Rafiki yangu mpendwa,

Mafanikio yoyote ambayo nimewahi kuyapata kwenye maisha yangu, kuna kitu kimoja ambacho siwezi kuacha kukishukuru.

Kitu hicho ni usomaji wa vitabu. Hii ni tabia ambayo imejengeka ndani yangu tangu kipindi nikiwa shuleni. Nakumbuka wakati wanafunzi wengine walikuwa wakipenda kusoma notsi zilizoandaliwa na walimu na watu wengine, mimi nilikuwa nasoma vitabu na kuandaa notsi zangu mwenyewe. Jambo hili moja liliniwezesha kuwa na ufaulu mkubwa sana kwenye masomo yangu, kwa sababu kupitia usomaji wa vitabu, sikuwa na kariri, badala yake nilikuwa naelewa dhana nzima na hivyo swali linapokuja tofauti kwenye mtihani, inakuwa rahisi kulielewa na kulijibu.

Tukija upande wa maisha, vitu vingi ninavyofanya sasa nimejifunza kutoka kwenye vitabu. Wakati nilipotoka chuoni nikiwa sijui nifanye nini, nilianza na kusoma vitabu, na hapo ndipo ulimwengu wangu ulipofunguka na kuona kila aina ya fursa ya kupiga hatua zaidi hata kama mambo ni magumu kiasi gani.

Ni faida hii kubwa ya usomaji wa vitabu imekuwa inanisukuma kila mara kuwasisitiza wengine kusoma vitabu zaidi.

soma vitabu zaidi

Kila mara nimekuwa natafuta ipi njia bora ya kuwasaidia watu kusoma vitabu zaidi, mwaka 2014 nilianzisha programu ya kusoma vitabu zaidi ya 100 kwa mwaka, kwa kusoma vitabu viwili tu kwa wiki, mwanzo ilionekana kuwa ngumu lakini mpaka sasa inaendelea.

Mwaka 2017 nilianzisha programu ya KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU, ambapo mtu alipaswa kusoma angalau kurasa kumi za kitabu kwa siku, kitu ambacho kitamwezesha kumaliza kitabu kimoja kila mwezi na vitabu zaidi ya 10 kwa mwaka. Nayo ni programu ambayo mpaka sasa inaendelea.

Pia kila mwezi na kila juma nimekuwa nashirikisha vitabu mbalimbali nilivyosoma na kuwashauri wengine wavisome.

Katika kufanya kazi hii ya kuwasaidia wengine  wengi zaidi kusoma, nimeziona changamoto mbili kubwa ambazo zinawazuia wengi wasiweze kusoma.

Changamoto ya kwanza ni muda, watu hawana muda kabisa wa kusoma vitabu, au hata kufanya mengine muhimu kwenye maisha yao. Kwa namna dunia ya sasa inavyoenda kasi, na teknolojia zinazotufuata kila tunapokwenda, muda wa kusoma umekuwa kitu cha mwisho kufikiriwa na wengi.

Changamoto ya ipi ni upatikanaji wa vitabu, wengi wamekuwa wanashindwa kupata vitabu vizuri vya kusoma, moja kwa kukosa fedha za kununua vitabu vingi vya kusoma na mbili kwa kushindwa kuelewa lugha ya kiingereza, ambayo ndiyo vitabu vingi vimeandikwa kwa lugha hiyo.

Lakini pamoja na changamoto hizi mbili kubwa, bado roho inaniuma ana pale ambapo naona watu wanateseka na maisha wakati majibu ya kila mateso ya maisha tayari yapo kwenye vitabu.

Na hapa ndipo nilipofikiria njia bora zaidi ya kutatua changamoto hizo mbili za usomaji wa vitabu, na kuja na CHANNEL MPYA YA TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA.

Kupitia channel hii, kila juma nasoma na kuchambua kwa kina sana kitabu kimoja. Kwenye kitabu hicho, tutapata makala ya TANO ZA JUMA ambayo inakuwa imezama ndani sana kwenye kitabu hisika, kisha tunapata masomo ya ziada (haya nayaita MAKINIKIA YA KITABU) kutoka kwenye kitabu husika. Na pia unapata kile kitabu nilichosoma na kuchambua.

Hivyo kwa kuwa kwenye channel hii, kila wiki unapata mafunzo hayo ya uchambuzi wa kitabu pamoja na kitabu chenyewe. Mafunzo yote unayapata kwa kwa mfumo wa nakala tete (pdf) na utaweza kuzitunza na hata kuzichapa kwa matumizi yako ya baadaye.

Hivyo kama huna muda wa kusoma kitabu kizima, unaweza kusoma uchambuzi wake, ambao utakusaidia sana kuweza kupiga hatua kwenye maisha yako.

Na kama hujui unapataje vitabu vya kusoma, unapata kitabu kila wiki.

Na kama huna fedha za kununua vitabu kila wiki, unapata chambuzi hizi na vitabu kwa kuwa ndani ya channel hii.

Na kitu kizuri ni kwamba, gharama ya kuwa kwenye channel hii ni sawa na bure kabisa, ni shilingi elfu moja pekee kwa juma. Hii ni sawa na kuninunulia mimi maji ya kunywa mara moja kwa juma, halafu unapata kusoma chambuzi za vitabu pamoja na kupata vitabu vyenyewe.

Karibu sana kwenye channel hii mpya ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA.

Channel hii ipo kwenye mtandao wa TELEGRAM, ambao ni mzuri sana kwenye kuhifadhi kumbukumbu za nyuma. TELEGRAM inafanana sana utendaji kazi wake kama ilivyo wasap.

Kwa kutumia channel ya telegram, mtu mpya anapojiunga anaweza kuona mafunzo ya nyuma tofauti na ulivyo mtandao wa wasap.

JINSI YA KUSHIRIKI KWENYE CHANNEL HII.

Kujiunga na channel ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA ni bure kabisa kwa wiki moja, ambapo utapata mafunzo hayo muhimu.

Baada ya wiki ya kwanza kuisha, kama utapenda kuendelea kuwa kwenye channel ya TANO ZA MAJUMA YA MWAKA utapaswa kulipia shilingi elfu moja (1,000/=) kila juma.

Hii ni ada ndogo ambayo itakuwezesha kuendelea kupata uchambuzi wa vitabu kila juma, kupata kitabu kilichochambuliwa kila juma na pia kupata mafunzo ya ziada (MAKINIKIA) yanayopatikana kwenye kitabu cha juma kilichochambuliwa.

Ada ya kuwa kwenye channel hii unaweza kuchagua kulipa kila wiki, au ukalipa kwa mwezi, miezi mitatu, sita au mwaka mzima. Na kadiri unavyochagua kulipa ada ya muda mrefu ndivyo ada inavyozidi kupungua na kuwa nafuu zaidi kwako.

Kama unalipa kwa wiki basi siku ya kulipa ni siku ya kwanza ya wiki ambayo ni jumatatu. Kila jumatatu utalipia tsh elfu moja (1,000/=) ili kuendelea kupata mafunzo kwenye channel hii.

Kama utalipa kwa mwezi basi utalipa siku ya kwanza ya mwezi ambayo ni tarehe moja ya mwezi husika. Kila tarehe moja ya mwezi utalipia tsh elfu tatu (3,000/=) ambayo itakupa nafasi ya kujifunza kwa mwezi mzima. Ukilipa kwa mwezi unaokoa shilingi elfu moja mpaka elfu mbili.

Na kama utachagua kulipa kwa mwaka mzima ili usisumbuke kutuma kidogo kidogo kila wiki au kila mwezi, itakuwa bora zaidi kwako. Kila mwanzo wa mwaka utalipa tsh elfu thelathini (30,000/=) ambayo itakupa nafasi ya kujifunza kwa mwaka mzima. Ukilipa ada ya mwaka unaokoa tsh 22,000/= ukilinganisha na kulipa kila wiki.

NAMBA ZA KUFANYA MALIPO.

Kujiunga na channel hii ni bure kwa wiki ya kwanza, hivyo tuma ujumbe kwa njia ya telegram kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na kwamba unapenda kujiunga na TANO ZA JUMA.

Baada ya wiki ya kwanza kuisha, utachagua kama utapenda kubaki na kuendelea kupata mafunzo haya ya uchambuzi wa vitabu na tano za juma. Kama utachagua kubaki na kupata mafunzo, utachagua unalipia kwa kipindi gani na hapo unafanya malipo na kuendelea kuwa ndani ya channel.

Malipo ya kujiunga na kupata mafunzo ya channel ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA, yafanyike kwa namba zifuatazo;

MPESA; 0755 953 887.

TIGO PESA/AIRTEL MONEY; 0717 396 253.

Ukishatuma malipo, tuma ujumbe kwa telegram kwenda namba 0717396253 ukiwa na majina yako na kwamba umelipia TANO ZA JUMA.

Karibu sana kwenye channel hii ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA, hii ni channel yako ya kupata uchambuzi wa kina wa vitabu, kuondoka na hatua za kuchukua ili maisha yako yawe bora zaidi.

Kujiunga na channel ya TANO ZA MAJUKA 52 YA MWAKA, tuma ujumbe kwa kutumia TELEGRAM kwenda namba 0717396253 na utaunganishwa bure kwa wiki moja na baada ya hapo utachagua kama utalipia kwa wiki, mwezi au mwaka.

JINSI YA KUPATA TELEGRAM KWA WASIOKUWA NAYO.

Kwa wale ambao hawatumii telegram au hawajui jinsi ya kuipata, ingia kwenye playstore au appstore ya simu yako na tafuta TELEGRAM MESSENGER kisha ipakue na kuinstall kwenye simu yako. Utaandikisha namba yako ya simu na ukishaiweka nitumie ujumbe kuja namba 0717396253 wa TANO ZA JUMA na nitakuunga kwenye channel.

Pia kama nuna simu yenye uwezo wa kuweka app. Unaweza kutumia telegam kwenye kompyuta moja kwa moja. Ukiingia kwenye tovuti yao; https://desktop.telegram.org utaweza kupakua telegram ya kutumia kwenye kompyuta. ukifungua link hiyo bonyeza sehemu ya GET TELEGRAM FOR WINDOWS au mfumo mwingine unaotumia, na utaweza kuipakua na kuweka kwenye kompyuta yako. Ukishaiweka kwenye kompyuta yako unaandikisha namba ya simu na utakuwa tayari kutumia.

Karibu sana tujifunze kwa pamoja kupitia usomaji na uchambuzi wa vitabu.

Wako rafiki katika safari ya kufikia mafanikio makubwa,

Kocha Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha