“When you make an effort not to blame other people, your life becomes much easier, but very few people make this small effort.” – Leo Tolstoy

Kama unataka maisha yako yawe rahisi, acha kuwalaumu wengine.
Shika hatamu ya maisha yako na jua chochote kinachotokea au kutokutokea kwenye maisha yako ni wajibu wako.
Huna yeyote wa kumlaumu, ni wewe mwenyewe kwa hatua ulizochukua au ambazo hukuchukua.

Unapolaumu wengine maana yale unajiambia wewe ni dhaifu na ambaye huna mamlaka na maisha yako.
Wale unaowalaumu unawapa nguvu kubwa ya kuyatawala maisha yako.
Unajiona ni mnyonge usiyeweza kuyasimamia maisha yako,
Na kadiri unavyowalaumu wengine, ndivyo unavyoshindwa kuchukua jukumu la maisha yako.

Kama kuna kitu chochote kimetokea au kutokutokea kwenye maisha yako, ambacho ni kinyume na ulivyotegemea,
Kuna mtu mmoja tu wa kulaumu, mtu huyo ni wewe mwenyewe.
Kama kuna mtu amekuibia, wa kumlaumu ni wewe, kwa kukosa umakini mpaka ukaibiwa.
Kama kuna mtu ulimwamini ila baadaye akakusaliti, wakulaumiwa ni wewe kwa kumwamini mtu asiye sahihi
Hakuna chochote kinachotokea kwenye maisha yako, ambacho wewe mwenyewe hujakichangia.
Ndiyo maana kuwalaumu wengine hakutakusaidia.

Ukiwalaumu wengine unajiona wewe ni mjamilifu na huna cha kubadili.
Hivyo unaendelea kurudia yale yale uliyofanya.
Lakini unapojilaumu mwenyewe, unaona wapi umekosea na hivyo kuhakikisha hukosei tena.
Unachotaka kwenye maisha yako siyo kuonekana huna hatia au hukosei,
Unachotaka ni kuwa bora zaidi kila siku,
Na huwezi kuwa bora kama unatumia muda mwingi kuwalaumu wengine.
Peleka lawama zote kwako na utaona hatua sahihi za kuchukua ili mambo yasijirudie tena.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania