Rafiki yangu mpendwa,

Kwa muda sasa nimekuwa naweka juhudi kubwa sana katika kukushirikisha maarifa bora kwa ajili ya mafanikio yako.

Msingi mkuu ambao nimekuwa nausimamia kwenye hili ninalofanya ni huu; MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA = MAFANIKIO MAKUBWA.

Hivyo wajibu wangu umekuwa kukuandalia wewe maarifa sahihi, wajibu wako ni kuyasoma na kuchukua hatua na matokeo ni mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Wapo watu ambao wamekuwa wanapenda sana kujifunza kupitia kazi zangu, lakini wengi wamekuwa wanasema wanakwama kwa sababu ya gharama kubwa ya mafunzo ninayotoa. Na hilo lina ukweli, lakini kuna eneo kubwa ambalo wengi hawaliangalii katika mafunzo ambayo ninayashirikisha.

Na kwenye makala hii ya leo nakwenda kukushirikisha jinsia ambavyo unaweza kupata maarifa bora kabisa ya mafanikio bila ya kulipa fedha yoyote.

Kabla sijakuonesha njia hiyo, nikushirikishe alichoniandikia msomaji mwenzetu kuhusu hili;

Asante sana doctor. Kwa mara ya kwanza nilipojiunga na AMKA TANZANIA nilifikiri sitaweza kujifunza chochote sababu sikuweza kulipa ile ada. Siku nilipo log in kwenye email yangu nikashangaa nakuta vitu vizuri, nlifurahi sana. Umekuwa Mwalimu wangu sasa. Mungu akubariki ASANTE – Agape Bernard.

Kama alivyoandika rafiki yetu Agape hapo juu, wengi wanaposikia ada ya kujiunga na programu mbalimbali ninazotoa hukata tamaa na kuona hawawezi kujifunza kwa kuwa hawana ada ya kulipa. Lakini hapo wanajizuia kupata mafunzo bora kabisa tena bila ya kulipa gharama yoyote.

NGAZI ZA MAFUNZO NINAYOTOA.

Rafiki, mafunzo ninayotoa yamegawanyika kwenye ngazi mbalimbali.

Ngazi ya kwanza ni mafunzo ya bure kabisa, haya unayapata bure bila ya kulipa hata senti moja. Mafunzo haya ya bure unayapata kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA na pia kwenye email yako ambapo mafunzo yanatumwa moja kwa moja unapokuwa umejiunga na mfumo wetu wa email. Kunufaika na ngazi hii ya kwanza ya mafunzo kila siku tembelea www.amkamtanzania.com na ujifunze. Pia jiunge na mfumo wetu wa email kwa kutembelea www.amkamtanzania.com/jiunge na ufuate maelekezo ya kujaza fomu na kila siku utapokea mafunzo mazuri kwenye email yako, bila ya kulipa gharama yoyote.

Ngazi ya pili ni vitabu mbalimbali nilivyoandika. Kupitia vitabu hivi unakwenda kupata maarifa mengi sana lakini kwa gharama ambayo ni ndogo. Mfano kitabu KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, kina sababu 25 zinazowafanya wengi kubaki kwenye umasikini, ambazo ukizifanyia kazi huwezi kubaki kwenye umasikini kamwe. Gharama ya kitabu hicho ni elfu 5 tu, sasa fikiria uwekezaji wa elfu 5 unaweza kukutoa kwenye umasikini, je huoni ni sawa na bure? Kupata vitabu mbalimbali nilivyoandika tembelea www.amkamtanzania.com/vitabu

KWA NINI SIYO TAJIRI

Ngazi ya tatu ni KISIMA CHA MAARIFA, hapa sasa unakuwa umeshajifunza bure kabisa na kuona maarifa ninayotoa yanaendana na wewe, umeyajaribu na kupata matokeo mazuri na kujiambia sasa nahitaji zaidi. Hapo sasa unakaribia kwenye KISIMA CHA MAARIFA ambapo unapaswa kulipa ada (ambayo kwa wengi ni kubwa) ili uweze kujifunza zaidi. Wengi wanaposikia ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA hustuka kwa nini ni kubwa. Lakini kwa wale ambao wameshajifunza kupitia AMKA MTANZANIA, wakafanyia kazi na kuona matokeo mazuri kwenye maisha yao, hawashangai ukubwa wa ada hiyo. Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA na utapewa utaratibu wa kujiunga.

Ngazi ya nne ya huduma ninazotoa ni huduma mbalimbali za ukocha. Hapa kuna ukocha kwa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING), ukocha wa kupiga hatua kwenye biashara (LEVEL UP) na ukocha wa kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako (GAME CHANGERS). Huduma hizi za ukocha zinakutaka kwanza uwe kwenye KISIMA CHA MAAARIFA ndiyo uweze kunufaika nazo. Gharama zake ni tofauti na ukiacha PERSONAL COACHING ambayo unaweza kuomba kushiriki muda wowote, LEVEL UP na GAME CHANGERS huwa zinakuja kwa msimu maalumu.

JINSI YA KUNUFAIKA NA MAFUNZO HAYA YA MAFANIKIO BURE KABISA.

Rafiki, ahadi yangu kwako kwenye makala hii ni jinsi gani unaweza kunufaika na mafunzo haya ya mafanikio bure kabisa.

Na nimeshakueleza kwenye hatua ya kwanza hapo juu, tembelea AMKA MTANZANIA kila siku, huko kuna makala zaidi ya elfu 2, zote ni nzuri na zina mafunzo mazuri kwako, kama ukiyafanyia kazi basi maisha yako hayatabaki pale yalipo sasa.

Pia jiunge na mfumo wetu wa email kwa kufungua www.amkamtanzania.com/jiunge kisha fuata maelekezo na jaza fomu.

USHAURI WANGU KWAKO KUHUSU KULIPIA HUDUMA NINAZOTOA.

Rafiki, nimekuwa nakushirikisha falsafa yangu ya maisha ya kufanikiwa kwenye maisha ambayo inasema ILI KUPATA UNACHOTAKA, WASAIDIE WENGINE WAPATE WANACHOTAKA.

Hivyo kazi hii ninayoifanya, lengo lake la kwanza ni kukupa kwanza wewe kile unachotaka kabla hujanipa mimi ninachotaka.

Ndiyo maana nimekuwa sishauri mtu yeyote alipie huduma zangu mara moja baada ya kukutana nazo. Badala yake nimekuwa nashauri mtu unapokutana na mafunzo yangu ya bure, kujifunza kwanza, kisha kuchukua hatua na unapopata matokeo mazuri basi unakaribia ili kujifunza zaidi.

Rafiki, karibu sana twende pamoja kwenye safari hii ya mafanikio, iwe una fedha au huna, una fursa kubwa ya kujifunza na kuyafanya maisha yako kuwa bora.

Muhimu ni uwe na utayari wa kujifunza na kufanyia kazi yale uliyojifunza na utaweza kuona matokeo mazuri kwenye maisha yako.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha