili uweze kutumiwa kitabu popote ulipo duniani. Kitabu hiki kipo katika mfumo wa soft copy yaani nakala tete, unaweza kusomea kwenye simu yako yaani smart phone, pc yaani kompyuta na hata tablet.
Hatua ya kuchukua leo; kabla hujaingia kwenye maisha ya ndoa pata kwanza elimu itakayokusaidia kuwa na maisha bora ya mahusiano yako, hakikisha unakuwa na vigezo ni mtu wa namna gani unapaswa kuwa naye.
Kwahiyo, unapokuwa na mwongozo wowote wa kufanya jambo katika maisha yako ni ngumu sana kukosea kwa sababu mwongozo utakuwa unakusaidia kukuelekeza njia sahihi ya kupita. Hivyo basi, tuwe watu wa kupenda kusoma vitabu vinavyohusiana yale ambayo tunayafanya ili tuweze kuwa bora. Kamwe usichukulie poa mahusiano yako unatakiwa kuyaboresha kila siku.
Makala hii imeandikwa na
Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa www.mtaalamu.net/kessydeo, vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI. Karibu sana.
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Mwl, Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana