Rafiki yangu mpendwa,

Wakati naanza kazi hii ya uandishi na mafunzo ya mafanikio, watu wengi sana walikuwa wakiomba tukutane kwa ajili ya kupata ushauri.

Kwa kuwa ninapenda sana kuwasaidia watu waweze kupiga hatua, nilikuwa nakubali tukutane kwa ajili ya ushauri. Lakini pia nikawa nawatafuta watu baada ya muda kutaka kujua ushauri niliowapa umewasaidiaje.

Hapo ndipo nilipopatwa na mshangao mkubwa, kwanza baadhi hawakuwa hata wanakumbuka tulishauriana nini. Na kwa wale waliokuwa wanakumbuka, hawakuwa wamefanya chochote. Bado walikuwa na sababu mbalimbali kwa nini hawawezi kuanza.

Na hapo ndipo nilipobadili mfumo wangu wa utoaji wa ushauri, ili ushauri ninaotoa uwe na tija kwa anayepokea, lakini pia nisipoteze muda ambao ningeweza kuutumia kutoa maarifa zaidi, kushauri watu ambao hawaendi kufanya chochote.

Kwa utaratibu mpya, nimekuwa natoa ushauri kwa wale ambao ni wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA pekee, kwa sababu watu hao nina njia ya kufuatilia hatua wanazochukua kwa tathmini wanazojifanyia kila mwezi.

Leo nakwenda kukushirikisha sababu tano kwa nini ushauri ambao umekuwa unaomba na kupokea umekuwa haukusaidii na hatua za kuchukua ili ushauri unaopata ukusaidie. Haya nimeyaona kupitia tathmini ambazo nimekuwa nafanya kwa wale ninaowapa ushauri kwenye maeneo mbalimbali.

Moja; Unapenda ushauri wa bure.

Kisaikolojia, sisi binadamu huwa hatuthamini kitu chochote ambacho tunakipata bure au kwa urahisi, huwa tunaona hakina thamani. Lakini kile ambacho tumekigharamia au kukipata kwa ugumu, huwa tunakithamini sana.

Ndiyo maana hata mtu anapopata fedha kwa urahisi, kama kushinda bahati nasibu au kupata urithi, huwa anazitumia hovyo mpaka zinaisha.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye ushauri, ukipewa ushauri wa bure huuthamini, unaona ni kitu cha kawaida na hivyo hufanyii kazi. Lakini kama utagharamia kupata ushauri, basi utahakikisha gharama zako hazipotei bure, utafanya kitu na huo ushauri.

Hivyo kama unataka ushauri ukusaidie, gharamia kupata ushauri huo.

Mbili; hutafuti ushauri, bali uthibitisho.

Mara nyingi unapoenda kwa watu kuomba ushauri, unachofuata siyo ushauri, bali uthibitisho. Tayari unakuwa umeshaamua nini utafanya, ila tu hujiamini, hivyo unataka kusikia wengine wanasemaje.

Hivyo mtu anapokushauri kinyume na ulivyochagua yeye, unaona ushauri wake haufai na hivyo huutumii. Tatizo linakuwa siyo ushauri, bali wewe mwenyewe.

Kama unataka kupata ushauri sahihi na utakaokusaidia, omba ushauri kabla hujafanya maamuzi yako mwenyewe. Hapo utaweza kunufaika na michango hata ya wale wanaokuambia usichopenda.

Tatu; huna anayekufuatilia kwa karibu.

Sisi binadamu tunaweza kuweka mipango mizuri na mikubwa sana, lakini inapofika kwenye utekelezaji, ndipo changamoto huanza. Tuna tatizo kubwa sana la nidhamu binafsi, ni vigumu kwetu kufanya yale tuliyopanga.

Ndiyo maana unaweza kushauriwa vizuri, na ukapanga hatua za kuchukua, lakini baada ya kuanza kufanyia kazi ushauri huo, hufiki mbali, unaishia njiani.

Ili unufaike na ushauri, hakikisha unakuwa na mtu au watu wanaokufuatilia katika utekelezaji wa yale uliyoshauriwa kufanya.

Nne; hujafanya maamuzi unataka nini.

Mara nyingi umekuwa unaona kitu fulani, unavutiwa nacho, unaomba ushauri, unashauriwa, kabla hujaanza kufanyia kazi, unaona kitu kingine, unakipenda na kuomba ushauri mwingine.

Kwa kipindi kirefu unajikuta ni mtu wa kuomba ushauri kwenye kila jambo, lakini hakuna hatua unazochukua na hakuna mabadiliko unayoyapata.

Kama unataka ushauri ambao utakusaidia, basi amua kwanza unataka nini. Na kama hujajua unataka nini mweleze wazi anayekupa ushauri, kisha chagua kufanyia kazi kitu kimoja mpaka utakapopata matokeo na siyo kujaribu kitu kipya kila wakati.

Tano; unaendekeza sababu.

Kabla hujaomba ushauri ulikuwa na sababu unazojipa kwa nini hufanyi. Unaomba ushauri na kupewa, lakini bado unang’ang’ana na sababu zako. Kwa njia hiyo, hakuna ushauri unaoweza kukusaidia.

Kama bado unaamini kwenye sababu zilizokuwa zinakuzuia, ushauri hauwezi kukusaidia. Hivyo unapoomba ushauri, weka sababu kando na chukua hatua kwenye yale uliyoshauriwa.

Rafiki, hizo ndiyo sababu tano kwa nini ushauri unaopewa haukusaidii. Nina habari njema kwako, kwamba ipo njia ya kupata ushauri ambao utakugharimu, utasimamiwa kutekeleza na hutapata nafasi ya kuleta sababu, je upo tayari kwa njia hiyo? Soma hapo chini.

Karibu upate ushauri utakaokusaidia.

Rafiki yangu mpendwa, kama umechoshwa na ushauri ambao umekuwa unaomba na kupata lakini haukusaidii, na umeshachagua nini unataka kwenye maisha yako, basi nikukaribishe sehemu ambayo utapata ushauri wenye manufaa kwako.

Sehemu pekee ambapo siyo tu utapata ushauri, bali pia mafunzo na fuatiliaji wa karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unapata nafasi ya kupata ushauri kutoka kwa kocha, lakini pia atakufuatilia katika utekelezaji wa yale mnayokuwa mmeafiki ufanyie kazi.

Rafiki, jua kabisa kwamba safari ya mafanikio siyo rahisi, na peke yako utakutana na vikwazo vingi. Unahitaji kuwa eneo ambalo litakupa nguvu ya kupambana na vikwazo hivyo. Katibu ujiunge kwa maelezo yanayopatikana hapo chini, yasome mpaka mwisho.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania